Mbunge mstaafu wa Chadema Dkt. Joshua Nassari ameomba radhi rasmi kwa Rais Magufuli kufuatia mambo maovu aliyomfanyia kabla hajahamia CCM.
Nassari ambaye alikuwa akiongea kimasai amewaomba radhi wanaccm na wana Arusha wote kwa machukizo aliyowasababishia akiwa CHADEMA.
Nassari amewataka malaigwanan na wamasai wote na wananchi kwa ujumla kumpigia kura Dkt. Magufuli.
Maendeleo hayana vyama!
====
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari ameomba kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuwa upinzani
Nassari alihamia CCM akitokea CHADEMA mwezi Julai 2020, miezi kadhaa baada ya kuvuliwa ubunge kutokana na kutohudhuria vikao vitatu vya bunge
Nassari amesema mambo mengi waliyokuwa wakiyasema alipokuwa upinzani yametekelezwa na Dkt. Magufuli katika muhula wa kwanza wa uongozi wake.