Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Shida yeye ni legend na ana wapenzi wengi wa nyimbo zake kwa hio ni kivutio cha show mwingine anaenda kwenye show kumuona Nature tu akiperfom alafu basi akishuka na yeye anaondoka au hujui?
Angesema hatokuwepo kwenye show inatosha mbona diamond kuna show anakataa kufanya na hajawahi kusema amelipwa kiasi fulani Ndio Maana hajafanya, alichofanya nature ni utoto makubaliano yoyote yanabaki kuwa wewe na unayekubaliana nae kukubali au kukataa ni sehemu ya makubaliano sio ugomvi
 
Hadhi muhimu sana.

Ya mia iuzwe mia na ua buku iuzwe buku
 
Laki 5? Nivuje jasho legend laki 5 wewe unaingiza MAMILIONI
 
Billnas ana jina kubwa kuliko nature kwasasa labda ungeniambia nature wa zamani Ndio Maana Wasafi wamemvalue kwa hiyo hela
 
Hawamjui nature hawa Leo hii kwenye show nature anafunika balaa ...ana balaa kiroboto
Ana magoma ambayo yana vibe yani sio rahisi kwa mtu aliyezaliwa miaka ya 2000 kuweza kumuelewa.

Halafu wengi wanaompinga Nature kwa kigezo cha hana nyimbo mpya ambayo ipo kwenye rotation, wengi wanaonesha hata hawajawahi kuhudhuria kwenye show.

Itakuwa ndio type ya wale watu amabo kwenye show wanazoenda ni zile ambazo CCM kwenye kampeni zake ilikuwa inawabeba wasanii.

So baadhi ya watu wakaona yes this is perfect angle to enjoy the show.

Nature kikawaida usimruhusu aanze kwenye show utafanya watu waanze kuwaona wasanii wanaofata wanafanya futuhi.

Nature muweke mwishoni ukimuanzisha utapata lawama kwa wasanii kwanini umewadhalilisha
 
Kwa wasiomjua nature aliimba hizi ngoma

Hakuna kulala
Mgambo
Kila siku za wiki
Kisa Demu
Inaniuma Sana
Sitaki Demu
Mtoto Iddi
Mzee wa busara....

Dah Kwa hizi ngoma hata Mimi ningekataa laki tano... Tatizo watoto wa DP WORLD hawawezi nielewa [emoji26][emoji16]
 
Humjui nature dogo weka shoo nature na msanii wa sasa yoyote nakuhakikishia nature atakuumbua brother muache tu

Cc: reymage
Hahahaaaa...ulionaaa...hawamjui nature ,hawamjui Hata kidogo Mimi bwana enzi za usichana fiesta nilikua nikienda nacheza mpk Asubuhi nyimbo zote naimba Sasa hv niwekee 100m niimbe nyimbo moja ya msanii yoyote mpya siijui
 
Ndiyo, ni kweli wasanii wa zamani Wana vibe kwenye stage. Lakini mashabiki hawajui Hilo. Mashabiki huwa wanafuata wasanii wanaotrend.
Wakishanunua tiketi na kuingia ndo mambo ya kuvibe nyimbo za zamani yanakuja baadae.

Ukisema best naso afanye show yake Furahisha na Mario afanyie yake kirumba, watu watajaa kwa Mario ingawa hao watatu watakaoenda kwa best naso watavibe kuliko maelfu walioenda kwa Mario..

Wanaoandaa matamasha hawakulipi msanii kwa uwezo wako wa kuliamsha kwenye stage, wanakulipa kwa uwezo wako wa kuuza tiketi.

Business is business.
 
Na shoo zote nature anakua mwishoni au WA pili kutoka mwisho ana balaa yule Mzee..Mimi nshaenda sana fiesta !!nature anakuumbua na wasanii wako ana uwezo WA kuimba bila kuchoka mda mrefu kaahh...sijaona Mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…