Jukwaa la habari msitafute mchawi, Chanzo kikubwa cha vyombo vya habari kufa ni kukosekana "Habari za kiuchunguzi"

Jukwaa la habari msitafute mchawi, Chanzo kikubwa cha vyombo vya habari kufa ni kukosekana "Habari za kiuchunguzi"

Nasubiri media fulani zife kabisa yale majengo yao nikafugie huko kuku wa nyama coz nowadays ni blaablaa
 
Media zinakufa sababu ya technology

Mtasingizia kila kitu
Uchawi ni internet tu

ni kweli lakin kwa case yetu sisi hapa kuna zaidi ya hilo, ndio maana magazeti km mwanaspoti hayajaathirika sana km haya magazeti ya habari za kawaida, kwa upande wa television wengi walikua wanapenda kuangalia habari ITV lkn leo hawapendelei tena ukiwauliza sababu na uhakika haitakuwa internet
 
Jukwaa la habari na wachambuzi mbalimbali wanadai kukosekana kwa wateja kwenye vyombo vya habari kumeletwa na teknolojia ya mitandao!

Wanadai kwamba Siku hizi watu wengi wanapata taarifa mitandaoni hivyo ndiyo maana hawanunui magazeti au kuangalia TV.

Madai kama haya hayaakisi ukweli halisi wa tatizo!

Chanzo kikuu cha kufa kwa vyombo vya habari ni ukosefu wa habari za kiuchunguzi (investigation)

Kwasababu watu wanahitaji habari halisi ili wavutiwe kutizama au kusoma magazeti!

Vyombo vya habari karibu vyote siku hizi vimekosa Investigation Journalism.

Ni kama kusifu na kupamba rangi ya nyumba pasipo kujadili nyufa nyumba!
Vyombo vingi vya habari vitapotea kama hawatajipambanua kutoa habari TECHNICAL!

Vyombo vya habari vinahoji watu walewale kama chanzo cha taarifa pasipo kujikita katika uchunguzi wa tatizo lenyewe!
Hata Mimi na kataa maoni yao,wamejichimbia makaburi yao wao wenyewe kwa mkondo wa utoaji habari waliouchagua.Wajiandae na maziko ya vyombo vingine vingi vya habari kama hawatafanya tathimini ya kweli na kujirekebisha.
 
Unaongea na still hujui unachoongea
Washington post iliuzwa Kwa kushindwa
Kupata faida ina survive now Kwa kuwa alienunua ndo mtu tajiri kuliko wote duniani
Haimpi shida kumiliki gazeti linalopata hasara

Hayo magazeti yote uliyotaja yote Yana struggle..
Mengine yana online contents na matangazo ya online
Mengine yanamilikiwa na big media houses zenye online branch na TV na kadhalika
Hakuna newspaper inayopata faida these days...
Kwa utaratibu wetu yakwetu yote tutayazika siku sii nyingi.
 
Anayebisha hii fact atangulie hapa Dodoma mirembe. Nilikua nanunue sana gazeti la mwananchi kabla ya uchanguzi wa 2015. Baada ya uchaguzi wa 2020 nimeacha hata taarifa za habari za vyombo vya Tanzania.
 
Media zinakufa sababu ya technology

Mtasingizia kila kitu
Uchawi ni internet tu
Sio kweli we denzel washington.marekani na uk mitandao ilianzia kule but magazeti yanauzwa sana.google circulation ya the washingtone post kwa siku ni nakala ngapi
 
Back
Top Bottom