Hawa jamaa wanazungumzia ushabiki kwenye masuala ya hela na uwekezaji wa watu.
Kwanza Wasafi Festival inahudhuriwa na vijana under 30 wengi kuliko watu wazima, sasa tiketi zitauza kwa nani kati ya Nature na let's say Jux?
Mtu anakwambia eti Juma alivyotoa album ya Ugali alikuwa sijui sekondari, mtu huyohuyo Wasafi Festival haina maudhui yake haendi ila anataka Juma Nature alipwe "kwa heshima". Na mtu huyo wala hashabikii msanii ambaye alivuma akiwa anatambaa, ila anataka rika la hiyo Festival lishabikie msanii aliyevuma kipindi halijaanza shule. Huwezi pata mauzo kwa kutumia hizi nadharia.
Suala la malipo honestly Nature kapewa dau dogo, sasa kakataa labda kwenye negotiations akataka dau ambalo waandaaji wameona hana thamani hiyo kwenye audience yao au yawezekana kakataa bid bila kutoa ofa yake. Hii show sio Hall of Fame kwamba unakuja kwa huruma ya fans wako na tunakuita kwa heshima, this is business.
Maudhui ya hii festival hayaendani na hadhi ya kina Juma Nature. Kuna show ya old school inabidi iandaliwe mahsusi na iwaunganishe legends wote hao. Msuguano utakaotokea kwenye maandalizi sio wa kitoto, humo kwenye legends kuna walevi kibao, watu pumzi imekata muda hawakumbuki last time wamepanda stejini lini, wahuni wasiozingatia makubaliano wapo wa kutosha na tabu nyinginezo. Na hapo ubahatishe hawa keyboard fans wenye majukumu mengi kwa sasa wanaodai watahudhuria. Waandaaji wanazingatia vitu vingi wanakacha event kama hiyo.