Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi naona poa tu, au mnataka akaolewe na LucyNde aka kibajaj aka kudadadeki!!!
Nassari usikurupuke mdogo wangu! Utakuja kujuta.
Nilidhani ni habari kutoka kwenye chombo cha habari,kumbe ni Habari leoMBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
"Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo," alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.
Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
"Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi," alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.
Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.
Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.
Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.
"Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili," alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu'.
Source; Habari Leo
Nassari usikurupuke mdogo wangu! Utakuja kujuta.
Are you marriage councilor or psychic?Nassari usikurupuke mdogo wangu! Utakuja kujuta.
Kwa mujibu wa mila na desturi ninazozikumbuka mimi a woman follows a husband na ndio maana walimu wanapenda kuolewa na wanaume wa mjini ili wapangwe shule za townLabda Halima atahamia Arumeru, hatuwezi jua.