Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Tatizo la umaskini wa maarifa, uelewa na negativity, ndiyo chanzo cha umaskini wa Watanzania wengi.Endelea kujidanganya. Mimi naishi Mashariki ya mbali huku na Juice za Azam zinauzwa hadi huku, sembuse Kenya? Kipindi Kikwete anatoka Azam walishaanza kuuza Juice zao Kenya ila mahusiano ya kinchi yaliharibika kipindi cha JPM ndio maana mauzo yalipungua. Haya makubaliano ni neema kwetu. Tatizo watu tumezidi woga. Wakenya ni watu wa kawaida tu.
Kuifungua Tanzania na kuufanya uchumi wake uchangamane na Dunia, ndiyo njia sahihi ya kuleta kwa kasi maendeleo ya kiuchumi.
Rais Samia asimame kwenye mstari sahihi, wala asipoteze muda kusikiliza upuuzi wa wajinga wachache wasio na uelewa wowote kwenye masuala ya bishara, uwekezaji na uchumi.
Hongera sana Samia, upo kwenye njia sahihi. Tembelea nchi kama Dubai (UAE), ukapate uzoefu wao wa kina namna walivyoibadilisha nchi yao ndani ya miaka 15. Tembelea nchi kama Botswana, Singapore, Malaysia, Hong Kong upate uzoefu wao, namna biashara huru zilivyoyajenga mataifa yao. Usijifungie kama marehemu aliyekuwa akiua maendeleo ya uchumi, huku akiamini anajenga uchumi wetu kwa kasi.