Joseph Selasini: Mwaka 2020 Mbatia alitupeleka na Anthony Komu kwa Dkt. Bashiru Ally kufanya makubaliano na CCM

Wacha kiupepo hiki kiendelee kuvuma ili tuendelee kuona uchi wa kuku.
 
Reactions: EEX
Hawa chawa wa Ccm ndani ya upinzani wako wengi sana. Zitto, mr30, wote ni hao hao, wakiona wameshindwa ndionhuleta vurugu. Yaani mchawi lazima mwisho wa siku atakuambia tuu amekuulia mtoto.

Ona sasa 30 kaanza kujitaja.
 

Yap, kula tano mkuu, hapa umesema ukweli wa wazi, na tulisema kabisa kuwa Magufuli alivunja makubaliano yake na kina Mbatia na Lipumba, baada ya kuona kura za CDM zingemuumiza hata yeye. Akaona isiwe tabu bora apore uchaguzi kabisa, maana hata kuiba bado ingekuwa ngumu kwani akina Mbatia hawakuwa na mvuto wowote. Akaagiza usalama wa taifa waende na karatasi za matokeo fake na hayo ndiyo yatangazwe.

Ilifika mpaka mahali Mbatia anapangiwa sehemu za kwenda kufanya kampeni, na ujumbe gani awe anatoa. Baada ya Mbatia kuacha hewani ndio imebidi awaunge mkono cdm kwani huko ccm hana support yoyote.
 
Chadema mfuatilieni vizuri Selasini. Anaonyesha ni janja janja Sana. Atawagombanisha yeye anaondoka. Viongozi ifuatilieni hiyo card. Ikiwezekana anyan'ganywe abaki na Mbatia wake.

Pili chadema kuweni makini na hawa wawili wasibomoe chadema. Hata Mbatia simwamini sana.

Ila Selasini Kuna mchezo anacheza na hayupo peke yake. Hayo maisha tunavyoyaona huku mitaani tunasema ni utapeli.
 
Kwamba inawezekana kweli Mbatia alienda na kina Komu kwa Bashiru ndio maana Mbatia akaonekana akifanya mikutano nje ya eneo lake kwa uhuru bila kusumbuliwa na polisi, naamini hii ilikuwa ni ruhusa aliyopewa toka juu, akaenda mpaka Mbeya.

Huyu Selasini hapa ana hoja ya msingi hasa nikiunganisha na matukio yaliyopita, lakini nae kwanini hakuyasema haya wakati ule? atuambie waliahidiwa nini mpaka wakakaa kimya? nadhani aliambiwa atapewa ubunge ndio maana, hivyo hii hoja yake kwa wakati huu inakosa uzito.
 
Lissu alivutia umati upi wa watu!!? Unajitekenya na kucheka.
 
Tukisema kwamba upinzani ni Chadema peke yake nchi hii muwe munaelewa,Watu wanakokotwa kwenda kuisaidia CCM halafu mnategemea wawasemee
Hiihii CHADEMA inayotumiwa na Samia atakavyo, au kuna nyingine?
 
Shauri zenu mnaomwamini Joseph Selasini. Huyu ni msaliti kuanzia kwenye familia yao (hawakuelewana na kaka yake marehemu Masumbuko Lamwai hadi anakufa, baada ya mtafaruku wa NNCR wa kipindi cha Marando).

Hakuaminika Seminari alikofukuzwa na Askofu Pengo miaka ya 1980s, aliwahi kuiba gari ya THB miaka ya 1990s akiwa Transport Officer kwa kisingizio kuwa limeibiwa.

Hata mtaani kwake anakoishi haaminiki
 
Nimekuelewa kwa tabu sana, tatizo langu ni kitu gani kilisababisha ushindwe kuueleza Umma mambo hayo tokea mwaka 2020 hadi Sasa. Je, visambusa na chai za asali ndivyo tu mlivyoambulia au kuna vingine ?
 
Tukisema kwamba upinzani ni Chadema peke yake nchi hii muwe munaelewa,Watu wanakokotwa kwenda kuisaidia CCM halafu mnategemea wawasemee

una uhakika gani CDM sio mali ya CCM..

unaikumbuka NCCR mageuzi iliyoitoa pumzi CCM mpaka marehemu JKN jasho likamtoka, baada ya hapo Lyatonga yuko wapi?..
 
Mbona viingozi wa upinzani na wachagga tu nchi hii kasoro zitto na rungwe
Acha ukabila wewe, kwanini mnakua na hasira na wachagga kiasi hiki? Kwani wao sio waTanzania? Mtu kapigiwa kura na mikoa yote kwani hawakujua ni Mchagga?

Mie kabila la Mama Samia au Majaliwa hata silifahamu na hainihusu maana Halina msaada wowote kwenye utendaji wa mtu, sasa why bother na kabila la Mbatia au Lipumba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…