:
#NUKUU_MWL_NYERERE: Ikulu ni mahali patakatifu. Mimi nimekaa pale Ikulu miaka 24 ambayo Rais mwingine kwa mujibu wa katiba tuliyonayo hataweza kukaa kama mimi, pengine kwa udikiteta. Kwa mtu muungwana, Ikulu ni mzigo. Ukiona mwanasiasa anapenda kukimbilia kwenda Ikulu, basi huyo mwogopeni kama Ukoma. Yawezekana amenunuliwa, na kama amenunuliwa, hizo fedha atazirudishaje? Kwani pale Ikulu kuna biashara gani?
--------------------------------------------------------------------------
Baada ya kujivuta na kusuasua kwa kipindi kirefu licha ya kuonekana utovu wa nidhamu pamoja na viashiria vya wazi vya kupanga kukihujumu Chama, serikali na Rais aliyeko madarakani, hatimaye Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya maamuzi magumu japokuwa kilichelewa yakiwemo ya kumvua uanachama kada wake mkongwe aliyekosa nidhamu kwa Chama kwa kiwango cha kupindukia, na huyu si mwingine bali ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mjumbe wa Kamati kuu, Halmashauri kuu kwenye awamu ya serikali iliyopita Mhe. Benard Camillius Membe.
Licha wa kuvuliwa uanachama kwa Benard Camillius Membe, wengine waliokumbwa na fagio la chuma ni waliowahi kuwa Makatibu Wakuu wa Chama hicho Mhe. Yusuf Makamba, aliyepewa msamaha baada ya kuandika barua kuomba msamaha na kukiri makosa pamoja na Abdulrahaman Kinana aliyepewa karipio kali pamoja na kuwekwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miezi 18 ikiwemo kuzuiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi.
Kwangu mimi, hatua hizi zilizochukuliwa na Chama cha Mapinduzi napaswa kuzipongeza kwa dhati kwani, nguzo kuu ya uhai wa Chama chochote cha siasa mahali popote duniani ni #Nidhamu. Hii ni kwa sababu, siri kubwa ya vyama vya kisiasa vilivyoko madarakani kwa kipindi kirefu kama Ccm na vile vilivyoko upinzani, ili viendelee kuwepo na kustawi, \
nidhamu kwa viongozi, makada pamoja na wanachama wake ndiyo silaha yao ya kwanza. Tuchukulie kwa mfano vyama vikongwe vya siasa duniani kikiwemo Chama cha Kikomunisti cha China, Chama cha Kikomunisti cha Cuba pamoja na Chama cha Kikomunisti cha Urusi, nidhamu kwa viongozi wake, Utii wa makada na wanachama kwa Chsma chao, ndiyo imeviwezesha vyama hivi kuendelea kuongoza mataifa yake kwa ufanisi mkubwa hadi sasa, licha ya kupitia changamoto mbali mbali zikiwemo siasa baridi pamoja na vita vya kiuchumi.
Kimalengo, Kimadhumuni na Kiitikadi ya kuunganishwa kwa vyama vya TANU (Bara) na ASP (Visiwani) kisha kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi, hakutofautiani sana na malengo, madhumuni na Itikadi ya kuanzishwa kwa vyama vikongwe nilivyovitaja hapo juu, ambapo ni kumkomboa mwananchi kifikra, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii, ikiwemo kujenga taifa la watu wenye usawa, haki na demokrasia.
Ni ukweli usiopingika kwamba, kwa miongo takribani mitatu (Miaka 30) Chama cha Mapinduzi kilitetereka kidogo au hata pakubwa. Chama kilipoteza dira, kilipoteza mwelekeo, kilitoka kwenye reli kikaacha malengo yake, madhumuni yake, na itikadi yake ya kuwakomboa nz kuwapigania wananchi masikini, wanyonge na badala yake kikaanza kupwaga na njia isiyo sahihi. Chama kikakumbatia maovu, ikiwemo rushwa, ufisadi, uzembe na kutowajibika kazini,
Ule mfumo wa Chama kuisimamia serikali ukafa na badala yake Chama ndicho kikageuka kuwa kichaka cha walanguzi na wanyang'anyi wa rasilimsli za nchi, na kama vile hiyo haitoshi, wenye meno wakafikia hatua ya kujitwalia na kujimilikisha mali za Chama, huku wenye kutafuta utajiri kwa kutumia fedha, wakajitwalia madaraka, fedha ikawa ndiyo mwamuzi wa fulani apewe cheo gani huku wenye sifa na uwezo wakizunguka mitaani, na kibaya kuliko vyote, nidhamu ndani ya Chama ikashuka,
Chama kikageuka kuwa mfano wa samaki kambale ambao kuanzia baba, mama na mtoto wote wana ndevu, na kwenye eneo hili ndipo wakazaliwa akina #HAAMBILIKI, mfano wa kina Benard Camillius Membe ambaye alipoitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama chake, akatoka huku akijitapa kwa majigambo lukuki, kama vile waliomwita ni wadogo, yeye ndiye mkubwa, akadiriki kujipa jina bandia la kukitisha Chama chake la #Niguse_Ninuke, lakini kwa sasa amenuka kweli.
Ni kufuatia kudorola kwa Ccm, nchi ikayumba kisiasa, kiuchumi, huduma za kijamii mfano Elimu, Maji, Afya, Umeme zikageuzwa kuwa sehemu ya bidhaa adimu. Mwenye fedha chafu ndiye akaabudiwa na jamii, huku watoto chini ya miaka mitano na mama wajawazito wakifariki kwa kukosa huduma bora za afya, achilia mbali elimu kugeuzwa kuwa biashara inayolipa kuliko watu kujenga viwanda. Kukazaliwa shule zilizoitwa Kayumba, huku mtoto wa mwenye nacho ndiye akawa na uhakika wa kufikia ndoto zake kielimu, na watoto wa masikini ikawa shida hata kuhitimu elimu ya msingi kutokana na ukubwa wa ada, michango lukuki isiyo na kikomo, mara leo mzazi lete hela ya dawati huku hata kumwandikisha mtoto darasa la kwanza sharti likawa fedha.
Kutokana na vikwazo hivyo, watoto wengi wa masikini wakaishia kukimbilia mijini kufanya shughuli za kimachinga ambazo nazo wslikumbsna na rungu la mgambo wa Manispaa ikiwemo kupigwa na kuporwa bidhaa zao, achilia mbali wasichana walioshindwa kuendelea na masomo au waliohitimu darasa la saba kusombwa vijijini na kwenda kutumikishwa kazi za ndani mijini. Haya yote yanafanyika huku Benard Camillius Membe akiwa Waziri serikalini, akiwa mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya Chama tawala. Haya yote ysnafanyika wakati Yusuf Maksmba na Abdulrahman Kinana wakiwa watendaji wakuu wa Chama tawala kilichoshindwa kuisimamia serikali.
Wananchi walipoona hawana mtetezi, wakaona isiwe taabu, wakaamua kumkumbatia shetani Chadema kuliko kuikumbatia Ccm. Hii ni baada ya shetani Chadema aliyeibuka na vazi la kondoo la sera ya kupinga rushwa, kutetea rasilimali za nchi zisiporwe kumbe ni mbwa mwitu walewale. Sasa mambo yamenyooka, hakuna pedeshee ndama mtoto wa ng'ombe mtaani, masikini na tajiri wote wanapata elimu sawia, dawa hospitalini zipo, wataalam wameobgezwa, vifaa kedekede hadi wagonjwa wa nchi jirani badala ya kwenda kutibiwa India, wanapishana angani kuja kutibiwa Tanzania, halafu anaibuka mtu mwenye fedha chafu alizopata kupitia rushwa anataka urais wa nchi? Pengine urais wa kuja kusomba twiga wetu kwenda ughaibuni, Urais wa kuja kuua tembo wetu pamoja na mchanga wa dhahabu kwenda nje ya nchi.
Nataka niwakumbushe watanzania kwamba, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi. Tutasikia kauli tamu sana zinazokolea masikioni mwetu kutoka kwa wanasiasa mbali mbali wakiwemo wa Chama tawala na upinzani. Hoja yetu kuu tusisikilize maneno matamu, kwa sababu huko nyuma tumeshaongopewa sana kwamba, tutafanyiwa hiki na kile au tutaketewa hiki.
Sisi wananchi tutazame kazi iliyofanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Uongozi wa Jemadari wa vita ya uchumi Dkt. John Pombe Magufuli kwa miaka mitano, kisha tumkabidhi kijiti kwa mara nyingine amalizie pale alipoishia. Tuache kuhamanika na siasa za maji taka kwamba serikali hii imesababisha maisha magumu. Maisha ya nyuma yalikuwa ya kuigiza.
Watu walikuwa hawafanyi kazi, walitegemea kipato cha wizi, kukwepa kodi, biashara ya magendo na uuzaji wa madawa ya kulevya. Vyote hivyo vimezuiwa, nchi imeshika adabu kila mtu anaithamini fedha leo. Rais wa kweli kwa maendeleo ya kweli ni Dkt. John Pombe Magufuli, hao wengine wote ni vibarska wa mabeberu. Kama vile Mbowe anavyowaambia wapinzani wake ndani ya Chama kwamba, Sumu haionjwi kwa ulimi, na mimi niwaeleze watanzania kwamba, utawsla wa nchi kamwe hsufanyiwi majaribio, tukithubutu, tutalia na kusaga meno.
#Majuto_Huja_mwisho_wa_Safari,
#Ningejua_Huja_baada_ya_kukosea,
#Chagua_Ccm_Chagua_Magufuli_kazi_iendelee.