Jumaa Kareem, Ijumaa ni siku ya furaha kwa Waislamu wote, Hakikisha leo unafika Msikitini

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Mtume Muhammad (s.a.w) anatujulisha mambo mawili muhimu yanayofanya siku ya ijumaa iwe bora miongoni mwa siku za juma. Kwanza ni kwamba, hii siku ya Ijumaa ndiyo aliyoumbwa Adamu. Pili ni kwamba siku hii ya ijumaa, baada ya Adamu kumkosea Mwenyezi Mungu aliomba msamaha na toba yake ikapokelewa. Tunahitaji kuyaangalia mambo haya mawili kwa kina zaidi ndani ya vitabu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu.

 
Kiama kitatokea siku ya Ijuma kati ya swala ya Ijuuma na swala ya Asr... kwahiyo tujiandae wakati wowote kitukute tukiwa wasafi na wenye kufanya ibada.
 
Ijumaa Karim. Mtukumbuke wote kwenye sala msitusahau. Pia muombe sala amani itawale duniani na mfumuko wa bei ushukee.
 
Kiama kitatokea siku ya Ijuma kati ya swala ya Ijuuma na swala ya Asr... kwahiyo tujiandae wakati wowote kitukute tukiwa wasafi na wenye kufanya ibada.
Porojo hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…