Jumanne Muliro: Askofu Gwajima akitaka, akate rufaa (rufaa inakatwa kwa Waziri Bashungwa)

Jumanne Muliro: Askofu Gwajima akitaka, akate rufaa (rufaa inakatwa kwa Waziri Bashungwa)

jitu zinzi na liongo kama hilo haliwezi mtumishi wa Mungu, huenda ni wakala wa shetani šŸ’
Lakini kumbuka Mtume wenu Magufuli alimpa Ubunge na UNEC na kuhusu ngono CCM ni kama Ibada maana mnampaka Msagaji Mkuu.
 
Ungekuwa Msikiti usingefungiwa
Acha kuingiza udini, akina Sheikh Ponda na wenzake walikula chuma kipindi gani na waliwekwa kolokoloni kipindi Cha mtawala wa dini gani, Mambo ya usalama wa nchi hayaamuliwi Kwa mihemko wa dini, ukizingua chuma tu
 
Shekhe panda alipigwa risasi,Hakuna udini,Ukifanya kosa taratibu zitakufuata.
Kama ni kosa apigwe risasi Gwajima siyo kufungia kanisa. Msikiti upi ulifungwa kwa kosa la Ponda?
 
Acha kuingiza udini, akina Sheikh Ponda na wenzake walikula chuma kipindi gani na waliwekwa kolokoloni kipindi Cha mtawala wa dini gani, Mambo ya usalama wa nchi hayaamuliwi Kwa mihemko wa dini, ukizingua chuma tu
Tumia akili.
Ponda alipokamatwa msikiti upi ulifungiwa? Kama ni kosa awajibike Gwajima kama alivyowajibika Ponda na siyo kufungia kanisa. Udini unakupogusha.
Ajenda yenu inajulikana. Wala msijifiche
 
Gamboshi hivi hakuna mwamba anaeweza kufutilia mbali huyu Samia ,wao walimuondoa Magufuli na sisi tumwondoe Samia.Walahi nimejikuta nina Putin mentality.
 
i vema kutambua kwamba Katika muktadha wa Tanzania, utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kufuta dhehebu au jumuiya ya kidini unategemea masharti yaliyowekwa chini ya sheria na kanuni husika na siyo hisia au msukumo wa kisiasa wa mtu na hasa kwa kuzingatia

1. Sheria ya Jumuiya za Kijamii (The Societies Act), Sura ya 337 (Revised Edition)

Sheria hii ndiyo inayosimamia usajili, uendeshaji, na uvunjaji wa jumuiya zisizo za kiserikali, zikiwemo jumuiya za kidini.

Mamlaka ya Msajili:

Msajili wa Jumuiya za Kijamii (katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) ndiye mwenye mamlaka ya kusajili na kufuta jumuiya, ikiwa ni pamoja na madhehebu ya kidini.Kwa hiyo kwa sheria hii anaweza kuonya,kuelekeza,au kusitisha lakini kwa kuzongatia masharti ya sheria na Katiba ya nchi.

Utaratibu wa Kufuata Kabla ya Kufuta Dhehebu:Msajili atatoa ilani au barua kuitaka dhehebu au taasisi

(i) Kuwasilisha Sababu za Kufuta (Section 12–14 of the Societies Act):

Msajili anatakiwa kuonesha sababu za kisheria zinazomfanya atake kufuta usajili wa dhehebu, kama vile:

1. Dhehebu limejihusisha na shughuli zisizo halali au za kuhatarisha usalama wa taifa;

2. Limeshindwa kufuata masharti ya usajili;

3. Linahatarisha amani, maadili au umoja wa kitaifa;
4. Limeshindwa kuwasilisha taarifa za kila mwaka kama inavyotakiwa.

Kuwasilisha Ilani
(Notice) ya Kufuta:

Kabla ya kufuta dhehebu, Msajili anatakiwa kutoa ilani rasmi ya maandishi (Notice of Intention to Cancel) kwa uongozi wa dhehebu husika, kwa kawaida kwa muda wa siku 30, akiwaeleza sababu na kuwapa nafasi ya kujibu au kujitetea.

Haki ya Kusikilizwa (Right to be Heard – Audi Alteram Partem):

Kwa mujibu wa kanuni ya haki ya kimsingi ya kisheria, dhehebu linapaswa kupewa haki ya kusikilizwa.

Msajili hana mamlaka ya kufuta bila kutoa fursa ya kusikilizwa kwa wahusika (fair hearing).

Mapitio au Rufaa ya Maamuzi (Judicial Review/Appeal):

Iwapo dhehebu linaona limefutwa isivyo halali, linaweza kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana na wasiporidhika kufungua shauri la mapitio (judicial review) katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga hatua hiyo,

Ufafanuzi wa Kikanuni (kwa baadhi yadhehebu):

Kwa madhehebu yanayohitaji kibali kutoka kwa taasisi nyingine (k.m. Baraza la Maaskofu CCT au Mufti Mkuu), Msajili pia hufuata taratibu za kushauriana na vyombo hivyo kabla ya kuchukua hatua.

Taratibu zingine za ndani:

1. Ukaguzi wa mali na hesabu;
2. Mkutano wa wanachama kujadili hatma;
3. Kufungwa kwa ofisi rasmi.

MUHIMU:

Kwa mujibi wa sheria Msajili haruhusiwi kufuta dhehebu kiholela. Lazima afuate mchakato wa kisheria unaojumuisha ilani, sababu za msingi, haki ya kusikilizwa, na fursa ya kupinga maamuzi yake.

Kufuta bila mchakato huo ni kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 13(6)(a) kuhusu haki ya Kusikilizwa

Msajili wa Jumuiya hizi ni aliye elimika na anajua fika kuhusu tararibu na vyote anavyotakiwa kufanya. Kweli kwa akili zake anaweza ameweza kutoa barua hiyo au ndio nishajijibu mwenyewe kwa D2?šŸ˜‚šŸ˜…šŸ˜…



from senior member wa jf
 
MUNGU akitaka kukuangusha cha Kwanza atakupa kibri na Msumari wa Mwisho uwa ni Upofu ndo kwisha hapo
 
Hakuna kukata rufaa, vita dhini ya ukristo ishatangazwa rasmi..watawala muwe tayari - CDM pumzikeni sasa ni vita vya makanisa na ukristo

Yaani kiongozi wa dini kusema kuna watekaji nchini inakuwa nongwa?? Unafikia hatua ya kulifunga kanisa.
 
Ngoja nimtetee kidogo, "kazi yake ni kusimamia sheria " ila asimamie kwa kutenda haki.
Ikivi
Asingeweza.
Katolic, Lutheran na sabato kidogo labda usumbuane na viongozi ila sio kuyafungia sababu nao wanafanya kazi kama serikali, sio yale makanisa yanayomilikiwa na mchungaji. Ukifungia kanisa katolic joto utakalopata kesho utafungua na kuomba radhi.
Ubataka kusema nn
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
1 Petro 3:12-14
[12]Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
Na masikio yake husikiliza maombi yao;
Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.
[13]Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?
[14]Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.

Asubuhi ya leo tukatafakari maandiko kutoka katika kitabu cha waraka wa 1 wa Petro

Haki huinua Taifa kupigania haki ni swala la kiimani zaidi lina swawabu ndani yake
Endeleza mafumbo kanisa ndo lishafungwa akatoe press makao makuu chadema
 
Back
Top Bottom