Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

Mfano sehemu gani unaona panapwaya bado watu hawajapajadili vizuri? Angle gani watu wanatumia hisia zaidi? Wapi watu wametumia maarifa vizuri na viongozi wakaamua kuchukua mawazo wakatekeleza? Mifumo inahitaji mawazo ya watu?
Hivi ni kwamba post yangu hujaelewa ?maana yangu nimesema hivii jukwaa limepoteza mvuto kwa watu kuleta porojo nyingi na matusi bila logic

Nimesema kwa upande wangu mwisho ni kasema kama unakubaliana na mimi una shauri nini kifanyike

Swali hili unalouliza ni kama hujaelewa mada iliyopo mezani
 
kila mada lazima iwe na opposing and proposing side hicho unachoweza kuita ni "pumba" ni kwasababu mtu akaenda nje na matakwa yako kwahiyo cha msingi wew focus na unayo yaona ni sawa na yasio sawa achana nayo

mfano hapo mwisho umeuliza kama mdau anakubaliana na wew kwamba jukwaa limepoteza mvuto, mind you kuna watu hawaoni kama mvuto umepotea ndo maana nyuzi za siasa hazijaacha kupostiwa humu
 
Shida ni kwamba ubongo wa watu umelala, huku jukwaani sasa hivi kuna watu ukiwaletea mada inayohitaji data, takwimu, au uchambuzi wa kina wa sera, wanapita kama hawaoni. Leta mada ya udaku wa kisiasa au nani kamtolea mwenzake maneno machafu kwenye mkutano wa hadhara, uone traffic itakayokuja hapo. Ni kama vile uwezo wa watu kufikiri kwa kina umepungua, kila mtu anataka mambo mepesi mepesi tu yanayofurahisha nafsi. To be honest, ukitaka kujua nchi ina safari ndefu, angalia tu mijadala ya vijana huku jukwaani. Tunafia kwenye mambo ya kijinga huku mambo ya msingi yanayohusu kodi zetu na mustakabali wa taifa yakipita hivi hivi.

Machawa na njaa zao ndio wanazidi kuharibu jukwaa, huwezi kukaa ukategemea intellectual debate kutoka kwa mtu anayetetea ugali wake hapa mjini. Shida yao kubwa ni kwamba wakiona hoja imenyooka na inabana, badala ya kujibu kwa hoja, wanaanza kukushambulia wewe binafsi au kukutukana, wanalipwa kwa idadi ya post wanazosifia, sio kwa uzito wa akili wanazotumia, huwa wanakuja na copy and paste za taarifa za habari bila hata kufanya tahakiki. Hii tabia inachosha sana na inafanya watu wenye akili zao waamue kukaa kimya na kuwa wasomaji tu, matokeo yake jukwaa linaachwa mikononi mwa wapiga kelele.

Hizi ID Fake zimetupa ujasiri wa kijinga, huu mfumo una faida zake kiusalama, lakini upande wa pili umefanya watu wawe mazuzu kwa kujiamini. Mtu anajua kabisa hakuna anayemfahamu, kwa hiyo anaona ana leseni ya kuandika pumba yoyote inayokuja kichwani kwake bila hofu ya kuonekana mjinga kwenye jamii inayomzunguka. Wale watu wenye upeo mkubwa na heshima zao uraiani wanaogopa hata kuchangia kwa sababu hawataki kushushwa heshima na watoto wadogo wanaojificha nyuma ya majina ya bandia. Matokeo yake, jukwaa linajaa watu wasio na nidhamu ya hoja, kila mtu anajiona yeye ndio anajua kila kitu huku ukiangalia uandishi wake tu unajua kabisa huyu kichwani ni empty.

Solution ni mod kupiga watu ban ya maana, kama tunataka hili jukwaa lirudi kwenye enzi zake, lazima kuwe na mabadiliko makubwa upande wa usimamizi. Hizi mada za marudio na za kichochezi zisizo na mashiko zifutwe mara moja. Mtu akileta mada laini laini au anayeleta matusi badala ya hoja, anapigwa ban ya maisha ili iwe fundisho kwa wengine. Lazima jukwaa liwekewe viwango fulani vya ubora wa mada, sio kila anayeamka na stress zake za nyumbani anakuja kutapika huku jukwaani. Bila kufanya hivyo, hili litabaki kuwa jukwaa la mipasho kama kijiwe cha kahawa badala ya kuwa chemchemi ya fikra mbadala kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.
 
kila mada lazima iwe na opposing and proposing side hicho unachoweza kuita ni "pumba" ni kwasababu mtu akaenda nje na matakwa yako kwahiyo cha msingi wew focus na unayo yaona ni sawa na yasio sawa achana nayo
Soma tena nilichoandika
Kuna sehemu umeona nimeegemea upande?
Huku unapwaya !
mfano hapo mwisho umeuliza kama mdau anakubaliana na wew kwamba jukwaa limepoteza mvuto, mind you kuna watu hawaoni kama mvuto umepotea ndo maana nyuzi za siasa hazijaacha kupostiwa humu
Nyuzi za siasa zinapostiwa yes je za aina gani?
 
Katiba itapatikanaje watu wasipokaa chini na kuanza kuchora mchoro wa hiyo katiba mpya

Katiba iliyopo sasa ilipatikana vipi?
kuna makundi yamegawanyika hapo mkuu kuna wanaoamini Katiba inaweza kupatikana hata bila maelewano hilo ni kundi dogo na kuna wanaoamini Katiba mpya haina maana yoyote hii inatosha nalo ni kundi dogo ukilinganisha na lile linalosema Katiba Mpya ipatikane kwa kuanza na maelewano hili ni kundi kubwa. Sisi tunaondoka na ile kauli "Wengi wape" na kila kikundi kinahoja zake..Wananchi tunataka KATIBA MPYA.
 
Tumeua akili na kujenga hoja tangu masekondarini tulipoacha mijadala/dabates na kuleta kusolve past papers na kule vyuoni kudesa! Kwa sasa tunataka sentensi fupifupi tu na nyepesi kama tweets!

Tukitaka kuleta tena mijadala yenye akili tunatakiwa kurudi square 1 kuanza kujenga upya, hii sio miujiza kwamba jamii itakuja tu automatically bila kuundwa! Tunavuna tulichopanda kuanzia miaka ya 90 na itachukua muda mwingine mrefu kwa sababu uchawa nao ulikuja tangu jekee achukue inchi so tuna miaka mingine kama 30 hivi ya kuishi uchawa na maombi ya kina mitume na manabii uchwara wazee wa miujiza, ahsante
 
😅 kasheshe!
Huu msemo haufai kutumika kila sehemu
Kusema kweli kuna hoja za maana na zinastahili utulivu ili kujibiwa kwa ufasaha.

Ila kuna hoja ambazo, anavyokuja ndivyo tunavyompokea, tunajaribu kuweka mizani sawa ili huyo anayeleta shallow topics ajipange wakati mwingine aje na mada fikirishi.

Kuna mdau kasema ni ngumu sana kujadiliana na mtu anayelipwa kutetea ugali wake. Tutawapokea namna wanavyokuja....
 
Back
Top Bottom