JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

Pascal.. Ikulu hawakabidhiani tu mwaka fulani ukifika.

Naona kama ni mbinu za kumtuliza Lissu akubaliane na matokeo ambayo kimsingi mnadhani yeye ndiye atakuwa mshindi.

Kwa siasa zetu, hilo ni gumu kutokea. Tukubaliane tu, kuwa hata sasa ikitokea akashinda,

Wakubaliane muundo bora wa kuunda serikali.

Haiwezekani mtu itokee mtuu anashinda kwa zaidi ya 30% asipate nafasi katika serikali. Hii iwe ni cdm ama ccm ama chama chochote kile.

Binafsi ningependa zaidi serikalini muunganiko kati ya chadema,ACT na CCM.

Hii ni kwa afya ya demokrasia ya nchi yetu na maendeleo yake.
 
Mkuu BAK, kwanza nakutangulizia pole kwa kipigo cha kesho.
Hakuna any first and hard rules, nani aseme nini, hatupangiani cha kuchangia!.

Sijui wewe uko wapi, unaishi nchi gani, wala siijui exposure yako, lakini Mkuu Mzee Mwanakijiji, anafahamika ni Mtanzania anayeishi Detroit Marekani kwa muda mrefu, hivyo ana good exposure, ameshauri kuwa kwa uchaguzi wa kesho, ni Magufuli, Lissu bado, he has a chance kwa 2025, akashauri Mbowe ni lazima aondoke kijiti ampe Lissu. Pia akamshauri Lissu nini cha kufanya ili 2025 aingie ikulu.

Mbowe japo amefanya kazi nzuri kuijenga Chadema, lakini amefikia mwisho wa uwezo wake, he is a saturated solution, it can take no more than it can, Mbowe amefanya mengi, makubwa, mazuri, ila hapo alipofika na kuifikisha Chadema ndio mwisho wa uwezo wake, amefikia optimum of his ability, he can do no more than what he has already done.

P
 
Hivi kama una maono kiasi hiki ya siasa, ulipataje kura moja kwenye kura za maoni?
Nilipata kura moja kwasababu wajumbe sio watu!. Mimi ni mtu wa siasa za Nyerere, sikunyoosha mkono!.
P
 
Toa UPUMBAVU wako hapa! Angekuwa mwanao kauwawa ungekuja humu kuandika huu UJINGA wako? Au ungekuwa unaomboleza? MPUMBAVU mkubwa wewe. Tatizo hujitambui hata chembe unaruka ruka tu huku na kule. Wapuuzi kama wewe ni watu wa hovyo sana katika Taifa lolote lile duniani.
 
Kwa nini kuwa mwanaharakati ni weakness kwa Kiongozi?
 
Mpuuzi tu wewe ambaye huna msimamo na wala hujitambui. Ukweli kwako ni adui mkubwa ili kutimiza matakwa yako ya kusaka teuzi maana unaona baada ya wizi mkubwa wa uchaguzi kutakuwa na teuzi za kumwaga hivyo umeamua kuongeza speed ya kujipitisha pitisha mbele ya huyo anayejiita MWENDAWAZIMU ili akuone nawe kama unasumbuliwa na njaa.


 
Paza sauti ili JIWE akusikie kwamba uko katika hali ngumu sana kutokana na kuvurunda kwake, lakini leo hii huwezi kuandika ukweli utajibaraguza baraguza na kujipitisha ili akuone na akusikie kwamba nawe kamongo huwa uko upande wake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Japo familia ya the Citizen Mwananchi, bado hawajatangaza kulia njaa, lakini kama hii ndio hali halisi ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, then hata Citizens, litakuwa halina jinsi, lazima nalo soon litatangaza kupunguza wafanyakazi.

Mimi mwenyewe na kale kajikampuni kangu ka PPR, ambapo tulibamba sana tenda za serikali, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, serikali inatangaza moja kwa moja na TBC, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu hapakaliki hivyo tumehama, tumehamia jengo la Posta House kwenye kajichumba.

Wito kwa waandishi wenzangu, walioajiriwa kwenye media industry, kwa hali hii ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, usitegemee ajira pekee na usisubiri kupunguzwa kazi, bali sasa kwa sisi wanaume tufuge kuku na njiwa, na Kwa waandishi wa kike ni mambo ya ndoo na kidumu.

Kwa sisi wanaume, kuku ni kazi ya kujiajiri) na njiwa (kazi ya kuajiriwa), ili njiwa akiruka, ubaki na kuku.

Kwa waandishi wa kike, kwenye kazi ya kuteka maji, teka maji kwenye ndoo (kazi ya kudumu) na kidumu (kujiajiri), ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, angalau unabaki na kidumu.

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki rais Magufuli aweze kufanikiwa kukuza uchumi wa nchi yetu na kuifanya, Tanzania ya Viwanda kufanikiwa, Tanzania ya uchumi wa gesi, Tanzania ya uchumi wa kati, tukielekea kuwa nchi ya ahadi kwa mabomba nchi mzima yatatoa maziwa na asali
Jumatano Njema.
Paskali

 
Unawashwawashwa sana na Mambo ya Chadema, Umepaniki? Relax
 
Jamaa fala kweli yan, si Ajabu akaitwa Njaa aka Mayala
 
Nope. Namkubali Mwanakiji ila kwa hili sipo naye. Kama atashindwa hata tukimpigia, so ni heri nimpigie tu sasa nipate kulala usingizi mwema? After all, kuna options nyingine beside Magu.
 
Pascal Mayalla punguza kebehi
Hii thumb up ni kebehi
Umeulizwa 'Angekuwa mtoto wako amepigwa risasi ungeandika haya..??' Funny enough unaweka thumbs up seriously!
Umekosa utu kabisa
Unafurahia yaliyomkuta Lissu kupigwa risasi
eti fulani sijui exposure mavi kunuka so what?
Unbelievable
Unafurahi sasa mitandao imezimwa watu wanauwana wewe upo na familia yako raha tele unasubiri uteuzi ama??!

Tukutane ng'ambo ile....
 
Lissu anashinda uchaguzi huu kwa uhakika. CCM mtakachofanya kama ilivyo kawaida yenu nikutumia mabavu kuiba kura nakujitangaza washindi. Hili halina mjadala kwani wewe Paskal unalijua, magufuli analijua na wote wanaccm mnalijua hata kama mnakata kwa nguvu zote. Hapa hakuna uchaguzi ni maigizo tu.
Tume, wasimamizi wote wa uchaguzi katika ngazi zote, polisi, mahakama wote ni CCM, halafu utegemee haki kutendeka? Utegemee mpinzani ashinde halafu atangazwe? Itakuwa siyo Tanzania. Ila tutafika tu.
 
Usiwapangie .
 
Busara kali na kuntu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…