Juma Nature: Nyota kubwa inayoelekea kuzimika

bluetooth23

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Posts
348
Reaction score
326
Daaah. Nakumbuka jamaa akipita mtaa wa Kongo watu walikuwa wanaacha biashara zao na kufunga mtaa, nakumbuka matamasha ya wazi pale mnazi mmoja, Coco Beach na Biafra Kinondoni yani alikuwa tatizo Juma Nature, mikoani ndio usiseme. Aliwahi kuonekana mkoani Kigoma yani wafanya biashara waliacha maduka kwenda kuangalia gari la matangazo alilokuwa amepanda Juma Nature.

Nakumbuka interviews alizokuwa akifanya Star TV, EATV na kwingineko, viewerz walikuwa wengi wakickia kipindi flani atakuwepo Juma Nature. Nakumbuka mkutano wa CCM Dodoma, watu waliacha kupanga foleni kumpungia mkono Kikwete na badala yake mamia kwa mamia walienda kusukuma gari alilokuwemo Juma Nature.

Jamaa now imebak historia.
 
Kila zama na kitabu chake aisee. Fursa kubwa katika maisha haziji mara mbili.
 
Sio imebaki stori waliopo sasa ni wakali kuliko kuna wimbo katoa na lady Jay Dee juzi kati mbayaa so ajipange tena sana.
 
Sijui wasanii wakubwa style zao zinapitwa na mda au wanazoeleka,maana utashangaa madogo wapya wanafunika mbovu
 
Co kuzoeleka hawalong tym mc's wanafel kusoma alama za nyakat
 
kitu cha kufaham ni kuwa huwezi kuwa juu milele, hakuna cha ajabu Kwa hilo,mfano Mariah Carey bado anahit mpaka leo?au kujaza ma concert the way she did back in the days.?jbu ni noo., kitu tunachoweza kustajabu labda heshima..nikiwa na maana kwamba msanii kama Mariah Carey bado ana heshima yake Kwa wapenzi wa Music,na hilo ndio tatizo kubwa Kwa wasanii wetu wa nyumbani,wanajishushia heshima zao wenyewe, mfano kuto kujitambua,personallity, usela kupita kiasi,I men hawa lindi heshima zao:.mfano wimbo wajuzi kati lady jd na na Nature,sjui unaitwa nn, maan kichefuchef hata kuukumbuka,kwamtu mwenyekulinda heshima yake asinge rekodi nyimbo ile au kukubali kushirikishwa..any way mengi yakusema ila (HESHIMA )wanakosa,ku shine si tatizo
 
Maisha ya jana na ya leo hayafanani hata kidogo,
Na uzee nao huooo!! unajongea.
 

Wakati si milele zimebaki story...!
 
Kwenye maisha kuna kupanda na kushuka, hakuna jipya
 
Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho...

Nakumbuka enzi hizo niko darasa la sita Kayumba alikuja Mkoani na Swebe wakawa wameamua kushuka kwenye gari na kutembea kwamiguu kuelekea hotelini iliyokuwa jirani na shule yetu wanafunzi wote shule nzima tulitoka nje kuwashangaa na kuwaacha walimu wakiduwaa tu na chaki zao. Baada ya hapo tuliambulia stiki na adhabu kisa Juma Nature na Swebe ambao leo hii hata akinipitia pembeni sigeuki kumshangaa lol!
 

Unaitwa KAMA JANA sio siri nimewadharau wote hasa verse ya mwisho ya nature.. Kweli uzee mbaya hasa ukiwa hauna Pension.
 
Nature hana kipaji Wala sio msanii wa kiwango...alitamba kwa sababu kulikuwa hakuna vipaji vikubwa those days
 
" those days" hata marais husahaulika wakimaliza muda wao...

Akina Musolin na Hitler waliteka habari za dunia wakapita... Tofauti ya hawa ni kuwa yamebaki matendo yao...

Ni jambo la kawaida hata Obama nae atapita na kubaki historia kama ilivyo kwa akina Kennedy ....Bill Clinton et al imebaki heshima na historia tuu...

Hivyo hata ndomo anayejitapa atavuma miaka mia atapita tu cha muhimu ni kujipanga kwa maisha ya mbele na kuacha cha maana kitakachokumbukwa na jamii....
 
Nature hana kipaji Wala sio msanii wa kiwango...alitamba kwa sababu kulikuwa hakuna vipaji vikubwa those days

Unasema? Hana kipaji? Enzi hizo hakukuwa na vipaji? Mzima kweli wewe?...nature alitamba kipindi cha kina jay,sugu,lady jaydee, mr paul,ay, solo, afande nk!ina maana hao jamaa hawana vipaji?..na hata hao unaowaona wana vipaji sasa walianza kuimba kwa style ya juma nature.nakuhakikishia nature akipanda jukwaani na hao watoto wenzio lazima awafunike. Wao wapige albam nzima kisha nature apige moja tu.. hili game.. halafu utazame jukwaa
 
Bro uko sahihi sana,guys nature akipanda na hili game,sidhan kama kuna mtu atafunika na jamaa ana kitu flan special yan akipanda jukwaan ana maneno yake lazima yakufanye ufurahi kwenye show
 
Kwenye music industry kuna kitu kinaitwa music cycle ku-justify uhalisia wa kua ni ngumu na haiwezekani kukaa kwenye peak kwa muda wote,Nature alitoa albamu ya kwanza mwaka 2000 "Nini Chanzo" na ukitrace back alianza kufanya muziki nyuma ya mwaka 2000 so ana almost 15 years kwenye hii industry na bado anafanya show mpaka kesho tena sio za kubahatisha ninachoamini Nature hayupo kwenye peak fo the time being ila bado anafanya vizuri nikihesabu wasanii kibao waliopotea kabisa ambao alianza nao au wengine walimkuta kwenye game lazima tukubali kua Nature ni mmoja kati ya ever green mcee hapa Bongo kwa maana hapotei na kusahulika pamoja changes nyingi zinazoendelea kwenye music industry na bado naamini hawa wanaovuma sasa ivi watakuja kufutika wakiiwaacha hawa ever green hapo walipo ingawa najua Nature hawezi kufanya kufikia level yake ya kitambo ila naamini bado ataendelea kuwepo leo na kesho,BTW sijawahi kukosa kununua albamu ya huyu jamaa toka ile ya kwanza na naendelea ku-support kazi na harakati za Kibra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…