Enzi za uhai wake mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake wakati ameishang`atuka aliwahi kusema kuwa Ikulu ni mahali patakatifu,alikuwa anatoa ushauri kwa waliokuwa Ikulu na wanaotaka kwenda Ikulu akihoji kuna biashara gani Ikulu hadi watu wanatumia pesa kutaka kuingia pale .
Kilichinivutia kujadili ni utakatifu wa Ikulu hasa baada ya juzi kusikia katibu mkuu kiongozi Ombeni sefue akitoa msimamo wa Raisi aliyeko IKulu kuwa atachukua hatua baada ya vyombo vya uchunguzi kuchunguza na kuhakikisha makosa ya watuhumiwa kabla ya kutenda.
TAKUKURU imeishafanya uchunguzi,CAG tayari ameishafanya uchunguzi,na ripoti zao zimejadiliwa na Bunge,nikakumbuka katika moja ya maelezo mengi ya sakata la ESCROW katibu mkuu wa rais Mbena alitoa maelekezo ya kwamba hela zitolewe.
Katibu mkuu wa raisi hawezi agiza kutoa pesa nyingi kiasi hicho bila ruhusa ya bosi wake ambaye ni rais,nchi wahisani zimesitisha misaada hususan ya bajeti ya serikali kufuatia sakata hili.familia ya raisi nayo hapa jamvini imetuhumiwa kuhusika na uchotaji wapesa hizi pia.
Tumeona nchini CHINA mafisadi,wala rushwa wakipewa adhabu kali za vifungo hata kunyongwa kwa makosa kama haya,haishangazi kwa rais kusema hivi kwani anawezaje kumkamata katibu wake kwa kuagiza kutoa maagizo ya kutolewa pesa hizo!
Toka tupate uhuru nchi yetu imeongozwa na maraisi wote kutoka CCM Je ni yupi ambaye anaweza akasimama na kutangaza kwamba mimi niko safi kiasi cha kumkosoa rais aliyeko madarakani pindi akikosea??Ni nani? Walau Nyerere alifanya makosa lakini dhamira yake haikuwa hata mara moja kufisidi,kuiba na kutumia Ikulu kwa manufaa binafsi.Ndiyo maana alikuwa hata na jeuri ya kukemea na kutoa ushauri katika matukio yoyote muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu.
Baada ya yeye nani anaweza akasimama kukemea makosa lukuki yanayofanywa na uongozi wa nchi hii,hakuna kwa sababu hawana usafi huo.
Mwinyi? na azimio lake la Zanzibar? Au Mkapa na ANBEN na mgodi wa Kiwira,Kuuzwa kwa kutupwa kwa NBC?tena kuna mambo mengi labda uandike kitabu, Je huyu aliyekuwepo Ikulu sasa hivi,ni kashfa juu ya kashfa,kwa hawa anaotangaza kila siku kuwa wanamuenzi Nyerere mbona wamekengeuka busara zake?
Sasa hivi wanajipanga CCM kuendelea kuingia Ikulu, kuna mtuhumiwa wa Richmond lakini tukumbuke kuwa Nyerere aliwahi kusema kuwa Mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa,huyu ametuhumiwa akajiuzulu basi atuambie nani ni mhusika halisi wa kashfa hii kama si yeye. kuna yule mtetezi MEREMETA ambaye kila mwenye akili anajua kuwa ni wizi lakini yeye alisema hata afanywaje hatosema,kuna yule aliyeteka rasimu maridhawa ya katiba kama ilivyotayarishwa na tume ya raisi iliyoongozwa na jaji Warioba akapitisha rasimu ya kuwatetea wezi ikiandikwa na mtuhumiwa wa pesa za rada,au yule aliyetete kwa nguvu baada ya kuwekwa hadharani mpango wa serikali ya CCM na biashara ya PEMBE za ndovu na rafiki zao wachina ,sijui kwa ahadi ya kujengewa bandari Bagamoyo? jamani IKULU NI MAHALI PATAKATIFU!
CCM wamepageuza IKULU kutoka kuwa mahali patakatifu hadi kuwa PANGO LA WANYANG`ANYI,sehemu ya kupigia dili za kuiba.
Hili nalo watahakikisha linapita pia, mbona mengi yamepita,sakata la jairo ingekuwa China kanyongwa,Seth mwizi wa fedha za watanzania anatamba hana wasi wasi kwa sababu anajua kuwa Kuna pango lao la wanyang`anyi liko Ikulu washirika wake katoka maovu.
Na jinsi watanzania tulivyokuwa tumerogwa tutalipigia jambazi lingine liingie Ikulu la CCM natamani kuhamia mwezini