Joseph Mbiliyi (Sugu) awaumbua CHADEMA, akiri walichelewa Uwanjani kumuaga Mzee Mkapa

Chadema kufuata ratiba tu hawawezi,

Wanaweza endesha nchi kweli??
 
kwahiyo hata kenya,Rwanda, Uganda,walichelewa ila Burudi tu ndio walio wahi?
 
Makene anasema vingine kabisa. Ahh mambo haya balaaaa. Nani ni nani hapo.
 
Hii ni kweli kabisa.
Hata Kama Wakoloni hawakujilimbikizia Mali zisizo na faida kwa umma kama wanavyofanya watawala wetu na CCM wanavyofanya Leo.
Wanashindana kutumia fedha za umma kujenga mahema utafikiri wataishi milele. Bora wangeanzisha viwanda vikatoa ajira kwa wananchi.
Bora wangeanzisha mashamba makubwa yakatoa ajira.

Ubinafsi mtupu.
Kila mmoja anawaza kujenga kijijini kwake kwa kutumia fedha za ofisi ya umma. Huku ni kuendekeza ukabila na sio utaifa. Wenzetu wana maeneo rasmi ya viongozi wa umma na hata maeneo ya kuzika viongozi wa Umma .
Sio kila MTU kijijini kwake na kaburi lake. Serikali inapata gharama kubwa kulinda maeneo yasoyo na uzalishaji zaidi ya magofu ambayo hata watoto wao hawakai.

Afrika tumelogwa kwa ubinafsi.
Walijimilikisha nyumba zote za umma zilizokuwa maeneo bora kabisa lakini haikutosha wanataka na vijiji vyao viwe ni maeneo rasmi ya makazi yanayohudumiwa na kodi ya walalahoi wanaoishi kwa mlo mmoja kwa siku.
Woga wao ni kuhisi kuwa ipo siku wataishi maisha yao halisi kwa vipato vyao bila kubebwa na serikali. Lakini wamesahau kuwa watakufa siku moja na ufahari wao na kila aina ya dhulma waliyoihubiri na kuisimamia vitakua vimefika mwisho na waliojiona bila wao kuwa madarakani nchi haitatawalika watakua wamefikia mwisho na nchi itasonga mbele kizazi baada ya kizazi.

Haki huinua Taifa.
Tundu Lisu Mungu amjalie siku moja afikie mahali watu wamsifu Mungu kwa Wema wake. Hakika ni muujiza unaoishi. Ifikie mahali aondoe aibu awaite waandishi wa habari awaonyeshe Makovu ya Risasi yaliyopo mwilini mwake aliyoyapata kwa ajili ya kutetea hoja zake kwa mdomo aliopewa na mwenyezi Mungu.
Simuungi Mkono Mbowe kamwe kwa uovu anaoufanya ndani ya Chadema akishirikiana na Waovu ndani ya CCM wanaowaza fedha na Kujilimbikizia Mali kupitia Siasa Lakini napinga sana wale wasiojulikana Waliofanya unyama kwa Tundu Lisu MTU Wa watu na asiye sita kusema ukweli anaouamini.

Kuna vichaa bado wanamsakama Lisu kwa ajili ya kutetea mifumo miovu ya Kidhalimu na ubeberu wa watu weusi ndani ya CCM.Hao watatuletea shida sana kwenye nchi mana kizazi kipya hakiipendi CCM zaidi ya Wazee na Wajumbe wao.

Tumemuomba Mungu Korona ikatoweka sasa tumwombe Mungu amalize Tatizo la wakurugenzi kutuletea huzuni na vurugu na hata vifo na majeruhi kwa sababu ya kubadili matokeo ya uchaguzi. Hili ni tatizo kama ilivyo Korona. Linatugawa na kutupa viongozi waovu wabaowaza dhulma na rushwa ya madaraka kwa ubinafsi wao huku wakijisahau kuwa wao nao ni binadamu watakao toa hesabu zao mbele za Mungu siku moja.
 
Chadema uache utoto na kulialia
Walitaka waingie mwisho ili kuinua watu majukwaani
Sijui mshauri wao Ni Nani hawa wahuni
 
Mungu ataiondoa CCM kama alivyoiondoa Corona TZ
 
Ilikuwa hivi. Kulikuwa na hisia kwamba huenda Liisu akiingia uwanjani na viongozi wa Chadema kwenye kuaga mwili wa Mkapa watu wangelipuka kwa kelele na vifijo, na hiyo ingempa kiki sana ya kisiasa ukizingatia vyombo vya habari vilikuwapo na Watanzania wengi walikuwa wakiangalia tukio hili kupitia television.

Basi uamuzi ulifanywa kwamba hilo lizuiwe kwa namna moja au nyingine.

Ndipo pendekezo likatolewa. Chadema wapewe muda wa kufika uwanjani ambao utawafanya wafike baada ya Raisi Magufuli kuingia, na hivyo waambiwe kwamba hawaruhusiwi kuingia. KIla mtu akashangilia jinsi mpango huo ulivyokuwa wa kijinias!

KIlichofuatia ni utekelezaji.

Lakini tuawaambie wazi wale waliopanga mpango huu - kwamba nadhani inafikia mahali mnavuka mpaka katika kukabiliana na upinzani. Huu ni utoto na uonevu. Mnamwogopa Lisu?
 
Ngumu kumeza
 
Waambie
 
Umemalizaaaaaah
 
Hakuna binadamu aliye sahihi, hajazaliwa bado
Hata usiseme hivyo! Mimi tu Nyarusare ndiyo siyo mnafiki Duniani, sIjawahi kuwa mnafiki , na sinto.. tatizo ni wale wanao niona mimi ni Mnafiki, na kutafakari akilini na Myoyoni mwao hivyo wanionavyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…