Hizi nchi maskini ni tabu kwa kwenda mbele, najaribu tu kuwaza catalogue ya Sir Nature, kuanzia nyimbo zake, nyimbo za kundi mpka zile za kushirikishwa!
Kwa nchi kama US ilibidi awe anakula tu maokoto ya digital platforms na angekuwa tajiri bila hata hizo shows.
Sasa kwa mfano ukienda spotify nyimbo zake hata 10 hazifiki, na sina hakika kama acc ni yake kweli.
Hapa kwetu hata museum ya tu ya kumbukumbu ya Bongo fleva ilikotoka hakuna, hizi nyimbo unakuta hata wasanii wenyewe hawana, kwahiyo dharau za kulipana laki 5 lazima ziwepo.
Ifike muda tuupe thamani muziki wetu, Sugu ameonesha njia na Bongo Flava Honors japo katuwekea stage ya hovyo sana hata stage ya bar ina afadhali.
Hata tukiamua kutenga mji mmoja uwe ndo kitovu cha Bongo Fleva inawezekana, Leo hii ukienda Nashville, Tennessee kuna kumbukumbu zote za muziki wa country, producers, song writers na record label za Country zipo Nashville na wameupa heshima kubwa muziki wao.