Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

CCM sio chama cha siasa tena na ilishaondoka kwenye ushindani wa hoja imebaki kutumia hofu na vitisho vya dola, haijalishi raia watoe hoja nzuri kiasi gani haitasaidia chochote.
 
Kaka ukitaka hayo ongea na lucas mwashambwa na chawa wake wanaotumiwa na ccm waache kupost pumba humu
 
Happy Sunday guys ❤️

Humu jukwaani kuna ile standard Ukiingia jukwaa fulani, unajua utakutana na nini
Ukiingia jukwaa kama hili la siasa unajua kabisa utakutana na quality fulani

Hata kama huyu mtu akiwa kwenye majukwaa mengine anaonekana tofauti, kuna ule msemo kwamba watu hawawezi kuwa serious muda wote✔️
So inategemewa mtu akifika kwenye hili jukwaa, itumike akili zaidi kuliko hisia

Mimi ni kijana mdogo, lakini nashangazwa na baadhi ya wakubwa zangu huku

Pengine kwa fikra au kwa maarifa, wanaacha kujikita kwenye hoja na kuanza kutukana au kuandika nachoweza kuita pumba, na jukwaa linakosa mvuto kama inavyotegemewa

Haya ni maoni tu, naomba yasionekane kama uchochezi

Na ukweli sio kwamba humu haziletwi mada nzuri na hoja zinaletwa
Ila unakuta watu wa kujenga hoja hamna, au sijui hawataki, au la sielewi🤔


Msiulize, Ooh, wewe mada za maana unazoleta ziko wapi?”
Zipo Nimeleta mara nyingi tu Ila watu hawapendi kujadili mada ngumu, wanapita juu juu
Ni wachache utakuta wanajadili huku zile post za ajabu ajabu zikipata airtime

Sasa mambo ya msingi yasipojadiliwa na kuanza kuangalia post laini laini, hii nchi wataijenga kina nani kwa mtindo huo?

Kuna wale wanaoitwa machawa
Hawa wapo wa upande tawala
Hawa wanalalamika kutukanwa
Japo siungi mkono matusi, lakini ebu njooni na mada za maana, za hoja nzito
Njooni kuwa prove wrong wapinzani wenu Kuwaambia, Nyie mnasema hivi, lakini ipo hivi

Acheni taarabu huku jukwaani
Jukwaa linapoteza mvuto

Na upande wa upinzani nao, hebu leteni hoja za maana watu wajadili
Acheni kuleta mada laini laini za marudio, jamani
Jengeni hoja jukwaani

Hii platform ni nzuri
Tupo kwa ID fake, japo usalama sio 💯 percent, ila hapa huwezi kulinganisha na IG, WhatsApp au FB

Wewe mdau wa jukwaa hili unakubaliana na mimi jukwaa limepoteza mvuto?

Je nini kifanyike ?

ShesRise_1 ✋️
Siasa ndani ya taifa letu ni kweli hazina mvuto kwani ndizo zinatumika kulibomoa taifa letu badala ya kulisaidia,siasa imekuwa ndiyo utekaji,kesi mchongo,ufisadi na hata mauaji,je siasa ya namna hiyo inatoa wapi mvuto.
 
kuna makundi yamegawanyika hapo mkuu kuna wanaoamini Katiba inaweza kupatikana hata bila maelewano hilo ni kundi dogo na kuna wanaoamini Katiba mpya haina maana yoyote hii inatosha nalo ni kundi dogo ukilinganisha na lile linalosema Katiba Mpya ipatikane kwa kuanza na maelewano hili ni kundi kubwa. Sisi tunaondoka na ile kauli "Wengi wape" na kila kikundi kinahoja zake..Wananchi tunataka KATIBA MPYA.
Wengi wape !
Hawa wengi sasa wafanye juhudi wapewe
 
Siasa ndani ya taifa letu ni kweli hazina mvuto kwani ndizo zinatumika kulibomoa taifa letu badala ya kulisaidia,siasa imekuwa ndiyo utekaji,kesi mchongo,ufisadi na hata mauaji,je siasa ya namna hiyo inatoa wapi mvuto.
Noma sana saisa siasa imekosa mvuto
 
Kuna machawa wanajuhudi sana wanavamia vibaya hadi kieleweke kwa hiyo inachosha kusoma maandishi yao hadi unajikuta unatukana
Kuwatukana pia ni kuwapa airtime kama hujui
 
Kweli Sasa kama mada zenyewe za kina tlaatlaah na mwashambwa kitu kama watu kutekwa wanashabikia,Kwa nini watu wenye mioyo ya jazba wasiwatukane!ingawa sipendi MATUSI.
Matusi hayasaidiii hata
 
Na zaidi kama hatua hazitachukuliwa kimsingi kizazi hiki kitaenda na kuacha uchawa na miujiza feki ya kutesha mimba jukwaani ikitamalaki! Kijacho kitakuja kuuona huu upumbavu na kuusafisha
Ngoja tuone mwisho wake
 
Mkuu,
Hatuwezi kufanana, ukitaka hivyo labda uwaambie mods wafanye sensorship ya mada, na hapo utaondoa dhana ya where we dare to talk openly. Kwa hiyo hata hizo tunazooona mada za hovyo, zinaruhusiwa as ni free forum, wanaoona zinawafaa watajadili, wanaoona zinazingua watatukana au kukaa kimya.

Wengine tutatukana in a very polite language ili kuondoa sumu kwenye ubongo, hatutakaa kimya.
Okay 👍
 
Kwa maoni yangu,
nadhani siasa imevamiwa na jamii ambayo haifahamu vema au haina ufahamu ya kwamba siasa ni sayansi, na sio porojo, mihemko, matusi, uongo, uzushi au mahali pa kutafutia excitements.

na hata hoja ikiletwa jukwaani katika sura nilizozitaja hapo juu, mbobevu katika sayansi ya siasa kamwe hawezi kubabaika wala ku-rate kwamba hoja hii ni ya maana au sio ya maana, bali atatoa mawazo yake mapya na fikra mbdala bora zaidi ya hicho cha maana au kisicho cha maana jukwaani. Kinachoonekana, wengi huenda zaidi ya kitu kinachoitwa siasa.

I think,
mihemko na matusi kwenye mijadala ya kisiasa jukwaani, hua ni ishara ya wazi kabisa kwamba mwenye hali hiyo hana ufahamu wala uelewa wa kutosha juu ya kwamba siasa ni sayansi. Ingawa ni haki yake, lakini pia hayo ndio maoni yake huru, hayapaswi kusababisha jukwaa kukosa mvuto.

Binafsi,
katika siasa naona kila kinachopostiwa JF kwenye jukwaa hili la siasa kina maana. Na ikiwa hakina maana, basi huyo aliona hakina maana inafaa atoe maelezo mujarabu yaliyo bora zaidi ya hicho ambacho anaona hakina maana.

Politics is a mind game. It's all about perceptions. And you can't run away about that truth, because that's the nature of politics. And there are only two constants in politics ie are interests and betrayal. Out of that, I don't know if it can be called politics.

hiyo ya kupoteza mvuto ama laa, sidhani kama inaweza kua ni siasa, unless ni kitu kingine ambacho binafsi sikijui.

Binafsi naona hoja za wadau ni nzuri kulingana na uelewa wao, na ninadhani ni vizuri kuendelea kuenzi hoja na maandko mbalimbali ya kisiasa humu jukwaani kwa kutoa mawazo mapya na fikra mbadala bora zaidi ya hoja zenyewe zinazopostiwa jukwaani. Matusi na vinginevyo, ni maoni huru ya wahusika, but
ni muhimu zaidi vichukuliwe kama fursa ya kujirekebisha, kujisahihisha, kua wastahilivu na wenye subra ili hatimae jukwaa liwe bora zaidi mbeleni.🐒
Asante kwa maoni 🤝
 
Utazungumza mengi lakini chanzo ni ccm wameua utoaji wa hoja.
Zaidi ukiwapinga kwa hoja utapigwa risasi, utatekwa rejea ya polepole na lissu.
Kwa msingi huo haya ndiyo matokeo yake.
Nini kifanyike kwa mtazamo wangu nature itaamua
Nature itaamua haya sana
Asante kwa maoni yako
 
CCM sio chama cha siasa tena na ilishaondoka kwenye ushindani wa hoja imebaki kutumia hofu na vitisho vya dola, haijalishi raia watoe hoja nzuri kiasi gani haitasaidia chochote.
Inasikitisha
 
Back
Top Bottom