Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Kauli ya Madam Rita kwa Media ya Mike 360
-------
Kitendo hicho ni kinyume na misingi ya maadili ya taaluma ya habari, na kinadhihirisha dharau, ukosefu wa adabu pamoja na kutokujali wajibu wa kuheshimu vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla.
JUMIKITA inasisitiza kuwa taaluma ya habari inapaswa kulindwa, kuheshimiwa na kuenziwa na wadau wote bila kujali nafasi au hadhi ya mtu katika jamii.
Kutokana na tukio hilo, JUMIKITA inatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kusitisha kumpa ushirikiano Madam Rita hadi pale atakapojitokeza hadharani kuomba radhi kwa umma pamoja na chombo cha habari kilichoathirika.
Imetolewa na:
Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA)
================