Joyce Kiria arudi kimya kimya kwa mumewe baada ya kumdhalilisha mitandaoni

Niliwahi ambiwa na babu kuwa mwanamke si wa kuamini akanipa kisa flani hivi; kuna jamaa alikua akisumbuliwa na mbwa wa jirani yule mbwa alikua na tabia ya kuua vifaranga vya kuku sasa akawa anamwinda ili ikiwezekana amuue, siku moja kukiwa na kigiza akasikia kitu kinatikisa majani ya mahindi kuja kwake jamaa alipo sikia mahindi yanatikisika akachukua rungu akampiga nalo akijua ni mbwa wa jirani kumbe ni mtoto wa huyo jirani na akafa palepale.

Alipogundua kuwa alichopiga si mbwa bali ni mtoto wa jirani akakimbia kwenda kumwambia mkewe tukio, basi wakakubaliana wafiche maiti ili ikifika usiku sana wakautupe mbali ili isijulika mtoto kaenda wapi, wazazi wa yule mtoto walimtafuta mtoto wao bila mafanikio.
Ilipofika usiku wa manane wakakubaliana wakamzike mtoto mbali huko vichakani, walimzika wakarudi maisha yakaendelea. Kwa bahati nzuri jamaa akaenda akamsimulia ndugu yake kilichompata nae ndugu yake akamuuliza kama mkewe anajua nae akamkubalia huyo ndugu yake akamwambia kama Mke anajua basi afanye jitihada usiku tena akahamuamishe huyo marehemu akamzike sehemu nyingine mbali anayojua mwenyewe Kwa sababu mwanamke si wa kuamini.

Na jamaa akafanya alivyoelekezwa na ndugu yake, siku zikapita nyingi baada ya tukio siku moja kukatokea ugomvi jamaa akampiga mkewe mwanamke akakimbilia polisi kusimulia kila kitu.

Polisi wakamkamata jamaa na mwanamke akawapeleka hadi walipomzika huyo mtoto lakini hawakumpata.

Huyu kaambiwa asipost yeye mbiyo kupost.
Mbona naona siku hizi amebadilika sana.
Siku za nyuma,mapenzi yakivyokuwa moto alikuwa akipigwa Dyudyu tu anapost insta anasifia show.

Atabadilika tu.Ni udhaifu fulani tu wa kupenda attention.Kuna watu hata wakijamba wanasimulia mitandaoni kwa strangers.
 
Ila kuna ushahidi wa shimo mkuu , na kama vipimo vikifanyika itajulukana palichimbwa pakazikwa mtu na kuhamishwa so jamaa anaweza kutwa na hatia[emoji1] [emoji1]
Kumbuka ni hadithi alisimuliwa na babu.
 
Jamaa alitakiwa kuhudumia kila kitu, halafu anamfungia tinted na Kuendelea na ishu zake. Maana kamvua nguo mitandaoni vya kutosha, mambo ya ndani unatangaza.

Hivi akija kufilisika ghafla si drama zilezile tu, maana hapo kilichomrudisha ni pesa na si mapenzi.
 
mwanaharakati mafi yangu,hapo ni mbesa baba mjini kugumu
 
...hizi ndoa za vyombo vya habari, zina shida sana!!!. Binafsi sioni haja ya kila jambo lako la kifamilia, uje utubwagie mitandaoni....huu ni uzwazwa na urimbukeni tu.

Watanzania tubadilike jamani, tufikie hatua ya kutambua kimapana "dhana ya neno, mtandao ?".....kwa kufanya hivyo, nadhani tutafika mbali.
 
Mambo ya ndani kuyaanika nje ni upungufu wa hekima na busara.
Mama kaona upweke umepitiliza kaona heri asarende
 
Asa joyce utaenda wapiii wanaume siku hzii wanataka vibinti vibichii,,,banana tu hapo kwa kilewo
 
Akiishiwa tena atarudi kupost kwamba "mwanaume mshenzi wewe,uliokota vijisenti ukalipa ada na kununua chakula,sasa umeishiwa umeanza kunitegemea tena,take your responsibility man"
Ingekuwa ni mm nisingemkubalia kurudi kwangu,ningewalipia wanangu ada kimya kimya,kila mtu akapambana na hali yake.
 
Niliwahi ambiwa na babu kuwa mwanamke si wa kuamini akanipa kisa flani hivi; kuna jamaa alikua akisumbuliwa na mbwa wa jirani yule mbwa alikua na tabia ya kuua vifaranga vya kuku sasa akawa anamwinda ili ikiwezekana amuue, siku moja kukiwa na kigiza akasikia kitu kinatikisa majani ya mahindi kuja kwake jamaa alipo sikia mahindi yanatikisika akachukua rungu akampiga nalo akijua ni mbwa wa jirani kumbe ni mtoto wa huyo jirani na akafa palepale.

Alipogundua kuwa alichopiga si mbwa bali ni mtoto wa jirani akakimbia kwenda kumwambia mkewe tukio, basi wakakubaliana wafiche maiti ili ikifika usiku sana wakautupe mbali ili isijulika mtoto kaenda wapi, wazazi wa yule mtoto walimtafuta mtoto wao bila mafanikio.
Ilipofika usiku wa manane wakakubaliana wakamzike mtoto mbali huko vichakani, walimzika wakarudi maisha yakaendelea. Kwa bahati nzuri jamaa akaenda akamsimulia ndugu yake kilichompata nae ndugu yake akamuuliza kama mkewe anajua nae akamkubalia huyo ndugu yake akamwambia kama Mke anajua basi afanye jitihada usiku tena akahamuamishe huyo marehemu akamzike sehemu nyingine mbali anayojua mwenyewe Kwa sababu mwanamke si wa kuamini.

Na jamaa akafanya alivyoelekezwa na ndugu yake, siku zikapita nyingi baada ya tukio siku moja kukatokea ugomvi jamaa akampiga mkewe mwanamke akakimbilia polisi kusimulia kila kitu.

Polisi wakamkamata jamaa na mwanamke akawapeleka hadi walipomzika huyo mtoto lakini hawakumpata.

Huyu kaambiwa asipost yeye mbiyo kupost.
aisee
 
Back
Top Bottom