Kwako Kilewo wangu,
Kwanza kabisa nakushukuru sana kwa uwepo wako katika Maisha yangu, UPENDO wako wa awali ulinifanya nione hakuna kama wewe hapa duniani. Ulinipenda, ulinidekeza, ulinijali, ulilinda hisia zangu, uliniaminisha hutakuja kunisaliti, uliniaminisha wewe ni Mume bora na Baba bora na Kiongozi bora. Nikakupenda sana, nikajitoa sana, nikakuheshimu na kukupa Thamani yako yote.
.
Nakushukurua sana kwa Baraka ya Watoto wazuri Lincon & Linston. Kipindi cha Miaka miwili bila Amani kwenye Ndoa yetu hakika wamekuwa Faraja yangu Kubwa sana. Japo muda mwingi nakuwa nimezubaa kwa mawazo, Watoto hujua na kuniuliza "mama mbona unanuna?" Huyo ni Lincon! Basi natabasamu kuwaridhisha wanangu japo Moyo wangu una MAUMIVU makali sana ambayo baba yao kanijeruhi.
.
Mume wangu umeisambaratisha familia yetu bila huruma, umetuacha hapa kama wakiwa. Ujasiri wa kunipiga kote kibao ni huyo MBWA, unafanya biashara nyumbani huleti hata shilingi kwa ajili ya huyo shetani, Huo ndo Uongozi Kweli Mume wangu? huo ndo UKAMANDA Mume wangu?
.
Tulikukosea nini Mume wangu? Unajimilikisha gari ya hawara bila aibu unazurura nayo kila kona , unakuja nayo mpaka nyumbani, ulitaka nikuiteje kama siyo MARIOOO. ulitaka nikuite nani Mume wangu, kama unaweza kuhongwa gari na Kahaba bila aibu unakuja nayo mpaka Kwangu ulitaka nikuiteje ebu niambie??? Sikupata jina baya zaidi hakika ningekuita tuu kwa MAUMIVU uliyonipa..
.
Nashukuru sana umenifanya nijifunze kumpenda MUNGU zaidi kuliko binadamu. Binadam tunabadilika sana. Nilikwambia kwa machozi Mengi sana kwama UNAMPENDA MUOE unipe Talaka. Ukanikatalia hutoki nae japo Dunia inajua ni mchepuko wako. inaumaaaa.. Pata Picha ingekuwa ni Mimi nakuja Nyumbani na gari ya Mwanaume unaesikia natembea nae... Ungekuwa unajiskiaje Mume wangu.
Mume wangu wewe ni Kiongozi, Chagua mwanamke unaempenda umuoe utulie. Ni aibu kujiita KIONGOZI lakini huheshimu familia yako. UONGOZI ni DHAMANA kubwa, unatakiwa uongoze watu kwa mfano mzuri.mfano wa kwanza ni kwenye familia yako Siyo kwenye Taasis, ukatibu wa chama, udiwani, ubunge, Ni nyumbani kwako. Nasikitika Watu wengi wanaokuzunguka wengi hamthamini familia zenu kabisa.. INASIKITISHA!
Source : JKiria Page