View attachment 364752
Wapiga dili,wauza unga,wachezesha disco,walanguzi,wapiga ramli,wabinafsi,wanyang'anyi,walafi,mafisadi,na wote wanaofanana na hizi characters kamwe hawatafanikiwa kutawala nchi hii kupitia white house labda watafute makazi mengine.
Walioingia kwenye nafasi za umma na wakabahatika kuingia kwenye ofisi hii waliondoka kwa aibu na wengine wataondoka kwa aibu kubwa zaidi ''IKULU NI MAHALI PATAKATIFU''.
Nina heri na amani moyoni kwa Rais Dr.Magufuli kwa kuendelea kufanya usafi wa uhakika ndani na nje ya muhimili wa mti huu mweupe.Kila la kheri na unapoondoka kamwe usiwaachie nchi watu wenye elements nilizorodesha awali hapo juu wapenye tena chonde chonde kiongozi wangu isije kuwa umefanya kazi ya kuwatengenezea ulaji watakaokufuata.
Siyo vizuri hata kidogo kurudia makosa yaleyale walioyofanya waliokutangulia kwenye usimamizi wa nchi na kuacha kwenye mikono salama.Hata kama wakuite kwa majina yote yaliyopo duniani haisaidii ila tu unachofanya ni kwa maslahi wa nchi na kwa dhamira njema bila kumwonea au kumpendelea mtu.KILA LA KHERI MY PRESIDENT.
DIRANQW.