Joseph Musukuma: Kikokotoo kinawaumiza wananchi, tunatengeneza taifa la wezi

Nani alikuambia wafanyakazi wa serikali ukiacha wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaishi ktk nyumba za serikali bure?. Hata hao wengine tunao wanaishi huku mitaani wamepanga. Walio ktk nyumba za serikali waliobakia hulipa 10%:ya mishahara kulipia kodi. Barua zao zote za ajira hazina kipengele cha kupewa nyumba ya serikali. Wanaobahatika kupewa nyumba ni wale wakuu wa wizra, vitengo ambao ni wachache sana na mara nyingi wanatokea ktk nyumba za kupanga kabla ya UTEUZI.

Hawa huwa hawana uwezo wa kujenga nyumba ktk miaka 30 wanayifanyakazi mpaka wanapostaafu. Vitu muhimu ni kuwa na familia kuikuza kiafya na elimu kwa mishahara midogo wanayopata.

Wanapostaafu ndio hupata pesa ya kujenga kajumba. Ndio sababu wanalalamika kulipwa 33% ya kiinua mgongo halafu ile pesa ya pensheni ya kila mwezi wanapata mwisho miaka 72. Hapo unaachwa ufe. Wakubwa wanaendelea kulipwa mpaka wafe kwa kikotoo cha zamani. UMEELEWA?
 
Kiongozi embu tuwe wa kweli

Mtu anaishi nyumba ya serikali rent mtaani nyumba anayoishi tena sio prime area labda laki 5-7 kwa mwezi. Ndani ya mwaka anaokoa million sita mpaka nane. Mafuta gari ya kazini kwa mwezi labda matumizi yake binafsi ni łąki mbili mpaka tatu, anaokoa millioni mbili mpaka tatu ukijumlisha ndani ya mwaka, mshahara million tatu plus kwa mwezi.

Kwa mwaka anaokoa kama 8-10 million kwenye mshahara wake. Halafu unakuta mtu private na mshahara wa millioni nne au tano kabla ya 40 years ana nyumba yake bila hizo ‘benefits-in-kind’ za watumishi na wenyewe wana ndugu hao hao wakuwasaidia na kusomesha.

Ifike wakati watu waambizane ukweli, uwezi kufanya kazi zaidi ya miaka 20 serikalini huku ukipokea benefits zote hizo usiwe na nyumba hata kama hukua mpiga deal.
 
Hata 10% ya kodi bado wana save kiasi kikubwa ndani ya mwaka kuweza kujenga taratibu kwa miaka 20. Iweje private kwa mishahara hiyo waweze halafu wao washindwe.
 
Nilichogundua mpaka hapa, wewe ni mfanya biashara, na kanuni ya biashara, ni uchoyo uliopitiliza kiwango cha utu

Inasemekana, ili ufaulu katika biashara, umeamka na miliono 20, mpango wake ni kuongeza na kupanua biadhara, hata ikitokea mzazi wako yuko taabani anahitaji elfu kumi kutoka kwenye m.20, usitoe, labda umtafutie kwingineko, na ikitokea umekosa, bora mzazi afe ili biashara iende

Mkuu, bado tuna nchi yenye watu masikini mno, 50k ya mshahara ya mtu mmoja kwenye jamii ya watu 10 masikini hawezi kujenga mpaka mafao aisee
 
Aijalishi unafanya shughuli gani jukumu la ‘personal finance’ ni lako. Kila mtu kwa situation yake anatakiwa kupanga goals za mbeleni especially watu walioelimika kama waajiriwa wa serikalini.

Hawa watu wanakuwa na advantages nyingi during their working life isipokuwa they make poor financial decisions or live reckless lives wakitegemea pension kama mwokozi ndio maana wanataka rules zao kwenye malipo badala ya kujipanga mapema.

Pension inatakiwa ikusaidie usipate tabu wakati wa kustaafu hiyo withdrawal ya 33% ndio muda wa kwenda mbugani au hata kwenda Kenya na mkewe/mume mtu anawaza kujengea au kuanzishia biashara.
 
Hayo uliyoandika ndio mkataba wao na serikali ulivyokuwa? Mkataba wa hao wazee na serikali ni kwamba wewe serikali changia 15% na Mimi mfanyakazi nachangia 5% na hizo Hela ni mali ya mfanyakazi.
 
Hayo uliyoandika ndio mkataba wao na serikali ulivyokuwa? Mkataba wa hao wazee na serikali ni kwamba wewe serikali changia 15% na Mimi mfanyakazi nachangia 5% na hizo Hela ni mali ya mfanyakazi....
Wafanyakazi wanalipwa kwa kodi za wananchi

Wapi wananchi walishirikishwa huo mkataba?

Huo wizi kabisa ni mkataba wa kifisadi wa kuiba pesa za walipa kodi.Haiwezekani mtu alipwe mshahara halafu umwambie nitakulipia pia Pension asilimia 15 wewe utachanga asilimia tano tu.Huo mkataba ni wa kifisadi kati ya serikali na wafanyakazi wake ufutwe upesi na kwenye kikokotoo hiki kipyac iondolewe hiyo asilimia 15.Walipwe kwa hizo asilimia 5 zao tu walizochangia

Kama serikali imeamua kulipia pension wananchi wake kwanini ibague wananchi mbona serikali haiwalipii pension hata asilimia moja tu kila mwezi wanaozalisha mazao yanayoingiza pato la pesa za kigeni na za ndani wanaopinda migongo kila siku ?
Hawa wakulima miaka 55 wanakuwa wamechoka sana wanastahili kudtaafu kilimo nao kwa nini serikali haichangii pension huko?

Wizi huo mkataba utenguliwe haraka ni wa kifisadi.Serikali na wafanyakazi wameamua kukubaliana kuibia wananchi
 
Mkuu, watu wanalalamika sababu mishahara ni midogo sana.
Toka jana, nilikuambia kunauwezekano hufahamu salary scale za watumishi wengi wa serikali.

Ungekuwa unafahamu, nadhani usinge thubutu kusema watumishi ni wazembe, haiwezekan aslimia 80 ya watumishi wawe wazembe? haiwezekani!

Tatizo kubwa ni kuwa mishahara ni midogo sana, saaana! how do you save If gross ni Tsh 720K then hapo ukatwe, PAYE, PSSF,HESLB,NHIF unabaki na 500 au 400+K, how can this amount be saved??

And mostly hiyo take home is for financing chakula, ada,and rent!
 
Hiki kikokotoo ndicho kitakachoiondoa serikali ya kifisadi ya CCM madarakani mwaka 2025 misa ya kwanza tu. Hawa mbwa wanatusumbua sana.
 
Vitu ratio ya hali ya maisha na kiwango cha mishahara uko nchi ulizotolea mfano ni sawa na hapa kwetu?
 
Tulia sindano ziingie wewe. Hizo 15% ni zile ambazo serikali inawaibia watumishi wa umma kwa kuwapunja mishahara yao. Sasa wanaamua kuzirejesha kwa mlango wa nyuma. Hata hizo 15% ni ndogo sana walipaswa waongeze hadi 30%. Unafurahi sana unapoona watu wakidhulumiwa haki yao. Mchawi mkubwa!
 
Elimu yetu imeshindwa kutusaidia, Bunge Lina watu wanaojiita wasomi ila hakuna wanachoisaidia nchi, mtu kama Msukuma mnaomwita Kilaza sio msomi ndio anaongea vitu vya kueleweka kuliko hata hao wanaojiita wasomi
Mkuu wasomi na usomi ni vilaza na ukilaza wenyewe , wasomi wengi wamefungwa kwenye fikra za watu wengine( vitabu).
 
I get it kuna struggle in the beginning but then salary inapanda over the years. Unapostaafu bado una faida pension inakuwa-calculate kwa kuangalia mshahara wako wa mwisho sio mwanzo.

So automatic unafaidika maana michango ya mwanzo ni kidogo na ndio miaka mingi, wakati calculations za malipo zinaangalia miaka ya mwisho hiyo hela ya nyongeza pension fund lazima wajue wanaitoa wapi.

Halafu kwenye jamii walau watumishi wana-pension, si ajabu wote mke na mume.

Huku kuna watanzania wengi sana with degree qualifications hawana ajira, zikitangazwa ajira kuna wakati walijaribu kufanya usaili uwanja wa Mkapa nusu ulijaa vijana.

Ili watumishi wapate hiyo pension yao serikali inatumia resources nyingi sana, bado kuna changamoto za pension investments to how they work hadi ulipwe average ya miaka ya mwisho na wao wana changamoto zao za ‘cash-flow’.

Sasa sidhani kama serikali ime set hiyo withdrawal ya 33% kwa intentions za kuonea watu ni kwa sababu ya uhalisia wa cash-flow za mfuko na available liquidity ya kila mwaka ili waweze kukidhi kulipa (story ni ndefu to how they increase their financial assets).

Jaribu kufikiria kwa mwaka kama kuna wastaafu laki moja tu huo mzigo wa malipo sio mdogo na kila mtu analipwa kwa average ya mshahara wake wa mwisho. Kila mtu akichukua 50% ya lump-sum withdrawal sidhani kama watabaki na kitu. Na uwekezaji wao mara nyingi pension funds ni kwenye bonds za miaka mingi hizi taasisi kawaida hazina liquid assets banks wana value tu za bonds na source kubwa ya hela zao interest earned.

Jumlisha na white elephants projects kibao za pension funds ambazo zimechukua hela nyingi ambazo hazirudi kwa haraka kwa hivyo mfuko financial una struggle that’s just common sense.

Ni hivi kuna changamoto na CAG anazielezea mara kwa mara kwenye report yake, serikali imekuja na utaratibu ambao wanadhani wanaweza mudu watu hawataki kuelewa, halafu anatokea huyo msukuma anataka mpaka mijitu iliyokuwa na uwezo wa kujenga katika muda wao (wale ambao wameishi nyumba za serikali waibe kama serikali aiwezi wapa 50%).

Binafsi naona watumishi ni ungrateful
 
Vitu ratio ya hali ya maisha na kiwango cha mishahara uko nchi ulizotolea mfano ni sawa na hapa kwetu?
Hiyo posts inaongelea watu wanaokaa nyumba za serikali na wanaopata marupurupu tele, halafu wanastaafu bila ya kujenga. Sasa hawa kutokujenga alaumiwe serikali pia.
 
Kwa mtazamo wako huu, wastaafu wote wa mafao walikuwa wanakaa nyumba za serikali au za bure wakiwa kazini?
Hapana labda nazungumzia hoja ya msukuma leo. sijasema watumishi wote wanakaa nyumba za seriali au ata wana-magari ya serikali.
 
Ndio sasa akistahafu alipwe chake .........unampatia 30% halafu hiyo 70% unabaki nayo.....akifariki ndio basi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…