Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Bro Huo ujinga wa watu unadhani umezalishwaje au umetokeaje au umekujaje? Maana hakuna unga tuliolishwa au malaika aliyeshushwa kuleta ujinga Tanzania.

I'm sorry to disappoint you kwamba jamii ya kitanzania always imekuwa ya wajinga wengi kuliko werevu. Tena Bora sikuhizi idadi ya werevu kidogo imeongezeka kuliko zamani.

Tofauti tu ni kuwa, baada ya kuwa na hizi social medias, Power ya kutengeneza trend imeondolewa kwa wenye media au watu maarufu na imepelekwa kwa watu wote mtandaoni (ndo tunapata watubaki wanatrend kama mzee wa 900 itapendeza,Pierre liquid,Nabii Tito,Harmorapa,RC wa Tabora,Mwijaku, babalevo Nk.)

Hivo imekuwa Rahisi kwa wajinga kusapoti ujinga wao kuliko zamani. Na Kwasababu wajinga Tanzania ni wengi ndio maana ujinga unatrend.

Na wasanii Kwasababu wanataka kutrend wanafanya vitu ambavyo jamii inataka.

Social media zimetengeneza mazingira ya echo chambers kwa watumiaji kuflock kama nyumbu kwa vitu wanavyovipenda.
Sasa Kwasababu watumiaji tayari waanaenda kama nyumbu, ni ngumu kwa msanii kuwapa kitu tofauti na walichokizoea wakakifuata.
Tofauti na zamani ambapo msanii ndo alikuwa ana power ya kufanya chochote na kutengeneza trend na yeye ndo anaweza kudirect upepo uelekee wapi maana jamii ilikuwa Haina alternative.

Ndomaana sikuhizi hata diversity ya mziki inapungua kwa Kasi, wasanii wote wanakuwa na ladha ileile kama ikitrend amapiano Kila mtu anaimba amapiano, sio kama zamani Kila msanii alikuwa na style yake unique.
Ujinga umepata nafasi kwasababu modern generation inapenda vitu rahisi haipendi kushirikisha ubongo.

Kitu kingine ni namna ambavyo sex imepewa mileage.

Kuna msemo unaitwa "Sex sells"

Hii inamaanisha audience inapenda kusikia, kuhisi, kuona na kuonja kila kitu kinachohusu sex.

Sex becomes bait for catching fans
 
Wasani wa sahv wao wanakuambia rushamikono juu
Say yeah yeahw3ka mkono juu
Upuz mtupu
Mara sjui honeyy honeyyy inama nkuweke kunywa bia sijui
[emoji1]

Ova
Kuna mwanangu anaitwa Nala aliwahi kuchana

Alisema

Kwanza huyu msanii amekuja amelewa, halafu hajasema samahani kwa kuchelewa.../

Show imeanza saa sita ye amefika saa nane, kila mtu amekunja ndita anatamani amtukane.../

Amemuambia Dj ashike si tupige kelele, wakati ye mwenyewe anapiga makelele.../

Makelele mchezaji au makelele chuo?, kama kawaida yenu show imejaa mizinguo.../

Amevua shati inaonekana ana usongo, hizi Gym za ukubwani zina waharibu ubongo.../

Tunataka show ye anaonesha mwili, na muda unazidi kwenda inakaribia alfajiri..../

Ni nyooshe mikono juu vipi wakinisachi simu, acha ujinga wako we msanii una wazimu.../

Tutakupiga wakubebe na machela, usilete utani hii show tumelipa hela.../
 
Nawaelewa wana jukwaa.

Sawa mnataka alipwe shilingi ngapi, maana wengine mmeanza zile afrikan kalakta zenu!.
Ishu sio alipwe shilingi ngapi, ishu ni kua ameikataa laki tano sababu kaona haina thamani kwake.... kama angeona inamtosha basi angeshiriki kiroho safi, shida imekuja chawa wa Mondi wanamind kwanini ameikataa wakati yeye ni wa zamani, wanaona kama Mondi amemsaidia ila jamaa hasaidiki wakati Kiroboto anajijua amesimama wapi.
 
Nadhani Kuna wasanii wawili tu naweza kusema walipitia mkono wa chuma wa clouds na bado wakatoboa 1. Jay Dee 2. Sugu. Ni hawa tu wawili japo kwa sasa wakati umeshawatupa mkono ila Diamond hapana mitandao ya kijamii imemsaidia.
True mkuu, inabidi umuangalie mtu kama Jide alivyopambana bila mitandao ndio utajua ugumu wa kuzishinda media tena kama zote zikiungana
 
Wakati Diamond anagombana na clouds sidhani kama alikuwa kafikia mafanikio aliyokuwa nayo lady jay dee..

Hivi hao waliopita mnadhani hawakuwa na fanbase, okey utasema Diamond alikuwa top artist, vipi kuhusu mb dog aliyekuwa anasimamisha kijiji East Africa yote bila skendo wala mitandao ???...

Mtu anaesema mitandao haisaidii angeanza kuangalia kwa nini Diamond kahakikisha familia yake ina online brand kubwa na pia watu kama juma lokole kwa nini kawaweka karibu. Leo hii Diamond anatoa wimbo, kesho watu wakubwa wamepost, bodaboda zote zinapita na hizo nyimbo etc

Mkuu Ogopa taasisi kama clouds ilivyokuwa inacontrol music supply, sidhani kama Diamond ni exptional talent kuzidi wote walioangushwa Ila muda ulimshika mkono na pia akawa agressive kibiashara. Ndo maana kabaki hapo
 
Legend kama yeye anapewaje laki tano, kweli dharau aisee.
Kimuziki, Juma nature ana thamani zaidi ya laki tano ila kibiashara ya muziki sioni akizidi laki tano.

Ni vyema tukatofautisha, kati ya Nature na hadhi ya yake ya ukongwe na uwezo wake wa kale dhidi ya hitaji la biashara ya muziki wa Sasa.
 
Hawa jamaa wanazungumzia ushabiki kwenye masuala ya hela na uwekezaji wa watu.
Kwanza Wasafi Festival inahudhuriwa na vijana under 30 wengi kuliko watu wazima, sasa tiketi zitauza kwa nani kati ya Nature na let's say Jux?

Mtu anakwambia eti Juma alivyotoa album ya Ugali alikuwa sijui sekondari, mtu huyohuyo Wasafi Festival haina maudhui yake haendi ila anataka Juma Nature alipwe "kwa heshima". Na mtu huyo wala hashabikii msanii ambaye alivuma akiwa anatambaa, ila anataka rika la hiyo Festival lishabikie msanii aliyevuma kipindi halijaanza shule. Huwezi pata mauzo kwa kutumia hizi nadharia.

Suala la malipo honestly Nature kapewa dau dogo, sasa kakataa labda kwenye negotiations akataka dau ambalo waandaaji wameona hana thamani hiyo kwenye audience yao au yawezekana kakataa bid bila kutoa ofa yake. Hii show sio Hall of Fame kwamba unakuja kwa huruma ya fans wako na tunakuita kwa heshima, this is business.

Maudhui ya hii festival hayaendani na hadhi ya kina Juma Nature. Kuna show ya old school inabidi iandaliwe mahsusi na iwaunganishe legends wote hao. Msuguano utakaotokea kwenye maandalizi sio wa kitoto, humo kwenye legends kuna walevi kibao, watu pumzi imekata muda hawakumbuki last time wamepanda stejini lini, wahuni wasiozingatia makubaliano wapo wa kutosha na tabu nyinginezo. Na hapo ubahatishe hawa keyboard fans wenye majukumu mengi kwa sasa wanaodai watahudhuria. Waandaaji wanazingatia vitu vingi wanakacha event kama hiyo.
Point zako zote zipo valid Ila kama wanaona kibiashara haipo vizuri walimfuata wa nini ??.....
 
Shida yako wewe unaleta u'team wa Dai na Nature....

Mambo ya nimejuaje hayo najua mimi....Na ndiyo maana nikaandika...ili mtu kama wewe usiyeelewa, uelewe,usipotaka unaacha

Narudi Bongo Flavour Honours ya Sugu wanalipwa vizuri....

Kumlipa mtu laki 5 kwa Show anazofanya Nature ni upuuzi kama upuuzi mwingine..Awalipe hao waimba Amapiano wenzake hiyo hela...
Hiyo bongo fleva honour yenyewe inadhaminiwa na Wasafi
 
Ishu sio alipwe shilingi ngapi, ishu ni kua ameikataa laki tano sababu kaona haina thamani kwake.... kama angeona inamtosha basi angeshiriki kiroho safi, shida imekuja chawa wa Mondi wanamind kwanini ameikataa wakati yeye ni wa zamani, wanaona kama Mondi amemsaidia ila jamaa hasaidiki wakati Kiroboto anajijua amesimama wapi.
Kama ameikataa kulikuwa na umuhimu gani wakapiga kelele
 
Back
Top Bottom