Niliwahi ambiwa na babu kuwa mwanamke si wa kuamini akanipa kisa flani hivi; kuna jamaa alikua akisumbuliwa na mbwa wa jirani yule mbwa alikua na tabia ya kuua vifaranga vya kuku sasa akawa anamwinda ili ikiwezekana amuue, siku moja kukiwa na kigiza akasikia kitu kinatikisa majani ya mahindi kuja kwake jamaa alipo sikia mahindi yanatikisika akachukua rungu akampiga nalo akijua ni mbwa wa jirani kumbe ni mtoto wa huyo jirani na akafa palepale.
Alipogundua kuwa alichopiga si mbwa bali ni mtoto wa jirani akakimbia kwenda kumwambia mkewe tukio, basi wakakubaliana wafiche maiti ili ikifika usiku sana wakautupe mbali ili isijulika mtoto kaenda wapi, wazazi wa yule mtoto walimtafuta mtoto wao bila mafanikio.
Ilipofika usiku wa manane wakakubaliana wakamzike mtoto mbali huko vichakani, walimzika wakarudi maisha yakaendelea. Kwa bahati nzuri jamaa akaenda akamsimulia ndugu yake kilichompata nae ndugu yake akamuuliza kama mkewe anajua nae akamkubalia huyo ndugu yake akamwambia kama Mke anajua basi afanye jitihada usiku tena akahamuamishe huyo marehemu akamzike sehemu nyingine mbali anayojua mwenyewe Kwa sababu mwanamke si wa kuamini.
Na jamaa akafanya alivyoelekezwa na ndugu yake, siku zikapita nyingi baada ya tukio siku moja kukatokea ugomvi jamaa akampiga mkewe mwanamke akakimbilia polisi kusimulia kila kitu.
Polisi wakamkamata jamaa na mwanamke akawapeleka hadi walipomzika huyo mtoto lakini hawakumpata.
Huyu kaambiwa asipost yeye mbiyo kupost.