Walimuita akakataa wakaachana nae akaenda kusema alivyodharauliwa. Hakuna sehemu Wasafi wameenda lalamika kuhusu kukosekana kwake.
Why walimuita? Sababu ni msanii.
Walikuwa wanamuonea huruma? Sivyo, waliitaka appearance yake kwenye event na wamlipe. Value yake wakaona ni 500k na akaona haifai.
Why unalazimisha awepo kisa aliitwa mwanzoni? Wamlete mtu kisa heshima wakati value ya anachokitoa wanaona ni ndogo kuliko price yake?
Brands kubwa Tanzania kama Tigo, Vodacom, TBL, Serengeti, CRDB, NMB, Cocacola wakiwa wanatoa deals za wasanii umeona wanawatafuta kina Mr. Nice, Johari, Wema Sepetu, Chidi Benz kwa heshima kisa walikuwa maarufu zamani?
Mtazamo wa kibiashara na kunyanyua mikono juu ni vitu viwili tofauti kabisa.