Shida ni kwamba ubongo wa watu umelala, huku jukwaani sasa hivi kuna watu ukiwaletea mada inayohitaji data, takwimu, au uchambuzi wa kina wa sera, wanapita kama hawaoni. Leta mada ya udaku wa kisiasa au nani kamtolea mwenzake maneno machafu kwenye mkutano wa hadhara, uone traffic itakayokuja hapo. Ni kama vile uwezo wa watu kufikiri kwa kina umepungua, kila mtu anataka mambo mepesi mepesi tu yanayofurahisha nafsi. To be honest, ukitaka kujua nchi ina safari ndefu, angalia tu mijadala ya vijana huku jukwaani. Tunafia kwenye mambo ya kijinga huku mambo ya msingi yanayohusu kodi zetu na mustakabali wa taifa yakipita hivi hivi.
Machawa na njaa zao ndio wanazidi kuharibu jukwaa, huwezi kukaa ukategemea intellectual debate kutoka kwa mtu anayetetea ugali wake hapa mjini. Shida yao kubwa ni kwamba wakiona hoja imenyooka na inabana, badala ya kujibu kwa hoja, wanaanza kukushambulia wewe binafsi au kukutukana, wanalipwa kwa idadi ya post wanazosifia, sio kwa uzito wa akili wanazotumia, huwa wanakuja na copy and paste za taarifa za habari bila hata kufanya tahakiki. Hii tabia inachosha sana na inafanya watu wenye akili zao waamue kukaa kimya na kuwa wasomaji tu, matokeo yake jukwaa linaachwa mikononi mwa wapiga kelele.
Hizi ID Fake zimetupa ujasiri wa kijinga, huu mfumo una faida zake kiusalama, lakini upande wa pili umefanya watu wawe mazuzu kwa kujiamini. Mtu anajua kabisa hakuna anayemfahamu, kwa hiyo anaona ana leseni ya kuandika pumba yoyote inayokuja kichwani kwake bila hofu ya kuonekana mjinga kwenye jamii inayomzunguka. Wale watu wenye upeo mkubwa na heshima zao uraiani wanaogopa hata kuchangia kwa sababu hawataki kushushwa heshima na watoto wadogo wanaojificha nyuma ya majina ya bandia. Matokeo yake, jukwaa linajaa watu wasio na nidhamu ya hoja, kila mtu anajiona yeye ndio anajua kila kitu huku ukiangalia uandishi wake tu unajua kabisa huyu kichwani ni empty.
Solution ni mod kupiga watu ban ya maana, kama tunataka hili jukwaa lirudi kwenye enzi zake, lazima kuwe na mabadiliko makubwa upande wa usimamizi. Hizi mada za marudio na za kichochezi zisizo na mashiko zifutwe mara moja. Mtu akileta mada laini laini au anayeleta matusi badala ya hoja, anapigwa ban ya maisha ili iwe fundisho kwa wengine. Lazima jukwaa liwekewe viwango fulani vya ubora wa mada, sio kila anayeamka na stress zake za nyumbani anakuja kutapika huku jukwaani. Bila kufanya hivyo, hili litabaki kuwa jukwaa la mipasho kama kijiwe cha kahawa badala ya kuwa chemchemi ya fikra mbadala kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.