DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Jukwaa la Uzalendo na Mabadiliko limetoa barua ya wazi kwa Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Joel Arthur Nanauka, likielezea wasiwasi mkubwa juu ya utekelezaji wa mpango wa Shilingi Bilioni 200 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya vijana nchini.
Katika barua hiyo iliyotolewa hivi karibuni, jukwaa hilo kupitia, Ibrahim Shukran Aloyce-Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Uzalendo na Mabadiliko, limebainisha kuwa ingawa hatua ya serikali ni ya kupongezwa, utekelezaji wake unakabiliwa na urasimu, ukosefu wa uwazi, na masharti yanayowaengua walengwa halisi.
Jukwaa hilo limekosoa mfumo wa sasa wa kupeleka fedha hizo katika wizara mbalimbali za kisekta badala ya kuwa na mfumo mmoja, jambo ambalo limeongeza urasimu. Pia, limeibua sintofahamu kuhusu utoaji wa hivi karibuni zaidi wa Bilioni 7 kwa wahitimu wa mradi wa BBT-Uvuvi, likihoji ikiwa fedha hizo ni sehemu ya Bilioni 200 na kwanini zimetoka kabla ya mchakato rasmi kukamilika.
Moja ya hoja nzito zilizoibuliwa ni sharti la kuwasilisha hati ya umiliki wa ardhi kama kigezo cha kupata mkopo. Jukwaa limesema sharti hili linawanyima fursa vijana wengi ambao hawamiliki ardhi binafsi. Aidha, limehoji uamuzi wa kupandisha umri wa mnufaika hadi miaka 40 katika sekta ya kilimo, likisema jambo hilo linakinzana na Sera ya Taifa ya Vijana (2007, toleo la 2024) inayotambua kijana kuwa wa miaka 18-35.
“Kutenganisha ajenda za ajira, kazi na maendeleo ya vijana kunapunguza uwezo wa wizara kushughulikia tatizo kuu la vijana, yaani ukosefu wa ajira na kazi, jambo linalopunguza tija ya sera na mipango ya uwezeshaji”, imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Ili kuleta tija, Jukwaa la Uzalendo na Mabadiliko limetoa mapendekezo matano ambayo ni kuundwa kwa Bodi Huru ya Mikopo itakayosimamia ugawaji wa fedha bila ushawishi wa kisiasa, kuanzishwa Dirisha Moja la Mikopo kwa Mfuko wa Fedha wa Vijana ili kuondoa urasimu wa wizara nyingi, kuzingatia Sera ya Umri kwa kurejea kwenye kigezo cha miaka 18-35 ili kutoa fursa halisi kwa vijana, kulegeza masharti kama hati za ardhi ili kuongeza ushiriki na kutofautisha na fedha za halmashauri kwa kuweka mipaka iliyo wazi ili kurejesha imani ya vijana iliyopotea kutokana na changamoto za mikopo ya asilimia 10.
Barua hiyo pia imegusia muundo wa wizara, ikisema kukosekana kwa Naibu Waziri na timu pana ya kisera kunaathiri ufanisi. Pia imelalamikia kutoundwa kwa Baraza la Vijana la Taifa ambalo limekuwa likisubiriwa kwa muda mrefu kama jukwaa la kuunganisha vijana.
Jukwaa limehitimisha kwa kutoa rai kuwa mafanikio ya Bilioni 200 yatategemea uwazi na ujasiri wa wizara kuondoa vikwazo vinavyowarudisha nyuma vijana wa Kitanzania.