Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Tatizo la umaskini wa maarifa, uelewa na negativity, ndiyo chanzo cha umaskini wa Watanzania wengi.

Kuifungua Tanzania na kuufanya uchumi wake uchangamane na Dunia, ndiyo njia sahihi ya kuleta kwa kasi maendeleo ya kiuchumi.

Rais Samia asimame kwenye mstari sahihi, wala asipoteze muda kusikiliza upuuzi wa wajinga wachache wasio na uelewa wowote kwenye masuala ya bishara, uwekezaji na uchumi.

Hongera sana Samia, upo kwenye njia sahihi. Tembelea nchi kama Dubai (UAE), ukapate uzoefu wao wa kina namna walivyoibadilisha nchi yao ndani ya miaka 15. Tembelea nchi kama Botswana, Singapore, Malaysia, Hong Kong upate uzoefu wao, namna biashara huru zilivyoyajenga mataifa yao. Usijifungie kama marehemu aliyekuwa akiua maendeleo ya uchumi, huku akiamini anajenga uchumi wetu kwa kasi.
 
Hii sana wachina wanatengeneza bidhaa mbovu kabisa, mfano tiles za Goodwill na Twyford ni takataka kabisa.

Halafu miradi ya serekali wanalazimisha kununua Bidhaa ya Tanzania.

Lazima tubadilike
 
Yaaani tunakoelekea hii nchi Mungu aingilie kati kenya wajanja sana kuzid Tz tujiandae kuumia kwa hili
Amekamata soko la Rwanda na Burundi tu, hilo la Kenya hawezi kuthubutu hata kidogo. Na hata hilo la Burundi na la Rwanda atanyang'anywa, rais wa Burundi sasa hivi yuko Kenya na yeye keshaweka dole!. Kenyatta safi!
Pessimism ni mbaya, kwahiyo unamuombea kufeli ama.
Yaani mtanzania mwenzako anapambana we unataka afeli
 
Ndugu unatofautiana na wadau wengine sehemu ndogo sana......hakuna anayepingana na haya mabadiliko mazuri nchini kwetu kwani ni neema.....wasi wasi wa wadau ni mazingira yetu ya kibiashara hayajaandaliwa kukabiliana na ushindani.......production cost kwa mujibu wa wadau ni kubwa sana hapa kwetu uki compare na nchi shindani.....hii haitaathiri ukuaji wa sekta yetu ya viwanda hapa nchini.....??
 
Ila
Kasome hayo makubaliano. Kenya wanataka hiyo sementi ya Dangote kwani grade yake ndiyo inafaa kwa ujenzi wa madaraja na maghorofa marefu. Sisi tunaweza kuletewa ile ya daraja hafifu inayozalishwa na viwanda vingi vya Kenya.
Ila wabongo sijui mna matatizl ya akili au vipi, aisee.
 
Umechelewa, tumeshaweka kidole (saini) tayari!
Hivi hapo Ikulu hakuna majasusi wa uchumi?

Si muoni yule vuvuzela wa chadema bwana Yericko Nyerere kwenye hili
 
Tusiwe wavivu kufikiri ipo mifumo ya checks and balances.Masuala ya Kodi ni mapana Sana zipo protocol za EAC pia.
Kinaondoshwa ni urasimu na maamuzi ya kibabe ya kishamba na kijinga kwa dunia ya leo.
Wewe ni mtoto ndogo sana kwenye haya mambo huwezi kuekewa kinachojadiliwa hapa
 
Kasome hayo makubaliano. Kenya wanataka hiyo sementi ya Dangote kwani grade yake ndiyo inafaa kwa ujenzi wa madaraja na maghorofa marefu. Sisi tunaweza kuletewa ile ya daraja hafifu inayozalishwa na viwanda vingi vya Kenya.
Kwamba wamespecify kabisa kwenye mkataba wanataka dangote cement?

Kenya kwa sasa wana projects kubwa za ujenzi, mfano nairobi express way , na hawatumii Dangote cement, wanatumia cement zao ambazo zina ubora mzuri kuliko zetu.
Linapokuja swala la standards kenya wapo juu sana kuliko sisi ,
 
Huyo huwa hana akili, kifupi huwa ni mduni wa hoja na kudharau akili za wengine kujifanya anajua sana.
 
Hivi hapo Ikulu hakuna majasusi wa uchumi?

Si muoni yule vuvuzela wa chadema bwana Yericko Nyerere kwenye hili
Umemsikia waziri wa maswala ya nje ya nchi akiwasiliasha bajeti[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Mungu kwakweli mwaka 2021,katupiga tz 11:0
 
Waheshimiwa huu ni mjadala muhimu kwa taifa letu hivyo lingetakiwa kujadiliwa kwa weledi na sio mihemko, jazba, chuki na ushabiki........

Wataalamu na wasomi waliobobea kwenye masuala ya uchumi na biashara waje jukwaani tuweze kupata maoni na mitazamo ili jamii ya waTanzania itoke gizani....

WATANZANIA wanahitaji kujua matokeo hasi na chanya kwenye makubaliano haya.......


KARIBUNI WATAALAMU, WADAU NA WASOMI......
 
Hii sana wachina wanatengeneza bidhaa mbovu kabisa, mfano tiles za Goodwill na Twyford ni takataka kabisa.

Halafu miradi ya serekali wanalazimisha kununua Bidhaa ya Tanzania.

Lazima tubadilike
Tiles za goodwill na twyford Tanzanzia mara kadhaa nimeshuhudia zikishindwa kuingia kenya kwa sababu ya ubora hafifu, ,
Twyford wana kiwanda kenya lakini products zao ni level za juu kuliko twyford Tanzania

Bila usbishi wakenya wapi vizuri kwenye quality control
 
Huyo huwa hana akili, kifupi huwa ni mduni wa hoja na kudharau akili za wengine kujifanya anajua sana.
Ana hoja nzuri sana isipokuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa JAZBA dhidi ya watu wanaotofautiana na mitazamo inayoendana na matakwa ya nafsi yake......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…