Joyce Kiria bado anatapatapa. Amvua nguo 'mume wake', Henry Kilewo

Joyce Kiria bado anatapatapa. Amvua nguo 'mume wake', Henry Kilewo

Chizi tu huyu!
Kwako Kilewo wangu,

Kwanza kabisa nakushukuru sana kwa uwepo wako katika Maisha yangu, UPENDO wako wa awali ulinifanya nione hakuna kama wewe hapa duniani. Ulinipenda, ulinidekeza, ulinijali, ulilinda hisia zangu, uliniaminisha hutakuja kunisaliti, uliniaminisha wewe ni Mume bora na Baba bora na Kiongozi bora. Nikakupenda sana, nikajitoa sana, nikakuheshimu na kukupa Thamani yako yote.
.
Nakushukurua sana kwa Baraka ya Watoto wazuri Lincon & Linston. Kipindi cha Miaka miwili bila Amani kwenye Ndoa yetu hakika wamekuwa Faraja yangu Kubwa sana. Japo muda mwingi nakuwa nimezubaa kwa mawazo, Watoto hujua na kuniuliza "mama mbona unanuna?" Huyo ni Lincon! Basi natabasamu kuwaridhisha wanangu japo Moyo wangu una MAUMIVU makali sana ambayo baba yao kanijeruhi.
.
Mume wangu umeisambaratisha familia yetu bila huruma, umetuacha hapa kama wakiwa. Ujasiri wa kunipiga kote kibao ni huyo MBWA, unafanya biashara nyumbani huleti hata shilingi kwa ajili ya huyo shetani, Huo ndo Uongozi Kweli Mume wangu? huo ndo UKAMANDA Mume wangu?
.
Tulikukosea nini Mume wangu? Unajimilikisha gari ya hawara bila aibu unazurura nayo kila kona , unakuja nayo mpaka nyumbani, ulitaka nikuiteje kama siyo MARIOOO. ulitaka nikuite nani Mume wangu, kama unaweza kuhongwa gari na Kahaba bila aibu unakuja nayo mpaka Kwangu ulitaka nikuiteje ebu niambie??? Sikupata jina baya zaidi hakika ningekuita tuu kwa MAUMIVU uliyonipa..
.
Nashukuru sana umenifanya nijifunze kumpenda MUNGU zaidi kuliko binadamu. Binadam tunabadilika sana. Nilikwambia kwa machozi Mengi sana kwama UNAMPENDA MUOE unipe Talaka. Ukanikatalia hutoki nae japo Dunia inajua ni mchepuko wako. inaumaaaa.. Pata Picha ingekuwa ni Mimi nakuja Nyumbani na gari ya Mwanaume unaesikia natembea nae... Ungekuwa unajiskiaje Mume wangu.

Mume wangu wewe ni Kiongozi, Chagua mwanamke unaempenda umuoe utulie. Ni aibu kujiita KIONGOZI lakini huheshimu familia yako. UONGOZI ni DHAMANA kubwa, unatakiwa uongoze watu kwa mfano mzuri.mfano wa kwanza ni kwenye familia yako Siyo kwenye Taasis, ukatibu wa chama, udiwani, ubunge, Ni nyumbani kwako. Nasikitika Watu wengi wanaokuzunguka wengi hamthamini familia zenu kabisa.. INASIKITISHA!

Source : JKiria Page
 
Pumbavu saana, ukweli ni kua Kiria bado anasumbuliwa na wivu na mumewe, alimuacha kwa tambo bado unalia lia nini sasa, MWANAUME ni MWANAUME TU
 
Pumbavu saana, ukweli ni kua Kiria bado anasumbuliwa na wivu na mumewe, alimuacha kwa tambo bado unalia lia nini sasa, MWANAUME ni MWANAUME TU
Instagram katoa tena povu kumlilia mtu ni kumvimbisha kichwa aisee
 
Yaani mumewe kuchepuka na mmoja tu analalamika dunia nzima kwa page ndefu ya lawama. Ingekuwa ni ile enzi ya mitume waliokuwa na wake zaidi ya 10 huyu angejiua. Wanawake wabinafsi sana. Unataka uwe peke yako kwani wewe ni mama yake mzazi.
Acha kukashifu mitume..hawakufanya na wala hawakutegemea kwa matamanio yao bali ni kwa amri ya mwenyezi mungu
 
Kama ni kweli, Joyce kwa mara ya kwanza namuonea huruma. Tunaweza kumponda kwa tabia zake za kuandika upupu ila inaumiza mno kufanyiwa vitendo hivyo, wenye ndoa mnanielewa.

Joyce ashauriwe vyema, kama ndoa imeshindikana, basi apewe taraka yake aishi kwa amani. Kuumia ukiwa ndanj ni tofauti na kuumia ukiwa nje!. Pole sana dada!! Wanaume sijui tuna shida gani?

Better u tell yo colors, ka unapenda wake wengi ijulikane, sio unaapa utakuwa na mmoja halafu unaoa mwngne. Kuchepuka kupo, ila sio mpaka umuoneshee madharau wife live!
Tatizo umekuta muvi ipo kati...
 
Back
Top Bottom