Mnaigopa sana Yanga. Timu zina madaktari. Issue ya kuchoma sindano hakuna team duniani Daktari wa wachezaji anakuwa hana sindano kama sehemu ya huduma ya kwanza endapo tatizo likitokea uwanjani.
Kagueni mikoba yote ya madktari nchini muone kama hakutakuwa na syringe kwenye mabegi yao. Kukutwa kwa syringe kwenye dustibin za vyumba vya kubadilishia nguo hakuna dhambi.
Matibabu ya mchezaji aliyeumia uwanjani huwa wanachomwa sindano kuzuia kuvilia kwa damu ili kurahisisha matibabu au kupona haraka kwa jeraha husika. Mfano kama aligonga goti na kuwa na mvilio eneo hilo sindano inaweza kuchomwa directly eneo hilo. Hakuna kosa kwenye hili wala kwenye ulimwengu wa michezo. Dawa zingine huchomwa ili kutuliza maumivu mchezaji aweze kucheza mpira.
Kwa sisi wakongwe kidogo tutakumbuka Wayne Rooney alienda Germany 2006 kwenye kombe la dunia akiwa hajapona vizuri majeraha. Alicheza akiwa anachomwa sindano za maumivu.
Mara kadhaa tumesikia wachezaji duniani wakisema wao wenyewe au management kuwa amecheza akiwa na maumivu ya sehemu fulani. Nini kilimsaidia mchezaji kuendelea kucheza? Ni dawa za maumivu.
Kwenye mechi ya Yanga na Azam mnajua wachezaji walioumia kipindi cha kwanza. Pia mechi dhidi ya Tabora mnajua wachezaji waliomuia . Mlitegemea wawaache wakia kwenye maumivu makali wakina Bocca, Kibabage, Andambwile bila huduma ya kwanza?
Kauli ya Ally Kamwe kuhusu wachezaji wanaoachwa na Simba kurudi kuwa vijana wakijiunga na Yanga si ajabu. Mnamkumbuka Juma Kaseja, Amis Tambwe, Kelvin Yondani waliocheza kwa muda mrefu na kwa mafanikio Yanga baada ya kuachwa na Simba.