Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Nature angekubali tu hiyo maana hata kama ana audience ni wale fungulia dogi yaani timua vumbi afu kingine hio 500k wamempendelea ni kama hisani tu diamond aachane na hawa watu wa hivi wasio na shukrani
Diamond anamjua Nature vizuri. Nature mtoto wa kihuni toka Temeke kwahio masela lazma wawe shazi. Muziki wake unaakisi maisha halisi huwezi kufananisha na miziki ya Big G ya akina Mondi.
 
Washamba wengi humu hawamjui Nature, wala sio utoto ni vile kipindi hicho wao walikua sigimbi wanalima magimbi,

Vyuo ndio vimewaleta wengi jijini, basi wanajikuuuuta na wao wamo, ndio utaona michango mingi ya walugaluga wanaona kiroboto anastahili hiyo laki 5.
Basi unajikuta mjaaanja.

Kumbe FALA tu.
 
Jukwaani watu hugewa muda.

Mfano dk 20 au 15 kila mmoja.

This means angeifanya kazi labda ya dk 30 kwa kulipwa laki tano.

Sasa tatizo ni kwamba Nature anaamini kwa huo muda yeye anatakiwa labda kulipwa milioni 5 kwakuwa hiyo siku anayogoma kwenda alitengeneza hicho kiasi kwa dakika hizo hizo.

Hichi kiasi ndicho Clouds walikuwa wanalipa wasanii wote wanaokuja kwenye show spesho kwa eneo husika tu na siyo wanaozunguka na show Tz nzima.

Nature ni legend yeah lakini umewahi sikia "If it doesnt make money, it doesnt make sense"?


Kuna watu wana principles zao beyond pesa, anaweza kuona ana thaman kubwa zaidi na ni haki yako. Do not challenge him maana humlishi
 
Yaani jf siku hizi hovyo kabisa Unaweza ukaumiza kichwa kumbe unabishana na kitoto cha 2006 kinamtetea rolemodel wake chinomanawan 😅😅😅😅
Hela anayoingiza Chino anaweza kukununulia zigo la chupi kiasi usiwe unafua chupi... Wewe ni kuvaa na kutupa kwenye 🗑️ maisha yako yote.
 
Nature hana njaa na wala dhiki amechagua kuishi maisha ya nje ya umaarufu, kipesa yupo vyema alishajipata muda sana. Ndiyo maana kila ikitajwa orodha ya wanamuziki wenye utajiri, kumi bora hakosekani na hapo hayupo active. Hiyo pesa ni dharau kwake, yaani akache miradi yake uende kumlipa kiasi hicho.

Mtu kuamua kuishi maisha yaleyale aliyokulia hata baada ya kufanikiwa, haimaanishi ni ana dhiki. Ile ndiyo staili yake hata alipokuwa akishika chat zote aliishi vilevile alivyo hivi sasa. Hawezi kukubali umpe hela anayoitoa kwenye mfuko wake wa shati.

Hiyo show mnasema analipiwa usafiri, chakula na malazi. Hayo mambo hawafanyi wasafi mpaka mseme wanataka kurudisha, wanafanya wadhamini wa show ile
 
Issue sio pesa Ila heshima na kwenye issue za mjini, ukishakubali 500k , ndio inakuwa gharama yako ya show kwa kila mtu atakaekufuata..
Kwa upande wangu nature yupo sawa kabisa
Nature alishakuwa na heshima kitambo... Pesa haimuongezei chochote.
Kukataa shoo hiyo kaonesha kutokukomaa ktk tasnia.

Nature kwa Sasa ni mtu wa kutoa misaada...shoo za hisani kusaidia masikini.
 
Back
Top Bottom