Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

Acheni taarabu huku jukwaani
Jukwaa linapoteza mvuto

Na upande wa upinzani nao, hebu leteni hoja za maana watu wajadili
Acheni kuleta mada laini laini za marudio, jamani
Jengeni hoja jukwaani

ShesRise_1 Nami nimepitia hali hiyo hiyo. Nilipoanzisha mjadala wa Muundo wa Muungano wiki iliyopita, licha ya kwamba niliibua hoja kuhusu Dola yenye Muundo wa Serikali moja (1) Lakini Jumla ya mihimili yake iwe minne (4), lakini nilikutana na wachangiaji waliojenga hoja za kina, waliokubali kutofautiana kwa heshima, na waliobadilisha mtazamo wangu kwa baadhi ya mambo. Lakini pia nilikutana na maingiliano yasiyo na uzito, na hata jaribio la kutumia sheria kama kisingizio cha kutaka uzi ushushwe badala ya kujadili maudhui yenyewe. Tofauti kati ya aina hizo mbili za wachangiaji ndiyo hasa unayoigusa.

Nadhani tatizo si Jukwaa la Siasa lenyewe, ni kwamba limebeba mzigo mzito kupita uwezo wake. Siasa, Katiba, sheria, na masuala ya maendeleo ya jamii ni mambo tofauti yenye tabia tofauti za mjadala, lakini yote yanalazimika kubanana jukwaa moja. Siasa ya kila siku huvuta hisia na majibu ya haraka, Kejeri za kisiasa na Upinzani, huku Mjadala wa kikatiba na kisheria unahitaji subira, marejeo, na uvumilivu wa kujenga hoja hatua kwa hatua. Ukiviweka pamoja, mjadala wa kina hupotea kwenye mkondo wa haraka wa majibu ya kisiasa.

Ninaunga mkono kikamilifu wazo la kuwepo Jukwaa maalum, kwa mfano "Katiba, Sheria na Maendeleo ya Jamii," litakalokuwa na masharti yake wazi: hoja zenye marejeo, mijadala ya kisheria, misaada ya kisheria kwa wanajamvi, na mada za maendeleo ya jamii, bila kuruhusu matusi wala mijadala ya vyama vya siasa ya papo kwa papo. Jukwaa la aina hiyo lingevutia aina ya wachangiaji tunaowahitaji, wale wanaokuja kujenga, siyo kuvunja, Matusi au Upinzani.

Naamini uongozi wa JamiiForums wangeweza kulipokea vizuri wazo hili likiwasilishwa rasmi kama pendekezo, kwa mantiki linaboresha ubora wa jukwaa zima, siyo kuligawa. Kama wewe au wengine mtaandaa pendekezo rasmi kwa uongozi, tayari nina mfano wa aina ya mijadala inayoweza kustawi humo, kama ile tuliyoifanya wiki iliyopita.

Kwa sasa, jibu la muda mfupi ni kila mmoja wetu kuendelea kuleta hoja nzito na kukataa kuvutwa kwenye mijadala midogo, hata kama itachukua muda mrefu kujenga utamaduni huo. Asante kwa kuinua hoja hii kwa uwazi na bila uchokozi.

Nitapenda kuona post hii inamfikia CEO Maxence Melo na kama atapendezwa kuunda jukwaa maalumu kwa ajiri ya wale wenye hoja nzito juu ya hoja nzito kama mimi, itakuwa ni heshima kubwa.

Marejeo ya Uzi wa: Muundo Bora wa muundano ni upi.? na pendekezo langu la Dola yenye Mihimili minne.
1. Baraza la usimamizi wa Taifa.
2. Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa Tanzania

(Hoja za kina zimewekwa ndani ya uzi huo)
 
Attachments

  • images - 2025-03-30T152501.267.jpeg
    images - 2025-03-30T152501.267.jpeg
    10 KB · Views: 6
@ShesRise_1 Nami nimepitia hali hiyo hiyo. Nilipoanzisha mjadala wa Muundo wa Muungano wiki iliyopita, licha ya kwamba niliibua hoja kuhusu Dola yenye Muundo wa Serikali moja (1) Lakini Jumla ya mihimili yake iwe minne (4), lakini nilikutana na wachangiaji waliojenga hoja za kina, waliokubali kutofautiana kwa heshima, na waliobadilisha mtazamo wangu kwa baadhi ya mambo. Lakini pia nilikutana na maingiliano yasiyo na uzito, na hata jaribio la kutumia sheria kama kisingizio cha kutaka uzi ushushwe badala ya kujadili maudhui yenyewe. Tofauti kati ya aina hizo mbili za wachangiaji ndiyo hasa unayoigusa.
Pole kwa hiyo changamoto mkuu
Na hongera kwa michango michache na mizuri uliyopokea
Nadhani tatizo si Jukwaa la Siasa lenyewe, ni kwamba limebeba mzigo mzito kupita uwezo wake. Siasa, Katiba, sheria, na masuala ya maendeleo ya jamii ni mambo tofauti yenye tabia tofauti za mjadala, lakini yote yanalazimika kubanana jukwaa moja. Siasa ya kila siku huvuta hisia na majibu ya haraka, Kejeri za kisiasa na Upinzani, huku Mjadala wa kikatiba na kisheria unahitaji subira, marejeo, na uvumilivu wa kujenga hoja hatua kwa hatua. Ukiviweka pamoja, mjadala wa kina hupotea kwenye mkondo wa haraka wa majibu ya kisiasa.

Ninaunga mkono kikamilifu wazo la kuwepo Jukwaa maalum, kwa mfano "Katiba, Sheria na Maendeleo ya Jamii," litakalokuwa na masharti yake wazi: hoja zenye marejeo, mijadala ya kisheria, misaada ya kisheria kwa wanajamvi, na mada za maendeleo ya jamii, bila kuruhusu matusi wala mijadala ya vyama vya siasa ya papo kwa papo. Jukwaa la aina hiyo lingevutia aina ya wachangiaji tunaowahitaji, wale wanaokuja kujenga, siyo kuvunja, Matusi au Upinzani.

Naamini uongozi wa JamiiForums wangeweza kulipokea vizuri wazo hili likiwasilishwa rasmi kama pendekezo, kwa mantiki linaboresha ubora wa jukwaa zima, siyo kuligawa. Kama wewe au wengine mtaandaa pendekezo rasmi kwa uongozi, tayari nina mfano wa aina ya mijadala inayoweza kustawi humo, kama ile tuliyoifanya wiki iliyopita.
Naunga mkono hoja kaka mkubwa 👏
Kwa sasa, jibu la muda mfupi ni kila mmoja wetu kuendelea kuleta hoja nzito na kukataa kuvutwa kwenye mijadala midogo, hata kama itachukua muda mrefu kujenga utamaduni huo. Asante kwa kuinua hoja hii kwa uwazi na bila uchokozi.
Sahihi sana🤝
Nitapenda kuona post hii inamfikia CEO @Maxence Melo na kama atapendezwa kuunda jukwaa maalumu kwa ajiri ya wale wenye hoja nzito juu ya hoja nzito kama mimi, itakuwa ni heshima kubwa.
Maxence Melo 🙏🙏
Marejeo ya Uzi wa: Muundo Bora wa muundano ni upi.? na pendekezo langu la Dola yenye Mihimili minne.
1. Baraza la usimamizi wa Taifa.
2. Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa Tanzania

(Hoja za kina zimewekwa ndani ya uzi huo)
Asante kwa link mkuu🙏🙏

Shukran sana asante kwa mchango wako mzuri kwenye uzi huu ni imani yangu tutakutana kwenye mijadala mingine zaidi 🫡🫡
 
Hizi lawama hata huwa sizielewi. Binadamu wanatofautiana katika namna ya kufikiri, kupokea na kutoa maoni/hoja pia.

Hili jukwaa limekuwa na hayo mnayoyalalamikia tangu enzi na enzi. Katika hayo mnayoyalalamikia pia kuna hoja kuntu za watoa hoja na hii imekuwa hivyo katika kipindi chote ninachoifahamu jf. Namna bora ya kumfundisha mtu ni pale unapoona ametoa pumba, nawe ukawa una hoja kuntu basi itoe hiyo hoja yako.

Lakini pia nyakati zimebadilika, hizi sio nyakati za kujifanya una akili sana au unajua sana. Yamewakuta watu mazito hivyo wamejifunza kuucheza muziki kulingana na mdundo wake.
 
Ndiyo tumetofautiana kufikiri ndiyo maana kuna waliolewa uzi wangu nini hasa nimelenga na hoja yangu imelenga kitu gani
Lakini pia nyakati zimebadilika, hizi sio nyakati za kujifanya una akili sana au unajua sana. Yamewakuta watu mazito hivyo wamejifunza kuucheza muziki kulingana na mdundo wake.
Comment yako ilikua ni hii

Asante kwa maoni
 
Ndiyo tumetofautiana kufikiri ndiyo maana kuna waliolewa uzi wangu nini hasa nimelenga na hoja yangu imelenga kitu gani

Comment yako ilikua ni hii

Asante kwa maoni
Ni kwanini kila anayejibu tofauti na jibu unalotaka unaona hajaelewa uzi wako?
 
Ni kwanini kila anayejibu tofauti na jibu unalotaka unaona hajaelewa uzi wako?
Umefanya huo utafiti sasa hivi?
Kuna tatizo gani nikisema hujaelewa uzi wangu ?
Ila wewe huoni tatizo kutoelewa uzi wangu?
 
Happy Sunday guys ❤️

Humu jukwaani kuna ile standard Ukiingia jukwaa fulani, unajua utakutana na nini
Ukiingia jukwaa kama hili la siasa unajua kabisa utakutana na quality fulani

Hata kama huyu mtu akiwa kwenye majukwaa mengine anaonekana tofauti, kuna ule msemo kwamba watu hawawezi kuwa serious muda wote✔️
So inategemewa mtu akifika kwenye hili jukwaa, itumike akili zaidi kuliko hisia

Mimi ni kijana mdogo, lakini nashangazwa na baadhi ya wakubwa zangu huku

Pengine kwa fikra au kwa maarifa, wanaacha kujikita kwenye hoja na kuanza kutukana au kuandika nachoweza kuita pumba, na jukwaa linakosa mvuto kama inavyotegemewa

Haya ni maoni tu, naomba yasionekane kama uchochezi

Na ukweli sio kwamba humu haziletwi mada nzuri na hoja zinaletwa
Ila unakuta watu wa kujenga hoja hamna, au sijui hawataki, au la sielewi🤔

Msiulize, Ooh, wewe mada za maana unazoleta ziko wapi?”
Zipo Nimeleta mara nyingi tu Ila watu hawapendi kujadili mada ngumu, wanapita juu juu
Ni wachache utakuta wanajadili huku zile post za ajabu ajabu zikipata airtime

Sasa mambo ya msingi yasipojadiliwa na kuanza kuangalia post laini laini, hii nchi wataijenga kina nani kwa mtindo huo?

Kuna wale wanaoitwa machawa
Hawa wapo wa upande tawala
Hawa wanalalamika kutukanwa
Japo siungi mkono matusi, lakini ebu njooni na mada za maana, za hoja nzito
Njooni kuwa prove wrong wapinzani wenu Kuwaambia, Nyie mnasema hivi, lakini ipo hivi

Acheni taarabu huku jukwaani
Jukwaa linapoteza mvuto

Na upande wa upinzani nao, hebu leteni hoja za maana watu wajadili
Acheni kuleta mada laini laini za marudio, jamani
Jengeni hoja jukwaani

Hii platform ni nzuri
Tupo kwa ID fake, japo usalama sio 💯 percent, ila hapa huwezi kulinganisha na IG, WhatsApp au FB

Wewe mdau wa jukwaa hili unakubaliana na mimi jukwaa limepoteza mvuto?

Je nini kifanyike ?

ShesRise_1 ✋️
Sichangii chochote mpaka labda niambiwe mimi pia ni Tatizo
 
Back
Top Bottom