Jukwaa gani ni pendwa kwako ndani ya JamiiForums?

Jukwaa gani ni pendwa kwako ndani ya JamiiForums?

Nalipenda sana jukwaa la siasa na ndio muda wote nashinda huko .

Lakini jukwaa la Habari na hoja mchanganyiko nimetokea kulipa heshima yake na kulipenda maana ndiko niliko mkuta na kunikutanisha na Binti ephen Mwanajeshi wa akiba aliyeuteka moyo wangu wote na kuunasa kama Sumaku.

ephen ephen popote ulipo wewe ndiye umenifanya nilipe heshima yake na kulipenda jukwaa la habari na hoja mchanganyiko.
 
Kipindi najiunga nilikagua kila jukwaa kwa kipindi fulani, japo huwa napitia majukwaa mengi sababu natumia mda mwingi jf hivyo kuchanganya majukwaa ili nisichoke kusoma
 
Hakuna jukwaa lenye tija, yote tu tunavamia. Mods tengenezeni algorithms watu wawe wanapelekwa majukwaa wanayofuatilia kwa sana unakuta limtu halipendi mada flani nalo linachangia tu kisa ni uzi unaotrendi. Mods fanyeni kama social media zingine kuwe na preferences kwa wachangiaji.
 
jukwaa lilofanya nijiunge JF ni jamii inteligence, kipindi hicho lilikua la moto kweli kweli.

nishawahi kukaa mwaka mzima bila kuingia jukwaa la MMU, nikiwa sina ishu ya mapenzi siendagi kabisa.

jukwaa langu pendwa kwa sasa ni Entertainment.

habari na hoja mchanganyiko ndo jukwaa langu bora la muda wote.

siasani huwa naangalia vichwa vya habari tu, kikinivutia nasoma kama hamna issue napita hivi.

michezoni huwa nadokoa dokoa tu. sijastick kiviile.

kwa kuhitimisha niseme tu, kila jukwaa lina umuhimu wake, it depends una interest gani kwa wakati huo.

mlale unono 😊😊😊😊😊
 
Back
Top Bottom