Sioni nafasi ya kupeleka lawama kwa social media kwenye tatizo lililotengenezwa kupitia ujinga wa watu.
Zamani hakukuwa na sources za burudani
Katika tafsiri yako ya hizo sources za burudani una maanisha ni lazima hizo burudani ziwe za kijinga jinga?
Ukisema ili u trend ni lazima ufanye kitu cha hovyo basi ni kweli upo kwenye jamii ambayo imeshiba sana ujinga.
Bro Huo ujinga wa watu unadhani umezalishwaje au umetokeaje au umekujaje? Maana hakuna unga tuliolishwa au malaika aliyeshushwa kuleta ujinga Tanzania.
I'm sorry to disappoint you kwamba jamii ya kitanzania always imekuwa ya wajinga wengi kuliko werevu. Tena Bora sikuhizi idadi ya werevu kidogo imeongezeka kuliko zamani.
Tofauti tu ni kuwa, baada ya kuwa na hizi social medias, Power ya kutengeneza trend imeondolewa kwa wenye media au watu maarufu na imepelekwa kwa watu wote mtandaoni (ndo tunapata watubaki wanatrend kama mzee wa 900 itapendeza,Pierre liquid,Nabii Tito,Harmorapa,RC wa Tabora,Mwijaku, babalevo Nk.)
Hivo imekuwa Rahisi kwa wajinga kusapoti ujinga wao kuliko zamani. Na Kwasababu wajinga Tanzania ni wengi ndio maana ujinga unatrend.
Na wasanii Kwasababu wanataka kutrend wanafanya vitu ambavyo jamii inataka.
Social media zimetengeneza mazingira ya echo chambers kwa watumiaji kuflock kama nyumbu kwa vitu wanavyovipenda.
Sasa Kwasababu watumiaji tayari waanaenda kama nyumbu, ni ngumu kwa msanii kuwapa kitu tofauti na walichokizoea wakakifuata.
Tofauti na zamani ambapo msanii ndo alikuwa ana power ya kufanya chochote na kutengeneza trend na yeye ndo anaweza kudirect upepo uelekee wapi maana jamii ilikuwa Haina alternative.
Ndomaana sikuhizi hata diversity ya mziki inapungua kwa Kasi, wasanii wote wanakuwa na ladha ileile kama ikitrend amapiano Kila mtu anaimba amapiano, sio kama zamani Kila msanii alikuwa na style yake unique.