Juliana shonza; Waambie wanawake wenzako kama hawawezi kuhudumia watoto wao wawapeleke kwa Baba Zao full stop na sio hizo ngonjera ulizotoa

Hatuzungumzii utakatifu tunazungumzia Wajibu, majukumu na HAKI
Wewe umeongea kana kwamba wanawake ndio waovu sana na wanaume ndio watakatifu sana
Hakuna anayekataa Baba kutoa huduma. Ila atoe huduma Akiwa nyumbani kwa Baba.
Kama Baba atapendekeza vinginevyo ndivyo mtoto akae kwa Mama.

Mama huwezi king'ang'ania watoto alafu wajibu wa kuwahudumia umpe Baba. Huo ni USHENZI, ukatili, dhulma, ubinafsi.
Kama huwezi kuhudumia huna haja ya king'ang'ania kukaa na watoto.
Sasa baba usipohudumia watoto wako unataka ufanye jukumu gani lingine kwao, unajua wanawake wana majukumu mangapi juu ya watoto wao ambayo wanaume hawayafanyi, hapo kati ya baba na mama nani anakuwa mbinafsi sasa
Yule dogo aliyekufa Dodoma Kisa Mamaake kumuacha usiku vijiweni kwenye bodaboda huko yeye akaenda kwenye starehe zake naye yupo kundi la Wanawake unaowazungumzia?
Ni cases ngapi tunazisikia za kina baba kubaka watoto wao wadogo hadi wanakufa kwahiyo hao wanawake wachache wasiojali watoto wao ndio wanafanya ujumuishe wanawake wote kuwa hawafai kuachiwa watoto, kwanza hata humo kwenye ndoa asilimia kubwa watoto wanalelewa na mama baba anaweza akakaa miezi anapishana tu na wanaye anawahi kuondoka anachelewa kurudi watoto wakiwa wamelala, na hata akikaa nao ni mara moja moja kwahiyo msidhani baba kuwepo ndio guarantee ya watoto kuwa na maadili si kila baba ni family man kwani watoto wangapi wameharibikia kwenye familia zenye wazazi wote
Mkishaachana majukumu yanabadilika.
Hayo majukumu ya Baba na Mama yapo kwenye Ndoa na watu wanaoishi pamoja.

Lakini baada ya kuachana wajibu na majukumu hubadilika.
Mwenye jukumu la kukaa na mtoto ni Yule anayeweza kumhudumia full stop. Hizo nyingine ni huruma zisizo na kichwa Wala miguu.
Mkishaachana majukumu yanabadilika kivipi, kwamba mkishaachana ndio mtoto mdogo anakuwa na uwezo wa kujitegemea na kujihudumia mwenyewe, mfano kujilisha, kujivisha, kujifulia na kujiuguza nk au mnategemea hayo majukumu anafanya nani
Kuhusu suala la Baraka Hilo achana nalo kwa Sababu lipo juu ya Akili za kawaida ambazo huenda wewe ndio unazo.

Kama unaona suala la Baraka ni suala la propaganda Basi bado unamambo Mengi ya msingi ya kujifunza
Hilo suala la baraka liko wazi sana wala halihitaji rocket science kulielewa miaka yote jamii zetu zimekuwa zikiamini na zikiona kwamba, baraka au laana za mama ndio zina uhalisia zaidi kwa mtoto kuliko za baba halafu wewe unaongea kinyume chake tena kana kwamba za mama hazina impact yoyote, case studies tunaziona watoto wengi waliotelekezwa na baba zao na kuwa kwenye ugomvi nao wakifanikiwa vizuri tu tena siyo kiuchumi pekee bali kwenye maisha kiujumla
 
Mkuu, Robert Heriel Mtibeli amesema kuwa uking'ang'ania kukaa na watoto, JITEGEMEE, usianze kuombaomba hela kwa madai kuwa ulishindwa kutafuta sababu ulikua unamsafisha mtoto.

Mwanaume akiachiwa watoto atatafuta wanawake wengine wa kuwalea lakini hataomba hela kwa mwanamke, basi na wanawake wafanye hivyo, watafute wanaume wengine wataotafuta hela ili wao waendelee kuwasafisha watoto au watafute wanaume wataowasafisha watoto wakati wao wanawake wameenda kutafuta hela.

Msingi wa bandiko ni kuwa, using'ang'anie watoto wakati hauna uwezo wa kuwatunza. Acha mwenye uwezo wa kifedha akae nao
Hoja ni kwamba mwanaume hana jukumu lingine kwa mtoto zaidi ya kumhudumia kiuchumi tu ilihali mwanamke ana majukumu mengi kwa mtoto, hivyo kutaka kumuongezea na hilo la uchumi ni kumtwisha mzigo ilihali baba ukibweteka tu na ukumbuke mtoto akiwa mdogo anahitaji zaidi malezi ya mama, na hata huyo mtoto akikuwa akafikisha umri wa kuweza kuishi na baba vipi kama yeye mwenyewe akichagua kuendelea kuishi na mama yake bila shinikizo la mtu yeyote napo utaacha kumhudumia kisa hajakuchagua
 
Wewe umeongea kana kwamba wanawake ndio waovu sana na wanaume ndio watakatifu sana

Sasa baba usipohudumia watoto wako unataka ufanye jukumu gani lingine kwao, unajua wanawake wana majukumu mangapi juu ya watoto wao ambayo wanaume hawayafanyi, hapo kati ya baba na mama nani anakuwa mbinafsi sasa

Usijitoe fahamu.

Linapokuja swala huduma na matunzo kunakuwa na masharti bila kujali uhusiano uliopo wa wahusika

Hiyohiyo serikali inapotoa HUDUMA ambapo ni wajibu wake ikitokea wananchi wanaenda kinyume na serikali inayowapa huduma. Serikali inaweza kusitisha HUDUMA

Ni cases ngapi tunazisikia za kina baba kubaka watoto wao wadogo hadi wanakufa kwahiyo hao wanawake wachache wasiojali watoto wao ndio wanafanya ujumuishe wanawake wote kuwa hawafai kuachiwa watoto, kwanza hata humo kwenye ndoa asilimia kubwa watoto wanalelewa na mama baba anaweza akakaa miezi anapishana tu na wanaye anawahi kuondoka anachelewa kurudi watoto wakiwa wamelala, na hata akikaa nao ni mara moja moja kwahiyo msidhani baba kuwepo ndio guarantee ya watoto kuwa na maadili si kila baba ni family man kwani watoto wangapi wameharibikia kwenye familia zenye wazazi wote

Hakuna sehemu nimesema kila mwanaume ni Family Man

Mkishaachana majukumu yanabadilika kivipi, kwamba mkishaachana ndio mtoto mdogo anakuwa na uwezo wa kujitegemea na kujihudumia mwenyewe, mfano kujilisha, kujivisha, kujifulia na kujiuguza nk au mnategemea hayo majukumu anafanya nani

Hayo majukumu apewe anayekaa naye ambaye anaweza kuyafanya.
Hakuna anayekataa mzazi kumhudumia Mtoto wake.
Lakini hatupo tayari Sisi wanaume kuhudumia matoto yenye Kiburi,jeuri,na yasiyosikia.
Wala hatupo tayari kutunza watoto wanaoishi na wanawake wasio na maadili. Hili hatupo tayari.

Hilo suala la baraka liko wazi sana wala halihitaji rocket science kulielewa miaka yote jamii zetu zimekuwa zikiamini na zikiona kwamba, baraka au laana za mama ndio zina uhalisia zaidi kwa mtoto kuliko za baba halafu wewe unaongea kinyume chake tena kana kwamba za mama hazina impact yoyote, case studies tunaziona watoto wengi waliotelekezwa na baba zao na kuwa kwenye ugomvi nao wakifanikiwa vizuri tu tena siyo kiuchumi pekee bali kwenye maisha kiujumla
Kuhusu suala la Baraka huna uelewa nalo.
Hivyo ni Bora uachane nalo tuu.

Wewe mwambie Mamaako akubariki alafu ndugu yako mwambie abarikiwe na Babaako alafu angalia Matokeo Kati yako na ndugu yako ni Nani kizazi chake kitakuwa na Baraka
 
Hoja ni kwamba mwanaume hana jukumu lingine kwa mtoto zaidi ya kumhudumia kiuchumi tu ilihali mwanamke ana majukumu mengi kwa mtoto, hivyo kutaka kumuongezea na hilo la uchumi ni kumtwisha mzigo ilihali baba ukibweteka tu na ukumbuke mtoto akiwa mdogo anahitaji zaidi malezi ya mama, na hata huyo mtoto akikuwa akafikisha umri wa kuweza kuishi na baba vipi kama yeye mwenyewe akichagua kuendelea kuishi na mama yake bila shinikizo la mtu yeyote napo utaacha kumhudumia kisa hajakuchagua

Kuacha kuzaa watoto taja majukumu mengine ya mwanamke Kwa mtoto ambayo Baba hayawezi
 
Ukweli mtupu, kuna watu huku wanajiita single mama eti wanalea watoto wenyewe hawataki msaada wa baba kisa tu walitofautiana na wazazi wenza kwa viburi na jeuri zao, wanasema wanajimudu wanalea wenyewe ila ukifatilia wanapata tabu sana katika malezi kuna hao mpaka wakadange ndo watoto wale baba wa mtoto akitaka mtoto hataki ila huku sasa anaenyeka mbaya mtoto anatukanwa muda wote hasira zake zinaishia kwa mtoto kumpa baba mtoto hataki na ukicheki baba wa mtoto ana uwezo mzuri tu wa kulea mtoto, wanawake ifike mahali tujitambue kama baba mtoto ana nafasi na anamhitaji mwanae mpe kufanya hivo haitabadilisha mtoto atabaki tu kuwa wenu siku zote baba kuishi na mtoto haina mana kwamba ndo mtoto hatokutambua utabaki kuwa mama hakuna kitu kitabadili hilo kuliko umtese mtoto bora ukampa baba ake amlee kama hauna uwezo kuliko kujikuta unayamudu kumbe unateseka vibaya, wengine wanajitolea na mifano eti si unamuona diamond we ngoja tu muda utaongea😂😂😂
 
Usijitoe fahamu.

Linapokuja swala huduma na matunzo kunakuwa na masharti bila kujali uhusiano uliopo wa wahusika

Hiyohiyo serikali inapotoa HUDUMA ambapo ni wajibu wake ikitokea wananchi wanaenda kinyume na serikali inayowapa huduma. Serikali inaweza kusitisha HUDUMA

Hakuna sehemu nimesema kila mwanaume ni Family Man

Hayo majukumu apewe anayekaa naye ambaye anaweza kuyafanya.
Hakuna anayekataa mzazi kumhudumia Mtoto wake.
Lakini hatupo tayari Sisi wanaume kuhudumia matoto yenye Kiburi,jeuri,na yasiyosikia.
Wala hatupo tayari kutunza watoto wanaoishi na wanawake wasio na maadili. Hili hatupo tayari.

Kuhusu suala la Baraka huna uelewa nalo.
Hivyo ni Bora uachane nalo tuu.

Wewe mwambie Mamaako akubariki alafu ndugu yako mwambie abarikiwe na Babaako alafu angalia Matokeo Kati yako na ndugu yako ni Nani kizazi chake kitakuwa na Baraka
Wewe ndiye unayejitoa ufahamu wanaume mnakwepa majukumu kwa visingizio vya kijinga sana yani ni kipi kinachofanya mtoto awe na haki ya kuhudumiwa wazazi wakiwa pamoja tu ila wakiachana haki hiyo aikose, ninyi ndio mnafanya watoto wa nje ya ndoa wajione hawana thamani kwenye hii dunia kisa ugomvi wenu wa kijinga huwa mnaona kama wanawake wanafaidi sana hela zenu, ilihali hizo mnazowatumia tu hazitoshi kuhudumia hao watoto nao inabidi waongeze za kwao halafu ninyi mnadhani kwamba wamama hawachangii kabisa kwenye malezi

Kwanza kwa hela gani mnazowapa hao wanawake hadi muone kwamba zinatosha kuhudumia watoto wenu na bado hao wanawake wafanyie matumizi yao, hakuna anayewalazimisha kiasi cha kutoa ninyi toeni kiasi ambacho mnaona hiki kinatosha matumizi ya mtoto wa umri fulani mama atajijua mwenyewe, kama ni ada muambie mama atafute shule ambayo utaweza kumudu akitaka shule yenye gharama zaidi wewe lipa ada unayomudu hiyo ada nyingine ataongezea mama yake mwenyewe

Jukumu la kuhudumia mtoto kiasili ni la baba haijalishi mko kwenye ndoa au la ndio maana hata kisheria baba akifariki kama aliacha watoto wa nje nao hutakiwa kupewa mgawanyo wa mali, sawa na watoto wa ndani ya ndoa bila kujali mama zao wana wanaume wengine au la na wala hawasemi kwamba eti kwa vile walishaachana basi watoto wa nje hawastahili kupata huo mgao, kisa eti mama zao walikuwa na viburi sijui ujeuri kwa hao wababa what a lame excuse from someone calling himself a father

Hebu hudumieni watoto wenu acheni visingizio kuna wanaume ndio chanzo cha wao na mama wa watoto zao kuachana kwa sababu zao binafsi lakini nao wanajificha kwenye kichaka hicho hicho cha kusingizia kuwa wanawake wana ujeuri na kiburi, sasa serikali ikisema iwasikilize wanaume kwenye hili basi kila mwanaume atasema hahudumii sababu mama watoto wake ni mjeuri na kiburi maana ndio sababu kubwa wanayoitoa wanaume wote waliotelekeza watoto wao hata kama ni uongo, mwisho wa siku mnawadhulumu watoto haki zao za msingi hudumieni watoto wenu hakuna aliyewaambia muwahudumie mama zao huo ugomvi wenu hautakiwi kuwahusu watoto

Kuhusu baraka nimekuambia usidhani mimi ndio naanza kujifunza hapa kwenye bandiko lako na wala sihitaji kufanya ulichoniambia ili kuthibitisha hilo, sisi wengine huwa tunajifunza kupitia maisha ya watu wengine hatusubiri mpaka yatukute sisi eti ndio tuamini, ukiachilia mbali hawa tunaowaona ambao wewe hauwafahamu angalia mifano hata ya watu maarufu ambao unawafahamu niambie ni wangapi wenye ugomvi na baba zao halafu angalia hali zao za maisha zikoje
Mtoto mdogo Hana uchaguzi
Hata Hilo hulioni

Au ndio mambo ya umama hayo?
Wewe nina mashaka na uwezo wako wa kupambanua hoja kwani kisheria mtoto anatakiwa kuanza kuishi rasmi na baba yake akiwa na umri gani, jibu ni miaka saba sasa mtoto wa miaka saba hawezi kuchagua kwamba anataka kuishi na baba au mama, narudia mtoto akiwa mdogo kwa asilimia kubwa anahitaji huduma ya mama yake na siyo tu mwanamke yeyote hata kama wewe unamuona mama yake ana tabia za hovyo ila ndio mama yake huwezi kubadili hilo
Kuacha kuzaa watoto taja majukumu mengine ya mwanamke Kwa mtoto ambayo Baba hayawezi
Na hii exactly ndio point yangu kwamba ukiacha kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha majukumu mengine yote kwa mtoto mzazi yeyote anaweza kuyafanya na ndio maana nikauliza kama mnayaweza kwanini sasa hamyafanyi, maana hata mkiletewa hao watoto bado mtawapa wanawake wengine wawalee huku ninyi mkitafuta pesa ila mwanamke akisema abaki nao mnataka afanye vyote yani awalee na awatafutie pesa sasa hapo nani mbinafsi
 
Wewe ndiye unayejitoa ufahamu wanaume mnakwepa majukumu kwa visingizio vya kijinga sana yani ni kipi kinachofanya mtoto awe na haki ya kuhudumiwa wazazi wakiwa pamoja tu ila wakiachana haki hiyo aikose, ninyi ndio mnafanya watoto wa nje ya ndoa wajione hawana thamani kwenye hii dunia kisa ugomvi wenu wa kijinga huwa mnaona kama wanawake wanafaidi sana hela zenu, ilihali hizo mnazowatumia tu hazitoshi kuhudumia hao watoto nao inabidi waongeze za kwao halafu ninyi mnadhani kwamba wamama hawachangii kabisa kwenye malezi

Hii ndio shida ya kuwa na uelewa MDOGO.

Watoto wa nje ya ndoa hawawezi kuwa na thamani na wa ndani ya ndoa. Hiyo iko hivyohivyo. Dunia iende au irudi. Kwa sababu Hilo Jambo lipo naturally. Wa Nje atabaki Nje na WA ndani atabaki ndani. Mengine ni kulazimisha tuu vitu.

Kama Wamama wanachangia kwenye malezi mbona wanataka wanaume wahusika kutoa huduma.
Mbona mtoto akikaa kwa Baba yake huwezi sikia Mwanaume akisema Mama yake hatoi huduma. Yaani hata ukipotea Moja Kwa Moja mwanaume hawezi kuwa na habari na wewe na Wala hatahitaji chochote kutoka kwako?

Hoja ya Mada yangu ni kuwa, wewe kama Mama huwezi kutunza Mtoto wako mpelekee Baba wa watoto wako. Uone kama atashindwa au atakupigia simu hata kukuomba thumni

Kwanza kwa hela gani mnazowapa hao wanawake hadi muone kwamba zinatosha kuhudumia watoto wenu na bado hao wanawake wafanyie matumizi yao, hakuna anayewalazimisha kiasi cha kutoa ninyi toeni kiasi ambacho mnaona hiki kinatosha matumizi ya mtoto wa umri fulani mama atajijua mwenyewe, kama ni ada muambie mama atafute shule ambayo utaweza kumudu akitaka shule yenye gharama zaidi wewe lipa ada unayomudu hiyo ada nyingine ataongezea mama yake mwenyewe

Sasa hela gani Kwa nini mnahangaika nazo na mnazihitaji.
Anayekaa na mtoto ndiye anatakiwa kujua mtoto atakula nini, atalala wapi, atavaa nini na atasoma wapi
Kwa nini asiyekaa naye aseme au aulizwe?

Kama umeng'ang'ania mtoto beba jukumu la malezi na matunzo
Au mpe Babaake uone kama utaulizwa hata swali Moja au utasumbuliwa.
Mwanaume atashughikia mambo ya mtoto wake Akiwa hapo Nyumba kwake

Kung'ang'ania kukaa na mtoto alafu huwezi kumhudumia ni kujipa umuhimu ambao hauna.

Kutaka kuonekana unaweza kumbe huwezi lolote bila Msaada

Mwanamke anayejitambua na mama Bora huwezi mkuta anang'a ng'ania Kuishi na mtoto ambaye hawezi kumtunza. WANAWAKE Bora wakiamua Kuishi na watoto wao husimamia kila kitu bila kumtegemea Mtu yeyote ikiwemo Baba wa watoto. Huyo ndiye MWANAMKE

Yani kuhudumia mtoto ni jukumu la baba haijalishi mko kwenye ndoa au la ndio maana hata kisheria baba akifariki kama aliacha na watoto wa nje nao hutakiwa kupewa mgawanyo wa mali, sawa na watoto wa ndani ya ndoa bila kujali mama zao wana wanaume wengine au la na wala hawasemi kwamba eti kwa vile walishaachana basi watoto wa nje hawastahili kupata huo mgao, kisa eti mama zao walikuwa na viburi sijui ujeuri kwa hao wababa what a lame excuse from someone calling himself a father

Kuhudumia mtoto ambaye anaishi na mama mshenzi, asiye na Adabu, mkosa maadili hiyo mwanaume hawezi kutoa pesa .
Ni kutoa pesa kwaajili ya kuwafanya watoto wawe mashangingi, mashoga, wasagaji, na mambo mengine

Mama asiye na maadili ataweza kumkuza nani awe mtoto wa maana.
Mwanaume mwenye akili atakubali kupoteza watoto lakini kamwe hawezi kukubali kupoteza vyote yaani pesa na watoto pia.
Hebu hudumieni watoto wenu acheni visingizio kuna wanaume ndio chanzo cha wao na mama wa watoto zao kuachana kwa sababu zao binafsi lakini nao wanajificha kwenye kichaka hicho hicho cha kusingizia kuwa wanawake wana ujeuri na kiburi, sasa serikali ikisema iwasikilize wanaume kwenye hili basi kila mwanaume atasema hahudumii sababu mama watoto wake ni mjeuri na kiburi maana ndio sababu kubwa wanayoitoa wanaume wote waliotelekeza watoto wao hata kama ni uongo, mwisho wa siku mnawadhulumu watoto haki zao za msingi hudumieni watoto wenu hakuna aliyewaambia muwahudumie mama zao huo ugomvi wenu hautakiwi kuwahusu watoto

Ilimradi mwanaume ndiye mtoaji lazima mpokeaji aombe kwa Nidhamu na maadili.
Nje ya hapo mtawadhuru watoto.

Alafu kuna Jambo wanawake hamlijui kuhusu wanaume.
Nitalisemea Hilo baadae

Kuhusu baraka nimekuambia usidhani mimi ndio naanza kujifunza hapa kwenye bandiko lako na wala sihitaji kufanya ulichoniambia ili kuthibitisha hilo, sisi wengine huwa tunajifunza kupitia maisha ya watu wengine hatusubiri mpaka yatukute sisi eti ndio tuamini, ukiachilia mbali hawa tunaowaona ambao wewe hauwafahamu angalia mifano hata ya watu maarufu ambao unawafahamu niambie ni wangapi wenye ugomvi na baba zao halafu angalia hali zao za maisha zikoje
Nitajie mtu Mmoja wa maana mwenye mafanikio ya maana na yenye maadili ambaye anaugomvi na Baba yake.
Nitajie Mmoja tuu.
Ukipata huyo Mmoja nitaandika uzi hapa nikutumie Laki tano.

Kwamba mtu agombane na Baba yake na asiweke mambo Yake Sawa na awe na Kinyongo na Baba yake alafu afanikiwe kwenye ishu za maana. Huyo mtu hayupo na hajawahi kuzaliwa.

Au unazungumzia hawa waharibu maadili Wasanii wa Muziki, Waigizaji wanaokaa uchi, au Wasagaji au mashoga, au wauza madawa.
Maana hao kwenu ndio wamefanikiwa

Wewe nina mashaka na uwezo wako wa kupambanua hoja kwani kisheria mtoto anatakiwa kuanza kuishi rasmi na baba yake akiwa na umri gani, jibu ni miaka saba sasa mtoto wa miaka saba hawezi kuchagua kwamba anataka kuishi na baba au mama, narudia mtoto akiwa mdogo kwa asilimia kubwa anahitaji huduma ya mama yake na siyo tu mwanamke yeyote hata kama wewe unamuona mama yake ana tabia za hovyo ila ndio mama yake huwezi kubadili hilo
Mtoto anaruhusiwa kuishi na Babaake Muda wowote hata Akiwa na siku Moja kisheria.

Serikali haiwezi ruhusu mtoto aishi na Mama asiye na maadili Kesi za hivyo zipo na mifano ipo.

Na hii exactly ndio point yangu kwamba ukiacha kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha majukumu mengine yote kwa mtoto mzazi yeyote anaweza kuyafanya na ndio maana nikauliza kama mnayaweza kwanini sasa hamyafanyi, maana hata mkiletewa hao watoto bado mtawapa wanawake wengine wawalee huku ninyi mkitafuta pesa ila mwanamke akisema abaki nao mnataka afanye vyote yani awalee na awatafutie pesa sasa hapo nani mbinafsi

Hatufanyi kwa Wanawake wasio na maadili.

Serikali yenyewe haiwezi Kupoteza pesa zake sehemu ambayo inajua fika hapa itapata hasara.

Wewe kama hujiwezi kuwa mpole.

Jeuri waachie wanawake wenye vipato na kujiweza kiuchumi.

Sasa kinamwanamke kimekalia ujeuri kinanuka umaskini, kujilisha tuu chenyewe tuu ni shida alafu kinaleta jeuri. Alafu mwisho wa siku kinataka kuishi na watoto uwezo hakina, kinamtegemea aliyemzalisha na anayemletea jeuri ndio alishe Watoto.

Hiyo mtasubiri Sana
 
Kama baba .mwenye akili, na unawaza kuwa ke anachukua hela za mtoto kwa starehe, kalipie ada shule, mnunulie mtoto material things kama woana mke anafaidi sana.

Ni kosa kubwa kumhukumu mtoto kwa ugomvi wenu.
Sijui kwanini watu mnanaona mwanaume kutoa hela ndio kulea, ni sehemu ya matunzo tu.
 
Vipi mama akiamua kumleta kwako ila mtoto mwenyewe akachagua kuendelea kuishi na mama yake napo utagoma kumhudumia
Kwani anayeomba hizo huduma ni mama u mtoto?? Yaani wewe mama umeamua kubaki na mtoto, unalazimisha nini baba yake amhudumie? Wewe ukimhudumia peke yako haitoshi?? Ikiwa unaona kuwa haitoshi kwa maana ya umezidiwa mzigo sasa si bora umrudishe kwa anayeweza kumhudumia!!

Halafu watoto huwa wanaulizwa wachague pa kukaa ikiwa wazazi wote mnagombania huyo mtoto, ila sasa kama wazazi mnaridhia mtoto akae kwa mzazi fulani, hakuna nafasi atayopewa mtoto kuchagua pa kukaa.

Kina mama hawawapendi watoto wao, bali huwa wanapenda hela inayotokana na uwepo wa hao watoto (child support). Mroto anakuwa chambo tu
 
Sasa hapo si mtoto anakua amekukana yeye mwenyewe?? Atafundishwa the hard way. Ni kama tu baba upambane home pakapikwa ugali na maharage halafu watoto wagome kula wakitaka samaki. Hao wanakuwa ni wakubwa tayari, wakajitegemee na kujitafutia samaki.
 
Wanawake wanaweza kuwa wabinafsi ila hata siku moja hawawezi kuwa wabinafsi kwa watu wanaowapenda hasa watoto wao wa kuwazaa
Thubutu, Kuna wanawake wapo radhi mtoto akalelewe vijijini kwa Bibi zao kuliko kumpatia Baba hata kama ana uwezo
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Juliana Shonza lazima uelewe hakuna Baba asiyeweza kutunza Mtoto wake. Huyo Baba hayupo.

Kama wanawake wametelekezwa kwa Sababu zozote zile kama hizo ulizotaja ikiwemo jeuri na kiburi Acha wapambane na Hali Zao.

Sisi wanaume hatuwezi kutoa pesa na kutunza watoto lafu hiyo Moto ilelewe na Mama asiye na Adabu, mwenye dharau na kiburi. Hatuwezi kufanya kitu kama hicho Sisi kama Wanaume. Tunajua matokeo yake.

Unafikiri kama mama analeta dharau na kiburi kwa mwanaume anaweza kumlea Nani akawa mtu wa maana. Si ndio haya matoto ya siku hizi yasiyo na Adabu.

Wewe mwanamke kama unataka kuishi na mtoto wako Hakikisha unauwezo wa kumtunza mtoto au watoto wako full stop.

Kwanza kitendo cha Mama kushindwa kumtunza mtoto wake aliyemzaa kina m- disqualify kuwa Mama.
Yaani Mpaka umtegemee mtu mwingine akulelee watoto uliozaa mwenyewe. KWELI? Hata Wanyama wenyewe watakushangaa Sana.

Juliana Shonza, waambie wanawake wenzako kama imetokea mmetengana, na mwanaume analegalega kutoa matunzo. Mama apambane na Hali yake. Na kama hawezi apeleke watoto kwa Baba yake.

Mtu huna uwezo wa kutunza au kulea watoto wako kinachokufanya uwang'ang'anie ni nini kama sio Roho Mbaya na ushenzi, ubinafsi, ukatili na tabia za kishetani.

Mimi nawajua watoto wengi wanaolelewa na Baba zao na wapo wanaume maarufu Duniani wanalea watoto wao wenyewe tena kwa amani Kabisa.
Watoto wanaishi maisha Safi Kabisa. Kinachokufanya wewe mwanamke umng'ang'anie mtoto ilhali huna uwezo wa kumhudumia ni nini kama sio ushetani na ubinafsi wako?

Kama Baba yake hawezi kumtunza mtoto kwa nini uombe matumizi ya mtoto kutoka kwake?
Acheni ushetani!
Acheni ubinafsi!
Acheni ukatili!

Wanaume wakilea watoto huwezi kuta wanasumbuana na mama watoto. Yaani mtoto anakuwa bila Kesi Wala mazonge. Hakuna kelele mambo yanaenda.
Tena huwezi kuta Baba Akiwa anamlea mtoto wake akamsema Mama vibaya hata kama huyo mama angekuwa anatabia za kiajabuajabu.

Hakuna aliyewazua wanawake kujishughulisha na mambo ya kiuchumi. Dunia ya sasa kila mtu yupo Huru.

Wanaume ambacho hatutakubali Dunia iende irudi ni kukosewa Heshima.

Wewe Mwanamke umezingua, unaleta dharau na Ujuaji. Alafu upo na watoto wangu. Hutaki kunipa alafu utegemee Mimi hao watoto niwachukulie kama watoto wangu kikamilifu. KWELI! Hivi Mnafikiri wanaume ni kama ninyi?

Hakuna mwanaume wa hivyo.
Wanaume tunajua, mwanamke mpumbavu lazima aambukize upumbavu wake kwa watoto.

Yaani uniletee upumbavu alafu kwa upumbavu wako utegemee sijui kuna serikali sijui kitu gani kitanilazimisha niwachukulie watoto unaowalea kama watoto wangu. KWELI?
Hata hao watu serikalini nao watakuwa wawatumii akili sawasawa.

Serikali yenyewe ukiwa upande wa upinzani kuna namna inavyokuchulia ndivyo hivyohivyo katika mambo Mengine.

Wanawake mjue na hili ni tangazo hata kwa watoto wapumbavu kuwa,
Sisi wanaume inapotokea tumezaa na mwanamke mpumbavu asiye na hekima, mwenye kiburi, dharau, asiye na maadili, Kahaba. Tunaamini kuwa tumepoteza.

Hatuhesabu kama tuna watoto na hao Wanawake. Labda wanawake watukabidhi hao watoto tuwalee na kuwakuza Sisi wenyewe na sio vinginevyo.

Na Sisi kama Wanaume na Baba, hatutegemei Jambo lolote kutoka kwa watoto zaidi ya watoto kuwa na maadili mazuri na wenye kuleta heshima katika Jamii.
Sasa kama Mwanamke anadharau na kiburi kwa mwanaume aliyemzalisha unategemea atamlea na kumkuza mtoto kuwa na sifa ya maadili au Jambo la maana lenye kumfanya Baba ajivunie?
Jibu ni Hapana!

Kuna wanawake wapumbavu ambao hudhani akili Zao za kupenda pesa hufikiri na sisi wanaume Tupo hivyo kama wao.
Ndio maana wengi wao husema, ngoja mtoto akue afanikiwe utaleta miguu yako hapa.
Sasa mtoto hata akifanikiwa alafu ni shoga unategemea mwanaume atajivunia huyo mtoto. Au mtoto kakua kafanikiwa lakini anakaa uchi mitandaoni huko au anauza madawa au ni danga unafikiri kuna Baba anajivunia huo upuuzi!

Tutahudumia watoto wetu lakini sio kwa kuweka rehani heshima zetu. Never ever. Tupo radhi Twende Jela.

Namna pekee ya mwanamke kudai pesa na huduma ya watoto hata kama umeachana na mwanaume ni kuwa mtiifu na mwenye maadili.

Lakini ukijifanya kichwa ngumu nakuhakikishia watoto hao unawaingiza mkenge.

Mnasababisha watoto wanapata Laana kijingajinga Kisa maujinga yenu.
Sasa kama Baba hajaridhia kutoa huduma, au anatoa huduma huku anasononeka hivi hao watoto watafika wapi zaidi ya kuleta Laana kwenye jamii na nchi.

Huko Ulaya mashoga na mambo ya ajabu yanazidi kuongezeka kwa Sababu hiyohiyo.

Inajulikana Baraka za mtoto zinatoka kwa Baba yake Hilo hakuna ambaye atabisha Dunia iende irudi.
Sasa mtoto kama Hana Baraka za Babaake unategemea atakuwa nala maana au zaidi atazidi kusongwa na matatizo na kuleta matatizo.

Mama mtu unagombana na Baba wa watoto wako. HUNA Adabu au labda yeye ni mkorofi lakini unakosa Busara ya kudili na Kesi ndogo kama hizo.
Hivi kama Mama unagombana na Baba watoto kwa kiwango cha dharau unategemea watoto wako Wapate Baraka za Baba kweli?
Au kuna Baba Mwingine?

Uliambiwa serikali inatoa Baraka?
Au uliambiwa Wanasiasa watampa mtoto wako Baraka?
Au uliambiwa ustawi wa jamii ndio watawapa watoto wako Baraka?

Wanawake Kila siku nawaambieni shetani anacheza na nyie kwa akili kubwa na ninyi hamjui Hilo.

Mmegombana na Mumeo Sawa. Mmetengana Sawa.
Zungumzeni kwa Wema Nani akae na watoto. Zingatieni Yule mwenye uwezo wa kiuchumi ndiye akae na watoto.

Ikiwa Baba atakataa kukaa na watoto akakuambia ukae naye. Mwambie atoe Pesa za matumizi na muandikishane.

Mbona rahisi Sana
Lakini sio ulazimishe ukae na watoto alafu matumizi utegemee kwa mwanaume. Wewe ni chizi unayetafuta Laana za kijinga kwa watoto.

Kama Baba hajaridhia ukae na watoto wake unategemea atawaangalia kama watoto wake? Unafikiri atawabariki kwa moyo mkunjufu.
Pumbavu! Tumieni Akili. Haya.

Acha nipumzike!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
hivi yule mdogo wake aliyeolewa na mwanamke mwenzie, yule mwanamke wa geita aliyechinjwa, ujane wake unaendeleaje?
 
Hii ndio shida ya kuwa na uelewa MDOGO.

Watoto wa nje ya ndoa hawawezi kuwa na thamani na wa ndani ya ndoa. Hiyo iko hivyohivyo. Dunia iende au irudi. Kwa sababu Hilo Jambo lipo naturally. Wa Nje atabaki Nje na WA ndani atabaki ndani. Mengine ni kulazimisha tuu vitu.
Ndio maana nikakuuliza ni kanuni gani ya kiulimwengu inayoamua kwamba, mtoto wa nje ya ndoa hawezi kuwa na thamani sawa na mtoto wa ndani ya ndoa, kama hakuna hiyo kanuni basi clearly ni wewe ndiye unayelazimisha vitu hapa

Halafu sijui ukoje huwa unahisi unajua kila kitu na uko sahihi kwenye kila kitu, kwamba mawazo yako ni kama sheria yani unataka unapoleta mada hapa jf basi kila mtu akuunge mkono, na mtu yeyote anayekupinga unamuona kama ana matatizo hivi akili yako iko sawasawa

Wajibu wako kwa mtoto wako unatokana na ushiriki wako katika kuzaliwa huyo mtoto na si vinginevyo, kutokuishi na huyo mtoto siyo sababu ya kugoma kumhudumia na ndio maana nikakupa huo mfano, kuwa hata sheria za nchi mbalimbali duniani zinamtambua mtoto wa nje ya ndoa katika mgawanyo wa mali
Kama Wamama wanachangia kwenye malezi mbona wanataka wanaume wahusika kutoa huduma.
Ofcourse kwa sababu ukitoa huduma za kiuchumi wewe baba huna jukumu lingine lolote kwa mtoto, sasa usipotoa hizo huduma wewe utakuwa na wajibu gani kwa huyo mtoto unataka mama ahangaike mwenyewe huku wewe ukila maisha tu siyo, na tutakomeshaje tabia ya wanaume kuzalisha hovyo ikiwa tunaona ni sawa tu wao kutowajibishwa na kukwepa majukumu kwa sababu za kipumbavu kama hizo
Mbona mtoto akikaa kwa Baba yake huwezi sikia Mwanaume akisema Mama yake hatoi huduma. Yaani hata ukipotea Moja Kwa Moja mwanaume hawezi kuwa na habari na wewe na Wala hatahitaji chochote kutoka kwako?

Hoja ya Mada yangu ni kuwa, wewe kama Mama huwezi kutunza Mtoto wako mpelekee Baba wa watoto wako. Uone kama atashindwa au atakupigia simu hata kukuomba thumni
Hiyo hoja ya kwamba baba akiishi na mtoto mbona haombi matunzo kwa mama wa mtoto hivi huwa hamuoni aibu kuitoa, yani unaombaje matunzo ya mtoto kwa mtu ambaye kwa asilimia kubwa ndio amechangia ukuaji wa mtoto huku wewe kazi yako ikiwa kumwaga mbegu tu, huo ni mgawanyo wa majukumu mkitaka wanawake nao wawe wanachangia huduma za mtoto kiuchumi basi nanyi anzeni kuchangia malezi ya mtoto toka akiwa mchanga zile hekaheka zote wanazopitia kina mama nanyi mshiriki kisha ndio mje muongee nao lugha moja
Sasa hela gani Kwa nini mnahangaika nazo na mnazihitaji.
Anayekaa na mtoto ndiye anatakiwa kujua mtoto atakula nini, atalala wapi, atavaa nini na atasoma wapi
Kwa nini asiyekaa naye aseme au aulizwe?

Kama umeng'ang'ania mtoto beba jukumu la malezi na matunzo
Au mpe Babaake uone kama utaulizwa hata swali Moja au utasumbuliwa.
Mwanaume atashughikia mambo ya mtoto wake Akiwa hapo Nyumba kwake

Kung'ang'ania kukaa na mtoto alafu huwezi kumhudumia ni kujipa umuhimu ambao hauna.

Kutaka kuonekana unaweza kumbe huwezi lolote bila Msaada
Hizo hela hawazihitaji wanawake bali wanazihitaji watoto, kama mnaona hao wanawake hawashiriki kwenye kuhudumia watoto, na kwamba hizo hela mkiwapa wanazitumia wao basi niambie hao watoto wanaishije
Mwanamke anayejitambua na mama Bora huwezi mkuta anang'a ng'ania Kuishi na mtoto ambaye hawezi kumtunza. WANAWAKE Bora wakiamua Kuishi na watoto wao husimamia kila kitu bila kumtegemea Mtu yeyote ikiwemo Baba wa watoto. Huyo ndiye MWANAMKE
Ni wapi imeandikwa kwamba mama bora ni yule ambaye analea mtoto peke yake baada ya kutelekezewa na baba, ninyi si ndio huwa mnawatukana single mothers wote kwa ujumla kwa kitendo chao cha kuzaa kabla ya ndoa bila kujali kama hao wanaume wanahudumia watoto au la, leo hii mnageuza kibao tena kusema wanawake waliotelekezewa watoto na wanawahudumia peke yao hao ndio wamama bora kwahiyo na hao wanaume waliotelekeza hao watoto nao ni wababa bora siyo
Kuhudumia mtoto ambaye anaishi na mama mshenzi, asiye na Adabu, mkosa maadili hiyo mwanaume hawezi kutoa pesa .
Ni kutoa pesa kwaajili ya kuwafanya watoto wawe mashangingi, mashoga, wasagaji, na mambo mengine

Mama asiye na maadili ataweza kumkuza nani awe mtoto wa maana.
Mwanaume mwenye akili atakubali kupoteza watoto lakini kamwe hawezi kukubali kupoteza vyote yaani pesa na watoto pia.
Kwamba unataka kusema, watoto wanaolelewa na single mothers tu ndio hawana maadili, ila wale wanaolelewa na baba zao au na wazazi wote wawili ndio huwa na maadili siyo

Kwamba hawa watu wote waliokuja kuwa wezi, vibaka, wazinzi, mashoga, mafisadi, matapeli nk wote hao wamelelewa na single mothers tu, na kwamba hakuna kati yao waliolelewa na baba zao au wazazi wote wawili

Halafu nikikuambia kwamba unaassume wababa ndio huwa watakatifu sana katika malezi ya watoto wao unabisha sasa unabisha nini ilihali huna hoja, yani hawa wababa tunaosikia kila siku wanabaka na kulawiti watoto wao na kuwafundisha tabia za hovyo kama ulevi na uhuni, ndio unataka kutuambia wao ndio wanafaa kuaminiwa kuachiwa full custody ya watoto kuliko kina mama
Ilimradi mwanaume ndiye mtoaji lazima mpokeaji aombe kwa Nidhamu na maadili.
Nje ya hapo mtawadhuru watoto.

Alafu kuna Jambo wanawake hamlijui kuhusu wanaume.
Nitalisemea Hilo baadae
Sasa unataka mpokeaji aombe kwa nidhamu na maadili kwani anaomba kwa ajili yake au anaomba kwa ajili ya kiumbe ulichoshiriki kukileta duniani, ingekuwa huyo mwanamke anaomba hizo huduma kwa ajili yake basi hata nami ningemshauri aombe kwa unyenyekevu kwa sababu siyo wajibu wako kumhudumia, ila unataka kuombwa kwa unyenyekevu kwa kiumbe ambacho ni wajibu wako kukihudumia we ulisikia wapi na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni gani
Nitajie mtu Mmoja wa maana mwenye mafanikio ya maana na yenye maadili ambaye anaugomvi na Baba yake.
Nitajie Mmoja tuu.
Ukipata huyo Mmoja nitaandika uzi hapa nikutumie Laki tano.

Kwamba mtu agombane na Baba yake na asiweke mambo Yake Sawa na awe na Kinyongo na Baba yake alafu afanikiwe kwenye ishu za maana. Huyo mtu hayupo na hajawahi kuzaliwa.

Au unazungumzia hawa waharibu maadili Wasanii wa Muziki, Waigizaji wanaokaa uchi, au Wasagaji au mashoga, au wauza madawa.
Maana hao kwenu ndio wamefanikiwa
Hakuna mahali nimewataja hao unaowazungumzia wewe kama mifano bali umejihami tu kwa sababu moja kwa moja akili yako ndio imekupeleka huko, kwamba unataka kusema watu wote waliofanikiwa kwenye nyanja mbalimbali duniani hawapo ambao wametelekezwa na kuwa na uhasama na baba zao, halafu hata hao hao ambao unaona mafanikio yao hayana maana mbona tunawaona baba zao ndio huwa wa kwanza kuwalilia wamalize tofauti zao na wawasaidie kiuchumi
Mtoto anaruhusiwa kuishi na Babaake Muda wowote hata Akiwa na siku Moja kisheria.

Serikali haiwezi ruhusu mtoto aishi na Mama asiye na maadili Kesi za hivyo zipo na mifano ipo.
Serikali inapimaje hayo maadili na inajuaje kama siku zote ni mama tu ndio huwa hana maadili, ila baba pekee ndio mwenye maadili au ni serikali ya kichwani kwako, unajua unapojenga hoja zako elezea uhalali wake vinginevyo useme kuwa haya yote unayoyaandika ni mawazo yako pamoja na wanaume wapumbavu kama wewe
Hatufanyi kwa Wanawake wasio na maadili.

Serikali yenyewe haiwezi Kupoteza pesa zake sehemu ambayo inajua fika hapa itapata hasara.
Acha kutoa mifano ambayo ni irrelevant hiyo serikali haiwezi kufanya hivyo ikiwa inajua inafanya hilo jambo kwa hisani na inatoa pesa zake mfukoni, ila kama inatumia kodi za wananchi hakuna serikali yenye jeuri ya kusema hilo hadharani labda kama imechoka kutawala, jambo ambalo ni wajibu wa serikali basi serikali haina budi kuangalia faida wala hasara bali inatakiwa itekeleze hilo jambo kwa sababu ndicho kilichofanya hiyo serikali iwepo hapo
Wewe kama hujiwezi kuwa mpole.

Jeuri waachie wanawake wenye vipato na kujiweza kiuchumi.
Sasa kinamwanamke kimekalia ujeuri kinanuka umaskini, kujilisha tuu chenyewe tuu ni shida alafu kinaleta jeuri. Alafu mwisho wa siku kinataka kuishi na watoto uwezo hakina, kinamtegemea aliyemzalisha na anayemletea jeuri ndio alishe Watoto.

Hiyo mtasubiri Sana
Sasa kama mnajua kuwa wanawake wa hivyo hawafai huwa mnawazalisha wa nini najua utasema mwenye maamuzi ya kuzaa ni mwanamke, sasa kama hamtaki kuzaa na hao wanawake huwa mnatembea nao wa nini kama mnajua kwamba wanawake masikini wana tabia ya kujibebesha mimba ili wapate child support, kwanini msitembee na wanawake matajiri tu ili hata mkizaa nao wasiwasumbue kuhudumia watoto kwanini hamtaki kuwajibika kwa makosa yenu you always just want to get away with it
Kwani anayeomba hizo huduma ni mama u mtoto?? Yaani wewe mama umeamua kubaki na mtoto, unalazimisha nini baba yake amhudumie? Wewe ukimhudumia peke yako haitoshi?? Ikiwa unaona kuwa haitoshi kwa maana ya umezidiwa mzigo sasa si bora umrudishe kwa anayeweza kumhudumia!!
Hizo huduma anayeomba ni mama ila anayezihitaji ni mtoto na yeye hawezi kuziomba au unataka kusema wamama ndio wanaozitumia hizo pesa na kama wanazitumia hao watoto wanaishije, wajibu wa baba kwa mtoto uko katika kushiriki kumleta huyo mtoto duniani na siyo kuishi naye tu, ndio maana sheria zinatambua hata mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kupata mgawanyo wa mali pale baba anapofariki bila kujali alikuwa anaishi naye au la
Halafu watoto huwa wanaulizwa wachague pa kukaa ikiwa wazazi wote mnagombania huyo mtoto, ila sasa kama wazazi mnaridhia mtoto akae kwa mzazi fulani, hakuna nafasi atayopewa mtoto kuchagua pa kukaa.
Ndio hapa tunaongelea pale ambapo wazazi wanagombania kuishi na mtoto, ndio nikauliza vipi mtoto akiamua kuchagua kuishi na mama bila shinikizo lolote, ni kanuni au sheria gani inayoamua au inayosema kwamba baba ana wajibu wa kuhudumia mtoto endapo anaishi naye tu
Kina mama hawawapendi watoto wao, bali huwa wanapenda hela inayotokana na uwepo wa hao watoto (child support). Mroto anakuwa chambo tu
Aiseee kweli nazidi kuamini kuwa kadiri miaka inavyozidi kuenda ndivyo jinsia yenu inavyozidi kupoteza uwezo wa kufikiri na kujenga hoja bali mnatumia mihemko badala ya logic, kwamba unataka kusema mwanamke analeta duniani na kukikuza kiumbe ambacho hakipendi kwa ajili ya hela tu, haya na mnapokataa kutoa hizo huduma nini huwa kinafuata je hao wanawake huwa wanawatelekeza au wanawaua hao watoto kisa wamekosa hizo pesa au
Thubutu, Kuna wanawake wapo radhi mtoto akalelewe vijijini kwa Bibi zao kuliko kumpatia Baba hata kama ana uwezo
Ukiona hivyo ujue hao wamama hawataki watoto zao wakalelewe na wamama wa kambo maana wanajua hasara zake
 
Hamna chochote, roho mbaya tu
Mtoto analelewa na Baba mzaa Mama ila mtu yupo tayari kuua future ya mtoto kijijini
 
Ndio maana nikakuuliza ni kanuni gani ya kiulimwengu inayoamua kwamba, mtoto wa nje ya ndoa hawezi kuwa na thamani sawa na mtoto wa ndani ya ndoa, kama hakuna hiyo kanuni basi clearly ni wewe ndiye unayelazimisha vitu hapa

Halafu sijui ukoje huwa unahisi unajua kila kitu na uko sahihi kwenye kila kitu, kwamba mawazo yako ni kama sheria yani unataka unapoleta mada hapa jf basi kila mtu akuunge mkono, na mtu yeyote anayekupinga unamuona kama ana matatizo hivi akili yako iko sawasawa

Wajibu wako kwa mtoto wako unatokana na ushiriki wako katika kuzaliwa huyo mtoto na si vinginevyo, kutokuishi na huyo mtoto siyo sababu ya kugoma kumhudumia na ndio maana nikakupa huo mfano, kuwa hata sheria za nchi mbalimbali duniani zinamtambua mtoto wa nje ya ndoa katika mgawanyo wa mali

Ofcourse kwa sababu ukitoa huduma za kiuchumi wewe baba huna jukumu lingine lolote kwa mtoto, sasa usipotoa hizo huduma wewe utakuwa na wajibu gani kwa huyo mtoto unataka mama ahangaike mwenyewe huku wewe ukila maisha tu siyo, na tutakomeshaje tabia ya wanaume kuzalisha hovyo ikiwa tunaona ni sawa tu wao kutowajibishwa na kukwepa majukumu kwa sababu za kipumbavu kama hizo

Hiyo hoja ya kwamba baba akiishi na mtoto mbona haombi matunzo kwa mama wa mtoto hivi huwa hamuoni aibu kuitoa, yani unaombaje matunzo ya mtoto kwa mtu ambaye kwa asilimia kubwa ndio amechangia ukuaji wa mtoto huku wewe kazi yako ikiwa kumwaga mbegu tu, huo ni mgawanyo wa majukumu mkitaka wanawake nao wawe wanachangia huduma za mtoto kiuchumi basi nanyi anzeni kuchangia malezi ya mtoto toka akiwa mchanga zile hekaheka zote wanazopitia kina mama nanyi mshiriki kisha ndio mje muongee nao lugha moja

Hizo hela hawazihitaji wanawake bali wanazihitaji watoto, kama mnaona hao wanawake hawashiriki kwenye kuhudumia watoto, na kwamba hizo hela mkiwapa wanazitumia wao basi niambie hao watoto wanaishije

Ni wapi imeandikwa kwamba mama bora ni yule ambaye analea mtoto peke yake baada ya kutelekezewa na baba, ninyi si ndio huwa mnawatukana single mothers wote kwa ujumla kwa kitendo chao cha kuzaa kabla ya ndoa bila kujali kama hao wanaume wanahudumia watoto au la, leo hii mnageuza kibao tena kusema wanawake waliotelekezewa watoto na wanawahudumia peke yao hao ndio wamama bora kwahiyo na hao wanaume waliotelekeza hao watoto nao ni wababa bora siyo

Kwamba unataka kusema, watoto wanaolelewa na single mothers tu ndio hawana maadili, ila wale wanaolelewa na baba zao au na wazazi wote wawili ndio huwa na maadili siyo

Kwamba hawa watu wote waliokuja kuwa wezi, vibaka, wazinzi, mashoga, mafisadi, matapeli nk wote hao wamelelewa na single mothers tu, na kwamba hakuna kati yao waliolelewa na baba zao au wazazi wote wawili

Halafu nikikuambia kwamba unaassume wababa ndio huwa watakatifu sana katika malezi ya watoto wao unabisha sasa unabisha nini ilihali huna hoja, yani hawa wababa tunaosikia kila siku wanabaka na kulawiti watoto wao na kuwafundisha tabia za hovyo kama ulevi na uhuni, ndio unataka kutuambia wao ndio wanafaa kuaminiwa kuachiwa full custody ya watoto kuliko kina mama

Sasa unataka mpokeaji aombe kwa nidhamu na maadili kwani anaomba kwa ajili yake au anaomba kwa ajili ya kiumbe ulichoshiriki kukileta duniani, ingekuwa huyo mwanamke anaomba hizo huduma kwa ajili yake basi hata nami ningemshauri aombe kwa unyenyekevu kwa sababu siyo wajibu wako kumhudumia, ila unataka kuombwa kwa unyenyekevu kwa kiumbe ambacho ni wajibu wako kukihudumia we ulisikia wapi na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni gani

Hakuna mahali nimewataja hao unaowazungumzia wewe kama mifano bali umejihami tu kwa sababu moja kwa moja akili yako ndio imekupeleka huko, kwamba unataka kusema watu wote waliofanikiwa kwenye nyanja mbalimbali duniani hawapo ambao wametelekezwa na kuwa na uhasama na baba zao, halafu hata hao hao ambao unaona mafanikio yao hayana maana mbona tunawaona baba zao ndio huwa wa kwanza kuwalilia wamalize tofauti zao na wawasaidie kiuchumi

Serikali inapimaje hayo maadili na inajuaje kama siku zote ni mama tu ndio huwa hana maadili, ila baba pekee ndio mwenye maadili au ni serikali ya kichwani kwako, unajua unapojenga hoja zako elezea uhalali wake vinginevyo useme kuwa haya yote unayoyaandika ni mawazo yako pamoja na wanaume wapumbavu kama wewe

Acha kutoa mifano ambayo ni irrelevant hiyo serikali haiwezi kufanya hivyo ikiwa inajua inafanya hilo jambo kwa hisani na inatoa pesa zake mfukoni, ila kama inatumia kodi za wananchi hakuna serikali yenye jeuri ya kusema hilo hadharani labda kama imechoka kutawala, jambo ambalo ni wajibu wa serikali basi serikali haina budi kuangalia faida wala hasara bali inatakiwa itekeleze hilo jambo kwa sababu ndicho kilichofanya hiyo serikali iwepo hapo

Sasa kama mnajua kuwa wanawake wa hivyo hawafai huwa mnawazalisha wa nini najua utasema mwenye maamuzi ya kuzaa ni mwanamke, sasa kama hamtaki kuzaa na hao wanawake huwa mnatembea nao wa nini kama mnajua kwamba wanawake masikini wana tabia ya kujibebesha mimba ili wapate child support, kwanini msitembee na wanawake matajiri tu ili hata mkizaa nao wasiwasumbue kuhudumia watoto kwanini hamtaki kuwajibika kwa makosa yenu you always just want to get away with it

Hizo huduma anayeomba ni mama ila anayezihitaji ni mtoto na yeye hawezi kuziomba au unataka kusema wamama ndio wanaozitumia hizo pesa na kama wanazitumia hao watoto wanaishije, wajibu wa baba kwa mtoto uko katika kushiriki kumleta huyo mtoto duniani na siyo kuishi naye tu, ndio maana sheria zinatambua hata mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya kupata mgawanyo wa mali pale baba anapofariki bila kujali alikuwa anaishi naye au la

Ukiona hivyo ujue hao wamama hawataki watoto zao wakalelewe na wamama wa kambo maana wanajua hasara zake

Na sisi hatutaki watoto wetu wakalelewe na Baba wa kambo. Kwa sababu tunajua hasara Zake.

Wewe Ka huwezi kutunza Mtoto wako mwenyewe uliyemzaa unamtegemea mwanaume ni kwamba hata Panya au Kuku wanakushinda Akili.

Mama ni Yule mwenye uwezo wa kutunza watoto wake. Kama huwezi huna sifa za kuitwa Mama.
 
Baba wa kambo anachangia malezi gani kwa mtoto tofauti na ya kiuchumi, toka lini baba akahusika direct kwenye malezi ya watoto (let alone huyo wa kambo), au we hujiulizi kwanini mtoto akiharibikiwa anayetupiwa lawama nyingi ni mama

We sema kabisa kuwa hayo ni mawazo yako binafsi na siyo kanuni ili ijulikane kuwa huna akili, maana uko huru kuwaza vyovyote hata kama ni ujinga ila shida inakuja pale, unapolazimisha huo ujinga wako ndio uwe uhalisia na kila mtu auunge mkono upite bila kupingwa

Vinginevyo serikali nyingi za dunia zisingeweka sheria ya child support toka kwa baba kuenda kwa mama tu, (aliyeachiwa watoto) na si kinyume chake au unataka kusema wewe ndio una akili sana, kuliko serikali nyingi duniani na wanaume wote wanaohudumia watoto wao wanaoishi na mama zao siyo
 
Hamna chochote, roho mbaya tu
Mtoto analelewa na Baba mzaa Mama ila mtu yupo tayari kuua future ya mtoto kijijini
Aliyekuambia mtoto akikaa kijijini future yake inaharibika nani, kwanza ninyi si ndio huwa mnasema huku mijini watoto ndio wameharibikiwa kuliko wa vijijini, una takwimu zozote zinazoonesha kuwa watoto wa vijijini ndio future zao huharibika kuliko wa mijini
 
Back
Top Bottom