BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Mtume Muhammad (s.a.w) anatujulisha mambo mawili muhimu yanayofanya siku ya ijumaa iwe bora miongoni mwa siku za juma. Kwanza ni kwamba, hii siku ya Ijumaa ndiyo aliyoumbwa Adamu. Pili ni kwamba siku hii ya ijumaa, baada ya Adamu kumkosea Mwenyezi Mungu aliomba msamaha na toba yake ikapokelewa. Tunahitaji kuyaangalia mambo haya mawili kwa kina zaidi ndani ya vitabu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu.