Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Kama wale waliouza chama chetu kwa mtu waliyetuambia kuwa ni fisadi papa, matokeo yake sasa wanatuulia chama chetu. Mungu anawaona.
 
Hahahaha babuuuuu.
Apumzike kwa amani huko uliko.
Natamani ningekuwa na uwezo wa kumrudisha lakini sina!
MBAYA UNAKUTA MH MMOJA WAZAZI AMETANGULIA HUJAWAHI SINGLE DAY KUMRUDISHA UMRUDISHE MZEE WA WATU LOH..ANZA WALIOTUTOKA KWANZA UPANDE HUOO
 
Hilo neno Malaya Mwalimu sijui ame lisema mara ngapi ,inaelekea alichukia kweli kweli
Kuna watu walikuwa wamemtibua sana na alikuwa akiwapelekea Ujumbe sijui ni akina Kambona nilikuwa sijazaliwa!Raha ya milele umpe Mwl. Nyerere eeh bwana........
 
Mwalimu iliiona kesho jana.

Aliiona Tanzania chini ya udikteta kutokana na Katiba mbaya. Aliwaona wanasiasa malaya wakati wa kipindi cha udikteta.

Wakati wa udikteta, Mwalimu aliwaona vijana waoga badala ya vijana jeuri, vijana wanaohoji.

Wakati wa udikteta, alikiona chama legelege, chama ambacho kiongozi wake anakuwa na nguvu kuliko chama. Chama kinachoshindwa kutoa mwongozo kwa watawala.

Mwalimu tunajua wewe ni mwanadamu, na yawezekana kuna sehemu wakati wa kuishi kwako ulimkosea Mungu au wanafamu wenzako, lakini tunakuamini sana katika dhamira yako kwa watanzania, dhamira ambayo haikuwa na hila, dhamira ambayo haikuwa na unafiki.

Baba yetu wa Mbinguni, kwa kuangalia dhanira yake njema, umjalie taji katika ufalme wako, nao waishio leo kwa tamaa ya madaraka hata kufikia kuiba kura, wenye kuwadhalilisha wenzi wao kwa nia ya kujikweza, wenye kujitangaza sana kufanya mema kwaajili ya kuutaka utukufu, wenye kutaka kuua au wale wauao kwa sababu hawataki maovu yao kutajwa, basi uwapatilize wao na vizazi vyao hadi watakapokurudia na kutambua kuwa wewe ni Bwana wa Haki na una mamlaka juu ya wale wakutiiao na wale wenye kulitaja jina lako kwa hadaa.


Ubarikiwe sana Mkuu.
 
Kweli hayati nyerere ni baba Wa taifa!
Angekua hai sipati jinsi ambavyo angeshudia sio Malaya sasa Bali nimakahaba wa kisiasa walikubuhu ndani ya Chadema, na angeshudia pia mnunuzi mkuu makahaba hawa ni mwenyekiti Wa CCM na ndo rais Wa nchi, sasa sijui ni rais anayetengeneza taifa LA Malaya na makahaba!? Sipat picha
 
Kosa lake kubwa kabisa ni kutuachia katiba mbovu sana tena kwa maksudi kabisa!!
Kwa hilo ninauhakika anajilaumu sana huko aliko.
Alihofia kufuta historian yake akiwa hai maana angejaribu kuleta katiba mpya

Muungano fyekaa
Ujamaa fyekelea mbali
 
Hivi Mzee unamfahamu vizuri Mmakonde au unamsikia ?
Jinsi Mwalimu alivyokuwa, ilikuwa siyo kawaida kuona kitu kibaya kinafanyika halafu yeye anyamaze kimya tu na kukiacha kipite. Hakuwahi kuwa mtu wa hivyo hata siku moja na angeziona kampeni za mwaka 2000 nadhani Mmakonde angeisoma nambaa: Sema bahati mbaya Mzee wetu hakufika.
sio kwamba hawakumfikisha.?
 
Back
Top Bottom