Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #21
Hatuzungumzii utakatifu tunazungumzia Wajibu, majukumu na HAKIYani hii jinsia ina shida sana halafu mkiambiwa ukweli mnakimbilia kuwatukana wanaowaambia ukweli badala ya kujibu hoja, hivi kwanini huwa mnapenda kujiona watakatifu sana na kuwatupia lawama wanawake kwenye kila kitu, sasa ugomvi wa baba na mama unahusiana nini na watoto
Baba anapomkosea mama mbona huwa mnataka watoto wasiingilie kati wala wasiwaone ninyi wabaya, kwa kusema kuwa ugomvi wa wazazi wao hauwahusu ila mama anapomkodea baba basi huo ugomvi unawahusisha mpaka watoto, kwa kusitishiwa huduma ambazo ni haki yao ya msingi na wajibu wako wewe kama baba
Hakuna anayekataa Baba kutoa huduma. Ila atoe huduma Akiwa nyumbani kwa Baba.
Kama Baba atapendekeza vinginevyo ndivyo mtoto akae kwa Mama.
Mama huwezi king'ang'ania watoto alafu wajibu wa kuwahudumia umpe Baba. Huo ni USHENZI, ukatili, dhulma, ubinafsi.
Kama huwezi kuhudumia huna haja ya king'ang'ania kukaa na watoto.
Wanawake wanaweza kuwa wabinafsi ila hata siku moja hawawezi kuwa wabinafsi kwa watu wanaowapenda hasa watoto wao wa kuwazaa, hizo hela mnazowatumia mnaona kama wanazifaidi sana siyo, kama wangekuwa wanatumia hizo hela za matunzo vibaya hao watoto wangeishije sasa
Yule dogo aliyekufa Dodoma Kisa Mamaake kumuacha usiku vijiweni kwenye bodaboda huko yeye akaenda kwenye starehe zake naye yupo kundi la Wanawake unaowazungumzia?
Kwenye cases kama hizi kiuhalisia ninyi wanaume ndio wabinafsi kwa sababu hamyafikirii majukumu aliyonayo mwanamke kwa watoto, ukiachilia mbali kubeba mimba, kuzaa, kunyonyesha (maana hayo mnasingizia ni majukumu ya kimaumbile), bado kuna jukumu la kuwalea hao watoto toka wakiwa wachanga hadi watakapoweza kujitegemea, mfano kuwalisha, kuwasafisha, kuwauguza wakiumwa je mnawasaidia hayo.
Mkishaachana majukumu yanabadilika.
Hayo majukumu ya Baba na Mama yapo kwenye Ndoa na watu wanaoishi pamoja.
Lakini baada ya kuachana wajibu na majukumu hubadilika.
Mwenye jukumu la kukaa na mtoto ni Yule anayeweza kumhudumia full stop. Hizo nyingine ni huruma zisizo na kichwa Wala miguu.
Hayo majukumu siyo ya kimaumbile hata ninyi mnaweza kuyafanya lakini hamko tayari kuyafanya, hata mkiachiwa hao watoto mtaishia kuwapa wanawake wengine wawalelee, ilihali wakiwa kwa mama zao mnategemea mama zao ndio wawalee na hapo hapo wawatafutie pesa wakati huo ninyi wanaume mkiwa mmebweteka tu
Hebu acheni kutafuta visingizio vya kukwepa majukumu yenu ugomvi wenu hauwahusu watoto, hata hao wanawake wawakosee vipi tafuteni namna ya kuhudumia watoto wenu acheni kuplay victims na kutafuta sympathy, hakuna namna mtakwepa kuonekana hamna hatia kwa kuwatelekeza watoto wenu hata msemeje timizeni wajibu wenu
Hayo mambo ya baraka za kina baba sijui malezi mabaya ya kina mama ni propaganda kama propaganda nyingine tu kuna watoto wengi wamefanikiwa huku wakiwa na uhasama na baba zao, na kuna watoto wengi wamelelewa na single mothers na wamekuwa na maadili mema usitake kulazimisha mawazo yako ndio yawe uhalisia, tena usivyo na aibu unaandika kwa kujiamini kabisa kana kwamba uliambiwa wote unaowaandikia humu ni watoto wa primary wasiojua maisha ya mahusiano na ndio wanaanza kujifunza kupitia maandiko yako
Kuhusu suala la Baraka Hilo achana nalo kwa Sababu lipo juu ya Akili za kawaida ambazo huenda wewe ndio unazo.
Kama unaona suala la Baraka ni suala la propaganda Basi bado unamambo Mengi ya msingi ya kujifunza