brightfuture
Member
- Jul 30, 2015
- 70
- 14
Visionary leader. Magufuli will follow his footprints.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TatizoNina hakika hawezi kuendelea na mbio hizo ama kasi aliyoanza nayo maana tayari wakubwa waishagundua dhamira take na sasa ile kasi hakuna tena!
kumuumbua baba yako hadharani inataka ujasiriNina hakika hawezi kuendelea na mbio hizo ama kasi aliyoanza nayo maana tayari wakubwa waishagundua dhamira take na sasa ile kasi hakuna tena!
TatizoNina hakika hawezi kuendelea na mbio hizo ama kasi aliyoanza nayo maana tayari wakubwa waishagundua dhamira take na sasa ile kasi hakuna tena!
kumuumbua baba yako hadharani inataka ujasiriNina hakika hawezi kuendelea na mbio hizo ama kasi aliyoanza nayo maana tayari wakubwa waishagundua dhamira take na sasa ile kasi hakuna tena!
Hii inahitaji mwehu yaani mwendawazimu ambayekishajitoa ufahamu na kuamua lolote na liwe lakini watu wangu wapone nabkikombe hiki kiwaepukeTatizo
kumuumbua baba yako hadharani inataka ujasiri
Umenena mkuuNIKITAFAKARI HUWA MACHOZI YANANITOKA:
Tulianza na Mwalimu Nyerere aliyepiga` kwata miaka 24 [1961 – 1985] pale Magogoni – Ikulu; kwanza kama Waziri Mkuu [1961], kisha kama Rais hadi mwisho. Yeye aliyaona maisha ya Ikulu kuwa mzigo; akasema, mtu mwenye hekima na busara atatamani daima kuutua mzigo huo kipindi kinapowadia ili kuwaachia wengine nao wajaribu kuubeba. Alitaka kuutua mwaka 1978 kama isingekuwa kuzuka kwa vita vya Kagera; akaona haikuwa busara kuiacha nchi ghafla katika vuguvugu la vita na baada ya hapo.
Mwalimu alijua, alilinda, alitetea na kuzingatia heshima ya Ikulu ikaheshimiwa. Kuitwa Ikulu enzi zile ilikuwa ni ama kuwajibishwa/kukanywa, kufukuzwa kazi kwa utendaji kazi usioridhisha, au kupongezwa kwa kazi nzuri na kutunukiwa cheo. Zilikuwa enzi za wajibu na kuwajibika. Waovu na wenye kulemewa na mizigo ya “dhambi” hawakukatisha; waliondolewa sawia wasije wakachafua Taifa.
Uteuzi wa viongozi haukuwa kwa njia ya urafiki, upendeleo wala kubahatisha. Vyombo vya dola, hasa Usalama wa Taifa, vilifanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa kuhakikisha kwamba, wale walioteuliwa kushika madaraka walikuwa watu safi, wasio na makandokando. Tukasifika kwa uzalendo, uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu. Na huu ndio msingi wa amani na utulivu tunayojivunia leo; lakini amani hiyo inayoyoma haraka kutokana na “ufisadi” na mafisadi kuachwa kutamba kiasi cha kutaka kuteka mhimili wa uongozi wa nchi.
Chini ya Mwalimu, Ikulu ilikuwa “kisima cha uzima na uhai wa Taifa” kwa sababu yeye mwenyewe alijitoa mhanga kutumikia kwa wema na si kwa maslahi binafsi. Wakati wengine wachache enzi hizo na hata leo, walifikiri Ikulu ni mahali pa kutumbua vinono, starehe na kujizolea mali ; Mwalimu alipaona ni mzigo na tundu la sindano kuweza kupita kufika hapo.
Alisema, “Ikulu ni mahali patakatifu; si pango la wevi na wanyang’anyi”; akatahadharisha kwamba, “mtu yeyote anayelilia kuingia Ikulu kwa udi na uvumba ni wa kuogopwa kama ukoma”, kwa maana atakuwa na lake jambo, na si kwa maslahi ya nchi.Kwa Rais DR.JPM naliona hili na matumaini mapya ya utaifa wetu utarudi soon,ilimradi tu akaze buti kwani watz tumempa dhamana hiyo.Nikitazama picha napata majibu haraka na baadhi ya maswali yangu ambayo mwl,Nyerere aliyafanyia kazi enzi hizo,na wewe tazama vizuri picha hizo unapata ujumbe gani???????????????????.
View attachment 349742
NCHI YANGU TANZANIA:KATIKA HILI LAZIMA TUITETEE NCHI NA WATU WAKE NA SI BIASHARA YA WACHACHE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!RAIS WETU TWENDE TU MUNGU NI ASILI YA MEMA YOTE MABAYA NI YA SHETANI.
Kjn uko vzr kwe kiswahil,,, vijana wachache wanaowez kutumia neno "KONGOLE "Congura....Umenena vema mkuu. Napata picha unafahmu Tanzania imetoka wapi, imepitia wapi, imefika wapi na inaelekea wapi. Historia hii wengi wa kizazi cha leo hawaifahamu kiasi cha kutaka kufanya maamuzi ya hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu. Uzi huu ni moja kati ya nyuzi bora kabisa ambao nimekutanao humu jf. Kongole, mtoa uzi.
Mkuu dhaaa,kwa kweli ni sisi wa kizazi hiki hatusomi maana ni mengi aliyoyasema na kuandika mwl.Nyerere ambayo yalipaswa yatuongoze.Tukiwa na watu aina hii naamini tutalisaidia sana taifa na watu wake.Ikulu ni zaidi ya majengo meupe, yale majengo yaliyojengwa na wazungu hayana maana ikiwa moyo wa yule anayeyatumia kama ofisi yake haujashikamana na wananchi wengi haswa wale masikini.
Ikulu huwa na heshima wakati mwenye mamlaka anapoamua kukiheshimu cheo chake. Mwalimu Nyerere wakati akiwa anajenga hoja aliwahi kutumia mfano wa kwenye biblia akisema huwezi kuwatumika mabwana wawili, yaani Mungu na mali.
Kuna suala la mtu kuweza kukwepa kishawishi cha mali ili utakatifu wa IKulu uweze kuwepo. Huo ni mtihani mgumu sana kwa wanasiasa wengi wa bara letu.
JPM pia anao mtihani huu, maadam ameamua kupambana na wale wenye mali ambao siku zote wanataka kubakia wao tu kama wenye mali hizo, basi wala asilegeze kamba. Vita ndio kwanza imeanza, ili Ikulu iweze kubaki na utakatifu wake.
Ni bora uwe uchi kimwili kuliko kiakili - Julius Nyerere akiongea na UWT pale Karimjee Hall miaka ya 80.Mkuu dhaaa,kwa kweli ni sisi wa kizazi hiki hatusomi maana ni mengi aliyoyasema na kuandika mwl.Nyerere ambayo yalipaswa yatuongoze.Tukiwa na watu aina hii naamini tutalisaidia sana taifa na watu wake.