Joyce Kiria bado anatapatapa. Amvua nguo 'mume wake', Henry Kilewo

Joyce Kiria bado anatapatapa. Amvua nguo 'mume wake', Henry Kilewo

Ukimfatilia kule insta..inaonesha ana msongo wa mawazo
Msongo anajitakia mwenyewe maana wadau wanamchamba vibaya mno.
Anashindwa nini kumove on aendelee na maisha yake? Kama kweli anampenda Kileo angekaa kimya wakasolve mambo yao kimya kimya.
Na hata kama Kileo anataka kurudi kwa mke wake sidhani kama ataweza tena maana kila kitu chake kipo exposed, hakuna mwanaume anayevumilia huo ujinga.
 
Lazima achanganyikiwe na yote kasababisha yeye mwenyewe. asingeanika mambo ya mumewe mtandaoni nakwambia jamaa angekuwa amesharudi kwa mkewe. Anatumia uharakati wake vibaya. Kileo harudi leo wala kesho labda Joyce aamue kubadilika, ana tabia mbaya
Mi namuona kama kachanganyikiwa vile mwanaume anamrusha roho[emoji26]

Na huyo Moza mambo yake super sijui kama kilewo atabanduka leo or kesho!

Poor Joy
 
Mi namuona kama kachanganyikiwa vile mwanaume anamrusha roho[emoji26]

Na huyo Moza mambo yake super sijui kama kilewo atabanduka leo or kesho!

Poor Joy
Lakini kuna kipindi alimuanika sana huyo kaka mabaya yake mitandaoni,
Kama aliona anaweza ishi bila yeye atulie tu.
Lakin kama hawezi akubali kushuka na aache kututangazia ya nyumbani kwake !
Matatizo ya ndoa hayasolviwi mtandaoni na watu walikua wanamchora tu wanamkomesha kwa kiherehere chake
 
Msongo anajitakia mwenyewe maana wadau wanamchamba vibaya mno.
Anashindwa nini kumove on aendelee na maisha yake? Kama kweli anampenda Kileo angekaa kimya wakasolve mambo yao kimya kimya.
Na hata kama Kileo anataka kurudi kwa mke wake sidhani kama ataweza tena maana kila kitu chake kipo exposed, hakuna mwanaume anayevumilia huo ujinga.
Ila huruma asee....lkn nasikia alimfanyia vibaya first husband wake
 
Kwako Kilewo wangu,

Kwanza kabisa nakushukuru sana kwa uwepo wako katika Maisha yangu, UPENDO wako wa awali ulinifanya nione hakuna kama wewe hapa duniani. Ulinipenda, ulinidekeza, ulinijali, ulilinda hisia zangu, uliniaminisha hutakuja kunisaliti, uliniaminisha wewe ni Mume bora na Baba bora na Kiongozi bora. Nikakupenda sana, nikajitoa sana, nikakuheshimu na kukupa Thamani yako yote.
.
Nakushukurua sana kwa Baraka ya Watoto wazuri Lincon & Linston. Kipindi cha Miaka miwili bila Amani kwenye Ndoa yetu hakika wamekuwa Faraja yangu Kubwa sana. Japo muda mwingi nakuwa nimezubaa kwa mawazo, Watoto hujua na kuniuliza "mama mbona unanuna?" Huyo ni Lincon! Basi natabasamu kuwaridhisha wanangu japo Moyo wangu una MAUMIVU makali sana ambayo baba yao kanijeruhi.
.
Mume wangu umeisambaratisha familia yetu bila huruma, umetuacha hapa kama wakiwa. Ujasiri wa kunipiga kote kibao ni huyo MBWA, unafanya biashara nyumbani huleti hata shilingi kwa ajili ya huyo shetani, Huo ndo Uongozi Kweli Mume wangu? huo ndo UKAMANDA Mume wangu?
.
Tulikukosea nini Mume wangu? Unajimilikisha gari ya hawara bila aibu unazurura nayo kila kona , unakuja nayo mpaka nyumbani, ulitaka nikuiteje kama siyo MARIOOO. ulitaka nikuite nani Mume wangu, kama unaweza kuhongwa gari na Kahaba bila aibu unakuja nayo mpaka Kwangu ulitaka nikuiteje ebu niambie??? Sikupata jina baya zaidi hakika ningekuita tuu kwa MAUMIVU uliyonipa..
.
Nashukuru sana umenifanya nijifunze kumpenda MUNGU zaidi kuliko binadamu. Binadam tunabadilika sana. Nilikwambia kwa machozi Mengi sana kwama UNAMPENDA MUOE unipe Talaka. Ukanikatalia hutoki nae japo Dunia inajua ni mchepuko wako. inaumaaaa.. Pata Picha ingekuwa ni Mimi nakuja Nyumbani na gari ya Mwanaume unaesikia natembea nae... Ungekuwa unajiskiaje Mume wangu.

Mume wangu wewe ni Kiongozi, Chagua mwanamke unaempenda umuoe utulie. Ni aibu kujiita KIONGOZI lakini huheshimu familia yako. UONGOZI ni DHAMANA kubwa, unatakiwa uongoze watu kwa mfano mzuri.mfano wa kwanza ni kwenye familia yako Siyo kwenye Taasis, ukatibu wa chama, udiwani, ubunge, Ni nyumbani kwako. Nasikitika Watu wengi wanaokuzunguka wengi hamthamini familia zenu kabisa.. INASIKITISHA!

Source : JKiria Page
Sijapata kuona mwanamke mpuuzi kama Joyce Kiria.
 
Back
Top Bottom