Julius K. Nyerere: Ikulu ni pahali patakatifu, sio pango la wanyang'anyi

Julius K. Nyerere: Ikulu ni pahali patakatifu, sio pango la wanyang'anyi

Ikulu Ni Ukumbi Kama Kumbi Za Bar, Hazichagui Wageni, Wendawazimu,mateja Wauza Unga,majambazi,wastaarabu Na Wasiostaarabika, USHAHIDI NI HUU, JUZI MSHINDI WA BIG BROTHER ALIKUWA IKULU NA KIKWETE,SHINDANO LA BIG BROTHER LINAENDESHWA KINYUME KABISA NA MAADILI YETU,MFANO KUFANYA NGONO HADHARANI,KUONESHA UCHI HADHARANI,WAUME KWA WAKE KUOGA PAMOJA,LAKIN IDRISA KASHINDA KWA MAMBO HAYO NA KAITWA IKULU KUPONGEZWA, DAIMOND MWENYE KUBADILI WASICHANA KAMA NGUO NA MWENYE KUJIREMBA KAMA MSICHANA NAE KAITWA IKULU. JANA KIONGOZI WA KIDINI MWENYE KUHESHIMIKA DUNIANI KADINALI PENGO ALIKUWA IKULU.Dhamani Ikulu Ilikuwa Ni Viongozi Wa Dini Tena Wa Kitaifa Ndo Pekee Walikanyaga Ikulu,leo Hadi Wavuta Unga Akina Ray C Wamekanyaga Ikulu, JE IKULU BADO NI SEHEMU TAKATIFU KWA MAONI YAKO WEWE???
 
Wasalaam Wanajukwaa Wote! Hili Neno Alilitamka Mwl Nyerere Akiwa Na Maana Kubwa Sana. Neno Mahali Patakatifu Nalifananisha Na Sehemu Za Kuabudia Kama Msikitini, Kanisani Nk. Hii Inamaana Kwamba Atakayeingia Mahali Pale Lazima Awe Msafi Wa Kiroho,kwa Waislam Usifi Ni Lazima Iwe Kiroho Na Kimwili, Awe Anayekataa Maovu, Lakini Haina Maana Waingiao Mahali Patakatifu Si Wote Ni Wasafi Kiroho Wengine Hutubu Dhambi Zao Mle, Wengine Huendeleza Dhambi Zao Mle.Ila Ni Muhimu Kiongozi Wa Mahali Pale Awe Msafi Angalao Kiroho. Kama Mchungaji Sio Msafi Huua Kanisa, Imam Aspokua Msafi Ataua Msikiti, Waumini Watakosa Imani Naye Hivyo Hutafuta Mahali Kwingine Pa Kuabudia. Kwa Hizi Mbio Za Uraisi Kweli Kunaweza Kua Na Padri, Imam Ama Kiongozi Msafi Kuwaongoza Hawa Wanakondoo Zaidi Ya Mil 40? Au Tusubiri Wapate Nafasi Wakatubu Dhambi Zao Mle? Au Ni Kwenda Kutenda Dhambi Mahali Patakaifu?
 
Nashangaa mafisadi nao wanataka urais! Eti Lowassa naye yumo!
 
Ccm wamefanya ikulu kuwa sehemu ya kupiga madili ya madawa ya kulevya
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mtawala na kiongozi. Ili tuendelee, tunahitaji watu (wananchi), ardhi (pamoja na madini, mafuta, gesi, nk), siasa safi na uongozi (na viongozi) bora. Nchi yetu ilibahatika kupata kiongozi bora toka miaka ya 1960 hadi miaka ya 1980 mwanzoni. Baadaye ilipata mtawala bora katikati ya miaka ya 1990 hadi mwishoni mwa mwaka 2005. Toka hapo tumepoteza mwelekeo, yaani hatujui kama tuna mtawala ama kiongozi.

Wakati mwingine najaribu kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu, kwa mfano, inakuwaje Tanzania tuna madini, gesi, ardhi yenye rutuba, mito, maziwa na mbuga pamoja na misitu lakini tumekithiri kwa kutembeza bakuli kwa mataifa masikini ya rasilimali kama Marekani? Napatwa na butwaa miaka ya 2000 hadi 2005 thamani ya shilingi yetu iliweza kuimarika hadi kufikia TSH 1200 kwa USD 1 wakati kwa sasa tumezalisha wasomi wengi na wataalam mbalimbali lakini thamani ya shilingi yetu imeporomoka hadi kufikia TSH 1860 kwa USD 1? Wakati huohuo tunazo rasilimali za kutosha.

Huko tuendako miaka kadhaa ijayo hali itakuwa tete kama mwendo tulionao ndio huu wa kuchagua watu wa kuingia Ikulu wasio viongozi wala watawala. Tujipime na tujitafakari.
 
haya haya manguruwe ndiyo yaliyomtanguliza baba yetu wa taifa ili yaweze kuiba vizr na hizo hotuba wanazisikiliza sana ila hawajali wanaendelea kula tu.

Nawashangaa sana watu wanaompigia chapuo EL, hawajui huyu jamaa na JK ni kama pete na chanda, wanataka wapeane zamu ya kuiibia nchi yetu
 
haya haya manguruwe ndiyo yaliyomtanguliza baba yetu wa taifa ili yaweze kuiba vizr na hizo hotuba wanazisikiliza sana ila hawajali wanaendelea kula tu.

Nawashangaa sana watu wanaompigia chapuo EL, hawajui huyu jamaa na JK ni kama pete na chanda, wanataka wapeane zamu ya kuiibia nchi yetu
 
Back
Top Bottom