Joto la sasa la Dar linaweza vunja rekodi

Joto la sasa la Dar linaweza vunja rekodi

Vyumba vitatu AC tatu, sebulen feni tatu plus friji. Nyumba niliyotoka nilikuwa natumia unit 3 tu kwa siku.
Ukiamua kubisha bisha tu ni haki yako
AC 3 utumie Unit 6, hivi wajitambua kweli?
Friji yenyewe tu hutumia zaidi ya Unit 1 kwa siku.

Feni ikiwaka masaa 18 inatumia Unit 1
AC ya BTU9000 hutumia zaidi ya 0.7kw kwa saa sasa wewe hizo 3 huoni watudanganua?
 
Noma sana. Mimi nlipokuwa natafta nyumba nikakuta hii nyumba ina ac na feni kila chumba na budget iko ndani ya budget nikafurahi ila sasa naona haya masuala ya umeme yanafanya matumizi yangu yaongezeke.
Mkuu mimi sijawahi tumia zaidi ya unit 3 toka nimeanza kuishi sema pia kipindi hicho sikuwa na familia kubwa.
Mpangaji unahama nyumba moja unahamia nyingne, Mungu umeninusuru na hili.
 
Dar Raia zinateseka sana

Raia zinapelekewa moto kweli kweli,utadhani zimebandikwa kwenye sufuria
 
Acha uongo dogo, AC moja ndani ya saa kumi na mbili inakata vizuri kabisa unit kuanzia 50 hadi 80 wewe hizo AC umezitoa wapi
Kiongozi mimi nimefunga A/C chumbani kwangu nnafeni vyumba vya watoto na friji umeme wa 5000 kwa siku unaisha ambapo ni unit 14 kwa siku sasa huyu ananiambia unit tatu kwa siku ? Aisee maana nimefatilia kama utawasha A/c masaa yote na vitu vingine basi kila lisaa inaweza ikala unit moja
 
Jana ilibidi niweke maji ya baridi ndio niogee. Wakati mwengine unajiskia km roho inaacha mwili
 
Sio kweli hiki ndo kipindi Cha joto Kuanzia mwezi wa 9 mpk kipindi Hadi tunaanza masika ndo joto linaanzia kupotea
Isipokuwa joto la mwaka huu limezidi viwango
Kila kitu cha mwaka 2023 kimezidi, baridi ilikuwa mpk watu wanaomba iishe, zikaja mvua ndio hizo mpk zimondoka na roho za watu na hili joto ndio komesha. Limekuja na homa watu wanajifia tu. Malaria zimepamba moto
 
Joto kali linaanza mida ya saa 5 asbuhi hibi, 6, 7, 8 ni balaa then linaanza kupungua..jioni kunakuwa na kiupepo fulani hivi....hatari sana
 
Back
Top Bottom