Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Haongei na media uchwara uchwara............Rita amefanya nini?
Si lazima kila mtu akubali kila chombo cha habari.
Kauli ya Madam Rita kwa Media ya Mike 360
-------
Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) kupitia Mwenyekiti wake, Ndugu Shaaban Matwebe, imesikitishwa na kulaani vikali kitendo kisicho na heshima wala uungwana kilichofanywa na Madam Rita dhidi ya chombo cha habari cha mtandaoni.
Kitendo hicho ni kinyume na misingi ya maadili ya taaluma ya habari, na kinadhihirisha dharau, ukosefu wa adabu pamoja na kutokujali wajibu wa kuheshimu vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla.
JUMIKITA inasisitiza kuwa taaluma ya habari inapaswa kulindwa, kuheshimiwa na kuenziwa na wadau wote bila kujali nafasi au hadhi ya mtu katika jamii.
Kutokana na tukio hilo, JUMIKITA inatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kusitisha kumpa ushirikiano Madam Rita hadi pale atakapojitokeza hadharani kuomba radhi kwa umma pamoja na chombo cha habari kilichoathirika.
Imetolewa na:
Jumuia ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA)
Mkuu,Nalitazama suala hili kwa pande mbili, moja kama dharau na ina impact kwa aliyedharauliwa na aliyedharau. Mbili ninatazama suala hili kama ubinadamu. Ni vizuri kujua kuwa watu hukosea na pengine hata yeye anajuta kwa kusema hivo.
Nb: Maneno yako yanaweza kuwa mlango au kuwa kifungo kabla hujaongea fikiri kwanza.
Sometimes mtu lazima uwe na standards.Haongei na media uchwara uchwara............
Huyo bibi hajafanya vyema kuwajibu vijana wapambanaji kuwa ni uchwarwa ni majibu ya kuvunja moyo
Yeah ni kweliMkuu,
Kuna upande wa mtu kutumia haki yake pia, na mtu kutumia haki yake kukataa kuongea na media fulani, au kuiita media fulani ya uchwara, si kukosea.
Hiyo ni haki yake.
Ila Watanzania wengi wameharibiwa na Ujamaa mpaka mtu akitumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu tu, tunamuona kakosea.
Huyo unaweza kukuta anaona kashanukuliwa vibaya, kashawekewa habari ndivyo sivyo, na pengine ana sababu ya muhimu tu ya kukataa kuongea na "vimedia vya uchwara uchwara".Yeah ni kweli