Uchaguzi 2020 Joseph Selasini, aviangukia vyama kuwasamehe vijana walioshindwa kura za maoni baada ya kuvihama vyama vyao

Uchaguzi 2020 Joseph Selasini, aviangukia vyama kuwasamehe vijana walioshindwa kura za maoni baada ya kuvihama vyama vyao

Huyu Selasini tangu alivyoleta bungeni hoja ya ombi kwa wanaume wa Kenya wakuwasaidia kingono wake za watu huko Rombo nimempunguza pakubwa sana! Ni tapeli wa siasa haaminiki!
 
Huyu mzee ni mpumbavu aliyepindukia. Mods nisameheni. Kwa iyo siasa zinazobeba hatma ya maisha yetu watanzania yeye anataka tuzichukulie kama fursa za kimaisha?????

Huyu mtu bora aliondoka Chama makini chadema. Kwa akili hizi anastahili kuwepo huko NCCR au CCM ambalo watu wanachukulia hatma za maisha zetu kama fursa zao za kiuchumi.

Kanipa hasira sana. Ndo mana nchi hii hatuendelei kwa kweli. Akili kama hizi hazitakiwi kabisa kuwepo kwenye kada ya uongozi
Pole mkuu
 
Yeye alihama CHADEMA kwenda nccr kwa mbwembwe, hivyo naye anaomba asamehewe arudi CHADEMA au wanaotangatanga ni vijana peke yao?!
 
Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini, ameviomba vyama vyote nchini kuhakikisha vinawapokea vijana wote waliohama vyao vyao na kuhamia vyama vingine lakini wakashindwa kwenye kura za maoni kwa kuwa walishaonesha wanao uwezo wa kufanya kazi.

Selasini ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 7, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na kuongeza kuwa vijana hao wanapashwa kuwapokea na kisha kuwalea na kuwarekebisha kwenye makosa yao na kuwapa nafasi za uongozi.

"Naviomba vyama vyote, chama changu cha NCCR-Mageuzi, CCM, CHADEMA tusiwatupe vijana, hata vijana ambao walihama kutoka CHADEMA kwenda CCM wakaenda kushindwa kwenye kura za maoni, tunajua vijana wanavyotangatanga hata katika kutafuta uchumba, wanatafuta fursa fungueni milango hao vijana warudi waweze, kufanya kazi ya Watanzania" amesema Selasini.

CC: Lijualikali.
Kiongozi bora ni yule mwenye maono na msimamo thabiti. Hao vijana pamoja na Selasini wameonyesha wazi hawana sifa hizi. Waache wavune walichopanda.
 
Mtu ana 250M halafu bado unalialia nini?Hivi kujiajiri huwa anaimbiwa nani?mbona watu wakitemwa uongozi wanaanza kulia hovyo,Umeshapata exposure na mtaji kwanini usijiajiri na kuajiri wenzako.
 
Mtu ana 250M halafu bado unalialia nini?Hivi kujiajiri huwa anaimbiwa nani?mbona watu wakitemwa uongozi wanaanza kulia hovyo,Umeshapata exposure na mtaji kwanini usijiajiri na kuajiri wenzako.
Kuitwa Mheshimiwa nako ni raha
 
Huyu Meku katumwa?

Ama ni kiherehere chake tu?
 
Back
Top Bottom