Juma Abdul Mnyamani umecheza mpira muda mrefu lakini hujui kuuchambua,Azam TV mtoeni huyo mtu

Juma Abdul Mnyamani umecheza mpira muda mrefu lakini hujui kuuchambua,Azam TV mtoeni huyo mtu

Kuna tatizo kubwa kwa wachezaji wetu wa kibongo unapowatoa kwenye pitch ukiwaleta kwenye ulimwengu mwingine msikilize Che Malone akiwa anauongelea mpira kisha msikilize Tshabalala ambaye ndo kaptain wetu utagundua tofauti na ndo maana wengi hawana mvuto nje ya uwanja, hii huenda ikachangiwa na.

1.wachezaj wetu kukosa exposure mfano ametokea kakakuona fc ya mbagala ghafla kaibukia Simba na kamalizia soka hapo
2. Elimu ya kawaida (hata lugha wengi huwa ni tatizo sana)
3.Elimu na malezi ya kisasa ya kisoka
 
Hata hao akina Kiemba walianza hivyo hivyo ila wakatendea haki huo mwaliko mpaka wakawa wachambuzi
Sasa mbaalikaje mtu hajui kujieleza
Wewe utakua ni Mmawia kutoka Msumbiji manake kiswahili kinakugonga ugoko kweli kweli..
 
Sio kila aliyewahi kucheza mpira anafaa kuwa kocha

Si kila aliyewahi kucheza mpira anafaa kuwa mchambuzi

Amri Kiemba na Ally Mayai mko vizuri,ila kwaJumaAbdul Mnyamani nasema No,anashindwa hata na akina

Samwel, Jeff Lea ambao hawajui kupiga hata danadana mbili
Hata Kiemba alianza kwa makosa akajifunza na kuwa hivi unavyomuona leo, tumpe muda.
 
Juma abdul sio mchambuzi wa mpira wa kulipwa,yeye amesomea taaluma ya uchambuzi,kwa kuthamini taaluma yake ya uchambuzi azam tv huwa wanamualiki ktk baadhi ya mechi kuendeleza taaluma yake,yani hapo huwa kama yupo field. Ni mchambuzi mzuri,mahiri na anajua vema histry! Sema uzoefu ataupata mdogo mdg. Tazamio letu ni kuwa atakuwa mchambuzi mkubwa kuzidi hao akina mayai na wenzake. Ndo mana hata azam tv humtambulisha kama "JUMA ABDUL MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA 2012-2020" na sio "JUMA ABDUL MCHAMBUZI AZAM TV"
 
Kucheza, kuchambua na hata kuufundisha ni taaluma tofauti hizoo.
nilikuwa namsikiliza kaseja akichambua game ya Simba na Constantine aise yule jamaa hata kujieleza itakuwa tabu kiujumla uchambuzi na kucheza mpira ni viwili tofauti ,big up kwa Amri kiemba
 
Back
Top Bottom