Joto la sasa la Dar linaweza vunja rekodi

Joto la sasa la Dar linaweza vunja rekodi

Nimeenda kumtembelea Manzi mmoja hivi maeneo ya Kigambon huko.

Aisee kuna joto la kufa mtu imenibidi nioge mara 3 ndani ya masaa mawili...

Mvua iliyonyesha haina faida kwa wakazi wa Dar zaidi ya hasara tu
Hili joto ni hatari mzee, nashinda bafuni kama chura, kila saa kwenye maji. Maajabu ya sasa ni kila nikitoka kuoga na jasho linatoka hapo hapo.
 
Binafc nilishangaa hiyo AC na fan kwa unit tano,natumia almost unit 4 kwa siku mataa ya nyumba fridge mbili na tv tu na kuchaji cm tu yani nilikua nafikiria kua na AC kama ingekua unatumia kiwango
Niliingia lodge nikalipa 20k, kuanzia saa kumi jioni hadi kesho saa nne na nimewasha kipupwe, inamaana wanakula loss?
 
Vyumba vitatu AC tatu, sebulen feni tatu plus friji. Nyumba niliyotoka nilikuwa natumia unit 3 tu kwa siku.
Ukiamua kubisha bisha tu ni haki yako
Acha uongo, Mimi sina AC na natumia hizo unit 6 Kwa 24 hours.
 
Mimi nilidhan shida iko kwenye hii nyumba mpya niliyohamia maana hata mvua inyeshe bado kuna joto.
Yani sasa hivi natumia unit almost 5 hadi 6 kwa siku maana mafeni na AC ndani ya nyumba zinawashwa muda mrefu.
Kumbe hata kwa wengine hivyo hivyo.
Kwa kweli hili joto ni balaa na sasa ilipaswa walau kuwepo baridi kidogo
Shida iko kwenye mipango miji. Uzembe wa kujenga kwa mpango ni janga ambalo kila mkazi na mgeni wa Dar atalilipa kwa gharama kubwa. Japo kweli Dar iko ukanda wa joto lakini hali imezidishwa na kujenga holela bila kuacha open spaces, kujenga kwa nafasi na kupanda miti mingi. Uzembe wa wananchi kuacha viongozi kufanya watakavyo unatu-cost. 1. Joto 2. Mafuriko 3. Magonjwa 4. Foleni ya magari 5. Kelele. Mwisho wa haya yote utakuwa ni kukubali kuwa tulifanya makosa na kubomoa (japo ni muda mrefu sana)
 
Joto la kawaida sana hilo...

Watu wa kusini au kaskazini mwa dunia, summer zao huwa zinakuwa na fukuto zaidi ya hilo...

India kipindi cha joto kuna watu huwa wanafariki sababu ya joto kali, watu wanaoishi karibu na mito huwa wanajiloweka tu mitoni...
Hili siyo joto la kawaida asikudanganye mtu, ni kama Mwaka Jana Uingereza Kwa mara ya Kwanza joto lilizidi mpaka mataili ya magari yakawa yanayeyuka.

Yani hapa Kwa tusiokuwa na AC inabidi umtowe wife kidogo hotel ili uweze kula tunda, feni halifui dafu.
 
Shida iko kwenye mipango miji. Uzembe wa kujenga kwa mpango ni janga ambalo kila mkazi na mgeni wa Dar atalilipa kwa gharama kubwa. Japo kweli Dar iko ukanda wa joto lakini hali imezidishwa na kujenga holela bila kuacha open spaces, kujenga kwa nafasi na kupanda miti mingi. Uzembe wa wananchi kuacha viongozi kufanya watakavyo unatu-cost. 1. Joto 2. Mafuriko 3. Magonjwa 4. Foleni ya magari 5. Kelele. Mwisho wa haya yote utakuwa ni kukubali kuwa tulifanya makosa na kubomoa (japo ni muda mrefu sana)
Joto lililopo halihusiani na hiki ulichoandika, Dar kuna kipindi tabia ikibadirika huwa tunajifunika duveti kabisa na baridi unaisikia.

Hii ya sasa NI noma, ndio watu wenye mitaji wazione hizi fursa na kujenga community swimming pool kila Kata unapinga pesa mpaka utashangaa.

Mamtoni summer time community swimming pool zinafunguliwa, hata joto likizidi kila kata wana pool Lao la kuenjoy na kupooza miili.
 
Of course siyo watu wote wanaoweza kuona uhusiano wa nilichondika na hili joto ndiyo maana mji umejengwa bila mpango kama ilivyo sasa. Sorry!
 
Ilisemwa mwaka 2023 ndio mwaka ulivunja rekodi kwa kuwa na joto kali.

Tutegemee mwaka 2024 nao kuelekea hukohuko.
 
Back
Top Bottom