Jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule ni la nani?

Wakuu,

Nani ana jukumu la kuweka mazingira ya shule safi? Ni walimu, wanafunzi au watu maalum wa kufanya usafi?

Shule hasa za serikali wanafunzi ndio huwa wanakuwa na jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule kwa kufagia uwanja, ofisi za walimu, kusafisha vyoo na hata wakipewa adhabu zinakuwa za kusafisha ama kulima kwenye maeneo ya shule na wakati mwingine huambiwa kufanya usafi hata kwenye nyumba za walimu.

Jambo hilo limekuwa likileta msuguano kati ya wazazi na walimu, na tukio la hivi karibuni mzazi kaenda kumpiga mwalimu sababu ya kumchapa mwanafunzi aliyekataa kudeki darasa.

Sasa je, nani ana jukumu la kufanya usafi kwenye mazingira ya shule?
Huyo mzazi aliyeenda kumpiga Mwalimu shuleni alibaki salama?
 
Duh!! Mzazi kampiga Mwalimu kisa mwanae amepewa kazi ya kusafisaha mazingira halafu kesho toto kama hili likiwa halina nidhamu halimuheshimu wala kumsikiliza mtu yoyote kutokana na malezi mabovu alioyapata kutoka kwa wazazi wake mnashangaa
Mimi miaka ya themanini wakati nasoma sio usafi tu tulikuwa tunalima mpaka mashamba ya shule
Kiukweli Mimi ni mwalimu wa sekondari Tena sayansi,najimudu kitaaluma na kihojo.mzazi kama hiyo kwangu angekula kipigo na kumfungulia kesi ya uvamizi kwenye majengo ya serikali na kukwamisha shughuli za ufundishaji.
Nilishawahi kufanya hivyo kipindi Cha nyuma.Nilimpa adhabu form 6,akagoma,akaenda kumleta mzazi naye akaja wa moto eti akanishika shati.Nilimpa kibano then nikamwita mlinzi akamweka chini ya ulinzi.Nilienda kituo Cha polisi kuripoti kuwa nimevamia na mzazi shuleni.Yeye na mtoto wake walibebwa na difenda kupelekwa kituoni.
Sasa Mimi nashangaa eti mwalimu anapigwa na mzazi Tena shuleni,Mimi utaniua labda iwe mtaani
 
Ukute ulinywea na kuchapwa stick na mzazi, mfyuuuh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kiukweli Mimi ni mwalimu wa sekondari Tena sayansi,najimudu kitaaluma na kihojo.mzazi kama hiyo kwangu angekula kipigo na kumfungulia kesi ya uvamizi kwenye majengo ya serikali na kukwamisha shughuli za ufundishaji.
Nilishawahi kufanya hivyo kipindi Cha nyuma.Nilimpa adhabu form 6,akagoma,akaenda kumleta mzazi naye akaja wa moto eti akanishika shati.Nilimpa kibano then nikamwita mlinzi akamweka chini ya ulinzi.Nilienda kituo Cha polisi kuripoti kuwa nimevamia na mzazi shuleni.Yeye na mtoto wake walibebwa na difenda kupelekwa kituoni.
Sasa Mimi nashangaa eti mwalimu anapigwa na mzazi Tena shuleni,Mimi utaniua labda iwe mtaani
Sio uungwana unampigaje mwalimu kwangu mm mwalimu ana hadhi sawa na mchungaji siwez hata mjibu vibaya .kama kuna jambo tutajadili kama mshirika wangu kwenye malezi
 
Wafanyakazia maalum walioweka kwa ajili ya usafi tu maana wanafunzi wapo kwa elimu bora sio kwa ajili ya usafi , mtoto akisumbuliwa sana kusoma nikazi angalia tu waliofanikiwa maisha ni wale waliojuwa maprefect mamonitor maana wao wakiamka tu wao huwa wanajiandaa kwenda kusoma tu sio usafi hawawazi cha maji wanatoa wapi kwanini wasifaulu
 
Japan wanafunzi sio tu husafisha shule bali husafisha mitaa inayowazunguka pia
Ile nchi natamani sana siku Moja nikajifunze mfumo wao wa malezi ya shule maana hutoa watu wenye nidham sana
 
Back
Top Bottom