JUMIKITA: Media zisimpe tena ushirikiano Madam Rita

JUMIKITA: Media zisimpe tena ushirikiano Madam Rita

Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) imetoa wito kwa vyombo vya habari kutompa ushirikiano Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production, Rita Paulsen (Madam Rita), hadi atakapoomba radhi kufuatia kauli aliyotoa dhidi ya chombo cha habari ambayo wameeleza si ya kiungwana.

JUMIKITA imesema kitendo kilichofanywa na Madam Rita kinadhihirisha ukosefu wa adabu pamoja na kutoheshimu vyombo vya habari.

View attachment 3575921

Alichokisema Madam Ritha hadi barua hiyo kutolewa:

Hana kosa yupo sahihi 💯 media za bongo ni takataka
 
Si lazima kila mtu akubali kila chombo cha habari.

Madam kaweka standards zake, vi media anavyoviona vya uchwara uchwara kavikataa.

Ana sababu zake, ziheshimiwe.

Aachwe afanye kazi na media anazozikubali ambazo nazo zinamkubali.

Tatizo liko wapi?

Taaluma ya habari kulindwa maana yake si kila mwanahabari kulazimisha interview na kila mtu, especially kama mtu mwenyewe si kiongozi wa kiserikali au public servant.

Wanahabari hamuelewi vipi mtu kukataa kuongea nanyi ni haki yake ya kikatiba na kibinadamu?
Trump huwa anaziita
fake news na waandishi wao hadharani kabisa, sijaona wakitaka kususa.

Kuna muda hata maswali yao hajibu kabisa.Hamna cha ajabu alichofanya Madam Ritha.
 
Yess ni haki yake kusema hivo japo kwenye uwasilishaji amewasilisha kidharau flani hivi.....kwa upande wangu siwezi kulala kwenye vigest uchwara uchwara vya 5000🤣🤣🤣
 
Aisee, mwandishi naona kajihisi yeye ni kama Pimbi tu, maneno makali Sana Yale angemwambia Tu kistaarabu mbona wengine wanaongea Tu ukweli lakini WA kiistarabu.
 
Trump huwa anaziita
fake news na waandishi wao hadharani kabisa, sijaona wakitaka kususa.

Kuna muda hata maswali yao hajibu kabisa.Hamna cha ajabu alichofanya Madam Ritha.

Trump muhuni tu.

Kwa Trump kuna standard tofauti kwa sababu Trump ni rais, kachaguliwa na watu. Anapoongelea media inambidi awe muangalifu zaidi kwa sababu yeye ni kiongozi wa kupigiwa kura na wananchi.

Hata Madam Rita angekuwa mbunge kwa mfano, standard za kumtaka aongee na waandishi wa habari zingekuwa za juu zaidi.

Ila Madam Rita kama mtu asiye kiongozi wa kupigiwa kura ana haki kubwa zaidi ya kukataa kuongea na media.
 
Yess ni haki yake kusema hivo japo kwenye uwasilishaji amewasilisha kidharau flani hivi.....kwa upande wangu siwezi kulala kwenye vigest uchwara uchwara vya 5000🤣🤣🤣
Hata kuwakilisha kidharau ni haki yake pia.

Hivyo vigesti unaweza kuona vya bei chee, halafu vikakuletea kunguni mpaka nyumbani.
 
Trump huwa anaziita
fake news na waandishi wao hadharani kabisa, sijaona wakitaka kususa.

Kuna muda hata maswali yao hajibu kabisa.Hamna cha ajabu alichofanya Madam Ritha.
Not entirely true.

Kuna wakati baadhi ya networks zilikuwa hazirushi hotuba zake kwa sababu alikuwa anadanganya sana.

Pia, hata mitandao ya kijamii ilimfungia. Na hii ndo ikawa sababu ya yeye kuanzisha mtandao wake wa Truth Social.
 

Kauli ya Madam Rita kwa Media ya Mike 360


-------

Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) kupitia Mwenyekiti wake, Ndugu Shaaban Matwebe, imesikitishwa na kulaani vikali kitendo kisicho na heshima wala uungwana kilichofanywa na Madam Rita dhidi ya chombo cha habari cha mtandaoni.

Kitendo hicho ni kinyume na misingi ya maadili ya taaluma ya habari, na kinadhihirisha dharau, ukosefu wa adabu pamoja na kutokujali wajibu wa kuheshimu vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla.

JUMIKITA inasisitiza kuwa taaluma ya habari inapaswa kulindwa, kuheshimiwa na kuenziwa na wadau wote bila kujali nafasi au hadhi ya mtu katika jamii.

Kutokana na tukio hilo, JUMIKITA inatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kusitisha kumpa ushirikiano Madam Rita hadi pale atakapojitokeza hadharani kuomba radhi kwa umma pamoja na chombo cha habari kilichoathirika.

Imetolewa na:
Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA)
Hii JUMIKITA(it's my first time kusikia) ilikuwa wapi wakati hivyo vi-media uchwara na mainstream media kwa makusudi kabisa zikaacha kuripoti mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Samia pamoja na genge lake, Watanganyika wanatekwa kila uchwao, kufirwa na kuuawa huwa inakuwa wapi hiyo organisation koko.
Anyway, ni vita vya chawa wenyewe kwa wenyewe acha waendelee kupopoana.
NB: Ritta ni maarufu na ana influence zaidi ya hako kakikundi koko.
 
Huyo bibi hajafanya vyema kuwajibu vijana wapambanaji kuwa ni uchwarwa ni majibu ya kuvunja moyo
Kama kweli ni vi-media uchwara ulitaka awe mnafiki?
NB: Rita naye ni chawa uchwara hana tofauti na hako ka-media uchwara.
 
Hizi media zingepambana kufichua uovu kama wafanyavyo JF tungefika mbali…
Sasa angalia wanaptomote kitu hakina kichwa wala miguu
 
Back
Top Bottom