Usupa staa unakuwa na sehemu yake ambayo huko ndio una play role yake.
Unajua kwasababu gani hao wenye vipaji hawasikiki?
Ni kwasababu ya jamii imeshiba sana ujinga (Dizasta Said)
Tukiwa na jamii ambayo ina vijana conscious hao kina Mwijaku hawezi kupewa air time ya kuongelewa kwasababu ataonekana mpuuzi machoni mwa watu.
Na kwanzia hapo kila mtu atajua namna pekee ya kukubalika ni kufanya kitu kwa weledi kuzingatia ubora kwasababu ndio soko linavyotaka
Kushiba ujinga unaweza kuzilaumu social medias.
Zamani hakukuwa na sources nyingi za burudani na ilikuwa ngumu kwa mtu kuburudika, mpaka asubirie saa 2 mizengwe au ze comedy au asubirie ngoma mpya ya professa J aisikilize kwenye kimemory chake na kiredio kwa mwezi mzima mpaka akariri mashairi yote. Ndomaana ilibidi wasanii wa zamani wawe very talented maana walikuwa wanategenewa kwa burudani na jamii ilikuwa inawasikiliza kwa mda mrefu. Msanii anaweza kutoa ngoma moja akatrend mwaka mzima au hata miwili.
Sikuhizi mtu akitaka kucheka au kuburudika ni bundle lake tu , akiingia Whatsapp status atakuta contacts zake wanamchekesha kwa vimeme kibao, akienda TikTok ni swala la kuscroll tu anapata burudani mpya Kila sekunde, akienda Instagram ndo usiseme, akiingia youtube atascroll mpaka achoke, Yani kumekuwa na abundance au oversupply ya entertainment ambayo inasababisha dopamine kwenye ubongo kuzalishwa kwa wingi mpaka kuleta uteja.
Hii imesababisha Attention span ya vijana kupungua. Ndomaana wasanii wa sikuhizi wanatoa ngoma Kila mwezi na Bado hawapati attention kama wasanii wa zamani. Mtu akishaisikiliza mara 2 basi anaenda TikTok kucheki mishe zingine.
Kama mlevi wa porno alivyo, kwakuwa ana uwezo wa kuscroll akaona wanawake hata 100 kwa lisaa limoja (Na anazoea kufanya Hivyo) inamsababishia kupungua uwezo wa kuburudika na mwanamke mmoja. Hata akiwa naye kitandani akipiga bao moja Chali maana attention kwake ishapotea.
Ndivo ilivo kwa kizazi Cha Sasa kuhusu burudani. ili utrend haitoshi kuwa na talent au kuongea vitu vya maana kama Dizasta. Inatakiwa uwe na Shock Value itakayomfanya mtu apay attention kwako. Sio unatoa ngoma ambayo mtu atatakiwa aisikilize mara 7 ndo aielewe.
Ndomaana wasanii wamechuja vipaji vyao na kuanza kuimba ujinga ambao una shock Value ya kumvuta mtu ndani ya sekunde kadhaa. Ndio maana kina Roma Bado wako relevant maana Wana Ile shock Value ya siasa. Ingawa kimziki anazidiwa na kina Fidq, Nikki mbishi au Dizasta
Hiyo ndo sababu kwann hata huku Jf Uzi za kijinga MUM zinatrend kuliko za JF intelligence. Kwasababu ya hiyo shock Value ya ujinga kama "Nimemfumania Mke wangu kwenye threesome na wazazi wangu"