Joshua Nassari Kumwoa Halima Mdee?

Joshua Nassari Kumwoa Halima Mdee?

Waandike kwanza rahma mke mdogo wa jk!na wassira anaishi na mke wa nani?
 
Nassari usikurupuke mdogo wangu! Utakuja kujuta.
 
Hilo ndo habari leo bana, kwa ufukunyungu tu halijambo..! Kuandika mazuri mengne ya chadema e.g mifuniko ya kampen za chadema zilivyokuwa huko arumeru, kwenu mwiko aiseee...!
 
Ukiona mwandishi wa habari anaacha kuandika mambo ya msingi,na kuandika mambo ya utani na jokes basi ujue hilo gazeti ni la udaku.Hii habri ilipaswa iandikwe na ijumaa wikeinda,Sani nk..Sasa kama Habari leo nao wanaipa habari kama hii covarage ujue ni kuchanganyikiwa kwa waandishi wa magazeti ya serikali na Chama Cha Matusi aka CCM.Uwezi kutarajia kuwa Halima Mdee au Joshua Nassari waongee maneno yale wakiwa wanaamnisha hasa mbele ya kadamanasi..

Nani asiyejua kuwa Halima Mdee ni charming Women? Nani asiyejua kuwa Halima Mdee ni msela(Mshikaji)? Nakumbuka kwenye kampeni zake kule Kawe Halima alikuwa anawaambia wananchi hasa vijana kuwa "Masela hati mie nimepigika ile mbaya,tuwaondoe CCM kuondoa kupigika huku" Nani asiyejua kuwa Joshua Nassari ni msela(mshikaji).Hii ilikuwa ni moja ya vibweka na vijimambo vya kushangilia ushindi,sasa kama hata jambo dogo kama hili linatushinda kuligundua basi tuna safari ndefu.
 
Huenda wanajua wazi yaliyosemwa ni utani. Na wanajua Joshua anamchumba na Halima naye vivyo.

Sasa wanataka kuwamaliza hawa wanasiasa vijana, hazina kwa CHADEMA lakini mwiba kwa CCM. Si mnajua unapotokea mgogoro kati ya. Wapendanao hata ufanisi na tija hushuka sana.

Watch out Joshua and Halima!!
 
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

"Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo," alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

"Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi," alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.

"Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili," alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu'.

Source; Habari Leo
Nilidhani ni habari kutoka kwenye chombo cha habari,kumbe ni Habari leo
 
mimi ni cdm lakini nisingependa hilo kutokea. Nassari atafute wake, na tuchukulie hilo lilikuwa ni utani tu. After all mdee ni mkubwa sana kwa nassari
 
Inawahusu nini hata kama wakiamua kuoana!!!! Kama wamekosa habari za kuandika waende kuwafumania vigogo watoe habari zao kwenye magazeti nyambafu.
 
......nadhan lishaanza kupoteza dira,ni bora tujue kwaba ni gazeti la udaku tulitoe kwenye roaster.
 
:rockon:wabongo tutofautishw utani wa watu wakiwa wamejawa na furaha,kwake ni dadaake!
 
Labda Halima atahamia Arumeru, hatuwezi jua.
Kwa mujibu wa mila na desturi ninazozikumbuka mimi a woman follows a husband na ndio maana walimu wanapenda kuolewa na wanaume wa mjini ili wapangwe shule za town
 
Frankly speaking mi inaniuma sana seeing the Habari Leo going like this coz nilishiriki kwa namna moja au nyingine kuliingiza sokoni wakati linaanzishwa.....Damn!
 
Huyu mwandishi ni kilaza,he/she can't dffrntiate btn jockes and reality. Halafu news yenyewe wameipa front page. Mbugilautine hawa.
 
Back
Top Bottom